Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,804
- 10,715
- Thread starter
- #521
Suala la punyeto aisee mwalimu umeeleweka na miongon mwetu ukianzia mimi mwenyw maarifa haya yamenisaidia KUACHA kabisa punyeto.
Nilikua na sababu nyingi za kuitetea lkn kupitia maarifa niliyoyapata humu nasema no, punyeto is very dangerous thing.!
Nimekuita mwalimu kwa sababu wanasema Learning is a permanent change behavior of the learner.
Huwezi kujifinza kama hakuna mwalimu ndio maan katika karama tano na mwalimu yupo.!
Kiufupi huko mi nimetoka kabisa na siwezi kurudi tena hata iwaje, is better i die without punyeto rather than living like msukule.!![emoji2][emoji2][emoji2]
This is another amoung of achievement that i made this year 2020.!
Sasa naomba kufahamu zaid kuhusu kujihusisha kimapenz na mtu asiye wako.
Correct me if i am wrong,
Kwa jinsi nilivyosoma nimeona madhara ya kufanya mapnz nje ya mke wa ndoa ni makubwa kama utakua unalala na wanawake wengi especially makahaba/ barmaids.
"nguvu za mwanamke zimo ndani ya mwanamume, kwa sababu mwanamke ni sehemu ya mwanamume. Mwanamume alalapo na mwanamke huachilia nguvu zake za uumbaji ndani ya mwanamke, naye huzihifadhi nguvu hizo ndani yake, ukizingatia kwamba hawa wawili ni mwili mmoja na roho moja. Kwa hiyo nguvu hizo HAZIPOTEI umpapo mkeo, bali katika roho bado ni zako tu."
Nashukuru mkuu kwa ukiri wako. Mimi naachilia ujumbe tu kama nilivyopokea, afanyaye kazi ya kumbadilisha mtu ni Roho Mtakatifu. Sifa na utukufu kwa Mungu wetu. Mimi pia nilipotea kama wewe, lakini majira yangu yalipofika niliiona kweli na tangu hapo sijaiacha. Naomba nifafanue sasa kadri ulivyouliza:
Naomba kuuliza kutokana na sehemu ya ujumbe wako,
1. Je mwanamke ambaye hajaolewa/hafanyi mapenzi atakua na nguvu chache ukilinganisha na yule aliye olewa ambaye hupokea nguvu kutoka kwa mumewe?
Kumbuka kuna nguvu za aina tatu. Kwanza kuna nguvu za kimwili, hili liko dhahiri. Kiasili mwanamke ni dhaifu ukilinganisha na mwanamume, lakini hoja yangu haiko hapa.
Pili ni nguvu za kiroho. Mwanamke alitolewa toka mwanamume, akawa nafsi huru. Kwa hiyo roho yake ni roho kamili kabisa, ndio maana itasimama kwenye hukumu. Pia anaweza kuomba na akaungana na Mungu kama ilivyo kwa mwanamume. Nguvu za kiroho ni kwa mwanamume na mwanamke.
Tatu ni nguvu za uumbaji. Hapa ndipo hasa nilipogusia. Nimesema wazi kuwa mwanamume huachilia nguvu ya uumbaji kisha mwanamke huipokea. Kimwili tunaona shahawa, lakini kiroho iko nguvu nyingine zaidi. Hiyo ndio emotional energy ambayo huleta mvutano kati ya mwanamke na mwanamume. Mwanamume ameumbiwa kupenda, mwanamke yeye hupendwa. Sasa nguvu ya mahusiano imo ndani ya mwanamume, ambaye huiingiza kwa mwanamke kupitia hisia (emotions) mpaka pale mwanamke anapojaa nguvu hiyo ndipo hujikuta akivutika kwa mwanamume huyo. Jiulize ni kwa nini mwanamke aweza kumkataa mwanamume kwa miezi mingi tu, lakini aking'ang'ania mwishowe hukubaliwa? Ndipo sasa hukamilisha tendo la uumbaji kwa kulala pamoja. Turudi kwenye swali:
Binti asiyeolewa bado, atakuwa na nguvu ndogo za uumbaji kwa kutazama emotion. Mwanamke asiyeamsha mapenzi anaweza kukaa miaka mingi bila kutamani kuingiliwa. Nguvu ya hisia huamshwa na ngono, pale mwanamume anapoingiza nguvu zake, ndipo utaona mwanamke hugeuka mtumwa wa mwanamume.
2. Je nisipozini na wanawake wengi mfano, mfano. Mke wangu yupo Mtwara na mimi nipo Dodoma, kuonana mpaka miezi kadhaa ipite kulingan na uchumi let say miezi 4, nikaamua kutafuta mwanake mmoja tu mahali nilipo je ataniletea madhara ya kupoteza nguvu?
Naam, huo ni uzinzi. Kumbuka mkeo ndio hazina yako. Sasa unapoweka akiba yako kwenye akaunti ya mtu mwingine haijalishi kama ni moja ama tano. Tayari umetapanya akiba yako. Tena unaleta vurugu kwenye ulimwengu wa roho kwa sababu una mafungamano na mkeo wa ndoa, ninyi ni nafsi moja. Sasa nikujulishe tu, ukifanya hivyo, utakuwa umelegeza kifungo cha ndoa, hivyo mkeo naye atajisikia upweke na haja ya kupata mtu wa kumliwaza usipokuwapo. Hilo liweke kichwani kabisa. Tena huyo mwanamke utakayemtwaa atakuwa na watu wengine waliomwingilia, hivyo nawe unakwenda kuongeza nafsi yako humo huku ukivuna roho wachafu watakaoiyumbisha ndoa yako.
3. Kwa nini manabii wa zamani walikua na wanawake zaidi ya mmoja na bado hawakuhesabika ni kosa, je sheria ya kupoteza nguvu kwao haikufanya kazi?
Wako manabii waliotumikia ofisi ya nabii pekee. Hawa ni kama Isaya, Yeremia, Ezekieli nk. Katika hawa HUWEZI KUONYESHA yupi alikuwa na wake wengi.
Halafu wako waliokuwa na madaraka tofauti licha ya kupokea unabii nyakati fulani mfano ni Gideoni aliyekuwa kamanda wa kijeshi na mwamuzi pia, Samweli aliyekuwa kiongozi wa Waisraeli na kuhani na nabii, halafu wapo wafalme kama Daudi, Suleiman nk. Hawa wote walikuwa na wake wengi.
Hoja hapa ni WAKE ZAO AMA MAKAHABA? Hiki na kipindi ambacho Mungu aliumba macho watu wakajitwalia wake wengi. Lakini siri kubwa ilikuwa kwenye BIKIRA. Mke alipaswa kuwa bikira ili myme awe pekee mwenye kuhifadhi nguvu zake humo. Kasoro ni moja tu, nabii Hosea, huyu alipewa maelekezo maalum akaoe KAHABA. Huyu ndiye nabii wa zama zetu sisi. Msome halafu urudi jukwaani tujadili. Lakini pia nikutonye kitu, je uliona mwisho wa Daudi tangu alupotembea na mke wa Uria? Soma kisa hiki ili uone kama nguvu zake kiroho (mahusiano yake na Mungu) zilibaki sawa. Pia ujiulize kwa nini basi Mungu akamzuia adimjengee nyumba yake!!
4. Kusex na mke wako huku umevaa kondomu je ni kosa??
Maana zile sperms ( nguvu) zitakua hazijaingia kwake na kuzitunza ambazo zinahesabika ni zako.
Pia labda naomba kujua nguvu unazozungumzia hapa Ni zipi?
Yesu Kristo alisema, ukimtazama mwanamke kwa kumtamani basi umezini naye. Sasa jiulize, nguvu ni shahawa? NO. Zile hisia za ndani hukamilisha tendo ndipo uthibitisho wa mwilini hufuatia. Ndio maana tunaambiwa sex ni tendo la kiroho.
Kumbe hata ukivaa kondomu, ngono tayari hukamilika pale mnapotamaniana. Sasa unapomwaga nje ya kizazi ni dhambi. Ni kama wamwagao mdomoni. Tumia njia za asili za uzazi, kalenda. Binafsi sijawahi kudhani kuna wanandoa hutumia kondomu. Lakini muhimu ni kutumia kalenda.