Nguvu ya Punyeto na kujichua katika Ulimwengu wa Roho


Nashukuru mkuu kwa ukiri wako. Mimi naachilia ujumbe tu kama nilivyopokea, afanyaye kazi ya kumbadilisha mtu ni Roho Mtakatifu. Sifa na utukufu kwa Mungu wetu. Mimi pia nilipotea kama wewe, lakini majira yangu yalipofika niliiona kweli na tangu hapo sijaiacha. Naomba nifafanue sasa kadri ulivyouliza:


Naomba kuuliza kutokana na sehemu ya ujumbe wako,
1. Je mwanamke ambaye hajaolewa/hafanyi mapenzi atakua na nguvu chache ukilinganisha na yule aliye olewa ambaye hupokea nguvu kutoka kwa mumewe?

Kumbuka kuna nguvu za aina tatu. Kwanza kuna nguvu za kimwili, hili liko dhahiri. Kiasili mwanamke ni dhaifu ukilinganisha na mwanamume, lakini hoja yangu haiko hapa.

Pili ni nguvu za kiroho. Mwanamke alitolewa toka mwanamume, akawa nafsi huru. Kwa hiyo roho yake ni roho kamili kabisa, ndio maana itasimama kwenye hukumu. Pia anaweza kuomba na akaungana na Mungu kama ilivyo kwa mwanamume. Nguvu za kiroho ni kwa mwanamume na mwanamke.

Tatu ni nguvu za uumbaji. Hapa ndipo hasa nilipogusia. Nimesema wazi kuwa mwanamume huachilia nguvu ya uumbaji kisha mwanamke huipokea. Kimwili tunaona shahawa, lakini kiroho iko nguvu nyingine zaidi. Hiyo ndio emotional energy ambayo huleta mvutano kati ya mwanamke na mwanamume. Mwanamume ameumbiwa kupenda, mwanamke yeye hupendwa. Sasa nguvu ya mahusiano imo ndani ya mwanamume, ambaye huiingiza kwa mwanamke kupitia hisia (emotions) mpaka pale mwanamke anapojaa nguvu hiyo ndipo hujikuta akivutika kwa mwanamume huyo. Jiulize ni kwa nini mwanamke aweza kumkataa mwanamume kwa miezi mingi tu, lakini aking'ang'ania mwishowe hukubaliwa? Ndipo sasa hukamilisha tendo la uumbaji kwa kulala pamoja. Turudi kwenye swali:

Binti asiyeolewa bado, atakuwa na nguvu ndogo za uumbaji kwa kutazama emotion. Mwanamke asiyeamsha mapenzi anaweza kukaa miaka mingi bila kutamani kuingiliwa. Nguvu ya hisia huamshwa na ngono, pale mwanamume anapoingiza nguvu zake, ndipo utaona mwanamke hugeuka mtumwa wa mwanamume.

2. Je nisipozini na wanawake wengi mfano, mfano. Mke wangu yupo Mtwara na mimi nipo Dodoma, kuonana mpaka miezi kadhaa ipite kulingan na uchumi let say miezi 4, nikaamua kutafuta mwanake mmoja tu mahali nilipo je ataniletea madhara ya kupoteza nguvu?

Naam, huo ni uzinzi. Kumbuka mkeo ndio hazina yako. Sasa unapoweka akiba yako kwenye akaunti ya mtu mwingine haijalishi kama ni moja ama tano. Tayari umetapanya akiba yako. Tena unaleta vurugu kwenye ulimwengu wa roho kwa sababu una mafungamano na mkeo wa ndoa, ninyi ni nafsi moja. Sasa nikujulishe tu, ukifanya hivyo, utakuwa umelegeza kifungo cha ndoa, hivyo mkeo naye atajisikia upweke na haja ya kupata mtu wa kumliwaza usipokuwapo. Hilo liweke kichwani kabisa. Tena huyo mwanamke utakayemtwaa atakuwa na watu wengine waliomwingilia, hivyo nawe unakwenda kuongeza nafsi yako humo huku ukivuna roho wachafu watakaoiyumbisha ndoa yako.

3. Kwa nini manabii wa zamani walikua na wanawake zaidi ya mmoja na bado hawakuhesabika ni kosa, je sheria ya kupoteza nguvu kwao haikufanya kazi?

Wako manabii waliotumikia ofisi ya nabii pekee. Hawa ni kama Isaya, Yeremia, Ezekieli nk. Katika hawa HUWEZI KUONYESHA yupi alikuwa na wake wengi.

Halafu wako waliokuwa na madaraka tofauti licha ya kupokea unabii nyakati fulani mfano ni Gideoni aliyekuwa kamanda wa kijeshi na mwamuzi pia, Samweli aliyekuwa kiongozi wa Waisraeli na kuhani na nabii, halafu wapo wafalme kama Daudi, Suleiman nk. Hawa wote walikuwa na wake wengi.

Hoja hapa ni WAKE ZAO AMA MAKAHABA? Hiki na kipindi ambacho Mungu aliumba macho watu wakajitwalia wake wengi. Lakini siri kubwa ilikuwa kwenye BIKIRA. Mke alipaswa kuwa bikira ili myme awe pekee mwenye kuhifadhi nguvu zake humo. Kasoro ni moja tu, nabii Hosea, huyu alipewa maelekezo maalum akaoe KAHABA. Huyu ndiye nabii wa zama zetu sisi. Msome halafu urudi jukwaani tujadili. Lakini pia nikutonye kitu, je uliona mwisho wa Daudi tangu alupotembea na mke wa Uria? Soma kisa hiki ili uone kama nguvu zake kiroho (mahusiano yake na Mungu) zilibaki sawa. Pia ujiulize kwa nini basi Mungu akamzuia adimjengee nyumba yake!!

4. Kusex na mke wako huku umevaa kondomu je ni kosa??
Maana zile sperms ( nguvu) zitakua hazijaingia kwake na kuzitunza ambazo zinahesabika ni zako.
Pia labda naomba kujua nguvu unazozungumzia hapa Ni zipi?

Yesu Kristo alisema, ukimtazama mwanamke kwa kumtamani basi umezini naye. Sasa jiulize, nguvu ni shahawa? NO. Zile hisia za ndani hukamilisha tendo ndipo uthibitisho wa mwilini hufuatia. Ndio maana tunaambiwa sex ni tendo la kiroho.

Kumbe hata ukivaa kondomu, ngono tayari hukamilika pale mnapotamaniana. Sasa unapomwaga nje ya kizazi ni dhambi. Ni kama wamwagao mdomoni. Tumia njia za asili za uzazi, kalenda. Binafsi sijawahi kudhani kuna wanandoa hutumia kondomu. Lakini muhimu ni kutumia kalenda.
 
"Kasoro ni moja tu, nabii Hosea, huyu alipewa maelekezo maalum akaoe KAHABA. Huyu ndiye nabii wa zama zetu sisi. Msome halafu urudi jukwaani tujadili."

Nilikua hata sielewi kama Hosea alipewa agizo hilo, ngoja nikasome hii assignment nitarudi kueleza nilicho jifunza.

Kweli nimeelewa kwamba kumbe kuna madhara ya kufanya mapenzi nje ya ndoa.

Mbali na hukimu ya moto siku ya kiama pia Kuna strength za mwilin na rohon tunapoteza.!


Kwa ufahamu wangu nilifikiri Daudi aliyumba kwenye utawala wake baada ya kulala na yule mke wa askari kwa sababu kwanza alilala na mke wa mtu maana yake aliiba ambalo Ni kosa, pia kitendo cha kumtengenezea kifo yule bwana likawa kosa jingine kubwa kwa Mungu.

Tunamshkur Mungu ambaye kupitia wewe anatufunulia mambo mazito Kama haya, kwani yamejaa ufunuo wa hali ya juu na hekima ndani yake.

Suala la matumizi ya uzazi wa mpango nitauliza zaidi muda mwingine.
Hiyo njia ya kalenda nimeona wengi wanalalamik kupata watoto wasio tarajiwa maana menstrual hubadilik badilik kw baadhi ya wanawak kwa kawaida wengin wakisafir au wakiumwa na kupona homa.
 
Samson? Destroyed by a woman. David? Seduced by a woman. You know what happened to Adam. Moral of the story? Masturbate.

..in my humble opinion.
 
Daudi aliua, hiyo ni dhambi. Halafu alizini, hiyo ni dhambi na kuvunja agano. Katika dhambi zote kwenye Biblia ni dhambi moja tu ambayo tumeambiwa tuikimbie, ZINAA. Tena tumeambiwa dhambi zote hutendeka NJE YA MWILI, isipokuwa dhambi moja tu, ZINAA. Kuua hakuna agano, lakini zinaa ni dhambi ya agano, mnakuwa mwili mmoja.

Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu. Pia kumbuka Daudi hakuomboleza kwa kifo cha Uria, bali aligoma hata kupiga msosi kwa sababu ya mtoto wa zinaa. Mungu kwa kulijua hilo akaamua kumwondoa huyo mtoto.
 
Samson? Destroyed by a woman. David? Seduced by a woman. You know what happened to Adam. Moral of the story? Masturbate.

..in my humble opinion.
Hakuna mwanamke mwenye uwezo wa kumwangamiza mwanamume, bali ni ile nguvu nyuma yake. Samsoni alikiuka agizo la kutooa binti za mataifa, kilichofuata tunakijua. Daudi aliumizwa na tamaa zake mwenyewe, yule mwanamke hakuwa hata na mpango naye. Adamu aliumizwq na nguvu iliyokuwa nyuma ya Hawa. Shetani alishamwingia mwanamke.

Sasa unapotumia visa hivi kuhalalisha utumwa wako unakosea. Fanya kwa sababu umekusudia na sio vinginevyo. Kumbuka pia sote tumrtoka jwa baba na mama, hivyo wangetenda hayo huenda ungekuwa chooni saa hii
 
"alizini, hiyo ni dhambi na kuvunja agano. "

Dah, Ni hatari, Mungu nisaidie nishinde haya Mambo maana impacts zake Ni kubwa San.
After all siku zenyw zimebaki chache za kutenda mambo mema.

Nashkur Sana kwani binafsi umenifunza Mambo mengi Mr. Nyenyere.
Wengi tulichukulia kufanya mapenzi na mtu asiye wako ni dhambi, lkn kumbe Kuna madhara Zaid ya dhambi ukiwa bado dunian, tuliichukulia simple kwa sababu haileti madhara kwa yeyote both involved mnainjoy, lkn kumbe inaonekana Ni dhambi kubwa zaidi kuliko nyingine kwa jinsi nilivyo elewa mimi kutokan na maandiko na maelezo yako mkuu.

Nasubir nondo za uzazi wa mpango siku ukiwa na mda tunaomba utushushie hapa.

Binafsi Mara nyingi i use kondom japo huwa mke siishi naye kwa muda mrefu yupo mbali.
Dawa zinasemekan zina madhar kiafya hata yeye huwa hataki kabisa, kalenda tunahofia kupata mtoto wa pili wakati mambo yetu ya kimaisha hayajakaa vzr.

Kimsingi hata Mimi sipend kondom lkn nalazimika, nimejaribu kuuliza kwa wakubwa wangu hawatoi jibu straight. Kuna baadhi niliona wanalalamikia kalenda imewaingiza chaka.!

Unaweza ukauanzishia uzi wake au hata hapa Ni vema pia naamin nitajifunza/tutajifunza.
 


Ulikaa mda gan mkuu ukarudi normal?
 
Ulikaa mda gan mkuu ukarudi normal?
Kwangu mimi ni kama kitu kiligusa moyo wangu na kuibadili nia yangu kabisa. Nilitokea kukuchukia hicho kitendo na tangu hapo sijawahi kurejea nyuma. Ni miaka kadhaa sasa sina kabisa hamu ya kujichua.
 
[emoji38][emoji38][emoji38] sawa mkuu
Njia za uzazi wa mpango ni dhambi??

Naomba kufahamishwa zaidi Biblia inasemaje juu ya uzazi wa mpango. Nipo tayari kujifunza zaidi.
 
Kuna ubaya Gani mtu kujishika sehemu zake kwa starehe zake binafsi?, Kati ya madhara ya Punyeto na uzinzi yepi yana Unafuu?
Kuliko mtu kuhatarisha Afya yake na future yake kwenye uzinzi, mi naona Bora kujishika aisee.. it's fun and less expensive!!
Tatizo linaanzia hapo je upo tayari kuacha usije na hoja za kuhalalisha mkuu
 
naona yule universal wa kuchukua sperm ztu kashafika..
 
demu anatembea na wanaume zaidi ya kumi eti na ww unamtumia huo uchafu nani atavumilia bora punyeto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…