...........
²⁰ Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
²¹ Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
²² Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
Kumbe Mungu aliwabariki hata wanyama pia, ila baraka zao ziko tofauti na mwanadamu. Wanyama wao walipewa NGUVU ya kuijaza nchi na bahari tu, wala hawakupewa KUITIISHA, YAANI kuwa watawala. Ni kwa kutumia nguvu hiyo wanatambua majira ya mwaka, wanajua wapi wapate maji ama chakula waweze kuendeleza nguvu ya kuijaza dunia. Ukitaza Simba kwa mfano: nguvu yake huthibitika kwa kuyamiliki majike, ndio maana huwezi kukuta madume mawili yakawa ndani ya kundi moja. Hakika mmoja lazima auawe, ndipo zilipo baraka za Mungu,hapo penye kuujaza ulimwengu.
Kwa binadamu ikoje?
.........
²⁶ Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.[/I]
Kwa hiyo kwanza kabisa uumbaji wa mwanadamu ulikuwa tofauti, KWA SURA NA MFANO WETU. Hapo ndipo penye mvurugano mwingine wa kitafsiri, lakini ni rahisi tu. Sura ya Mungu ni HAKI YAKE (righteousness) na mfano wake ni kutawala kwa sababu Yeye ni mtawala wa vyote.
“Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.”
— Zaburi 17:15
“As for me, I will behold thy face in righteousness: I shall be satisfied, when I awake, with thy likeness.”
— Psalms 17:15 (KJV)
Hapo mzaburi anasema nikutazame uso wako katika haki, kila ninapoamka asubuhi NIRIDHIKE PALE NINAPOFANANA NA SURA YAKO. Ndivyo alivyo mwanadamu siku ya kuumbwa kwake. Tuendelee...
²⁷ Mungu akaumba mtu kwamfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Kumbe toka siku ya kuumbwa mwanamume, mwanamke pia aliumbwa!! Kwa vipi? Waliumbwa kwenye ulimwengu Wa roho, ni kama mjenzi anapoandaa ramani yake kwanza kisha iakiona ni njema hujenga.
Tena ona hapo inaposema Mungu aliumba MTU kwa mfano wake. Haisemi watu kana kwamba ni wengi, bali MTU!! Halafu inamsema huyo mtu wa mfano wa Mungu kuwa ni mwanamume na mwanamke. Hii inaonyesha wazi kuwa mwanamke na amwanamune walikuwa mwili mmoja toka kuumbwa kwao, hakuumba mwanamumebpeke yake na mwanamke peke yake, ok?
²⁸ Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Hapa Mungu akambariki huyo MTU aliyemwumba, alimwambia ZAENI.... Iweje wawe wengi? Ni kwa sababu Mungu alimwumba mtu mmoja mwenye sehemu mbili tayari,yaani alikuwa na roho moja yenye sehemu ya mke na mume ili kuwa kamilifu.
Kwa sababumwanadamu ni zaidi ya mnyama, akampa pia KUITIISHA DUNIA. Hapo ndipo nfuvu ya kutawala ilipokuja, kama Yeye alivyo mtawala. Kwa sura na mfano wake. Akampa jimbo la kutawala nalo ndilo dunia yetu.
.........
³¹ Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Baada ya kuumba katika roho akaona kila kitu kimekaa sawa kabisa, lakini kumbuka hakuna kitu kilichotokea physically bado. Ndipo tunasema kwa kuwa tu mfano wa Mungu, mambo yetu yanapaswa kuumbwa katika roho kwanza, kisha huja kudhihirika katika mwili.
Hiyo ni kanuni ya maisha ya mwanadamu tangu kuumbwa kwake, atawale kutokea rohoni (kumbuka mpaka hapo bado mwanadamu ni roho, hana mwili bado). Ndivyo alivyoishi Yesu Kristo kwani alisema wazi, hakuna neno alilisema isipokuwa amemsikia Baba akilisema. Kwamba hakuenenda kwa kuangalia mambo ya duniani bali kusikiliza mambo ya rohoni ambayo ndiyo yanayomwongoza kuitawala dunia.
Tuendelee.....[/I]