Mandela5599
Member
- Jul 28, 2020
- 93
- 306
Mchakato wa handshake (maridhiano ya kisiasa nchini Kenya) yalikutanisha makundi hasimu ya kisiasa kati ya Rais Uhuru Kenyatta kwa upande wa Jubilee na mpinzani Raila Odinga.
Binafsi mwanzoni nilitazama kama mbinu ya kisiasa ya kuua upinzani Kenya, kwamba Ruto na Kenyatta walitengeza mgogoro fake ili kudhoofisha nguvu ya Raila Odinga kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2022
Handshake imepooza nguvu ya upinzani Kenya, wamekosa nguvu ya kuhoji mambo ya msingi ya taifa lao kwa sababu ni kama wamekua sehemu ya serikali.
Kuanza kwa mchakato huu mwanzoni Ruto aliunga mkono ila baadae walipotaka usiishie njiani na kutaka uwe sehemu ya katiba Ruto alijitenga na kuanza kuupinga.
Mahakama Kuu kuitupilia mbali BBI ni ushindi kwa Ruto na jinsi mwitikio mkubwa wa wakenya kuunga mkono maazimio ya mahakama ulivyo mkubwa ni dhahiri kwamba Ruto amepata nguvu zaidi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.
Mahakama kuwa na nguvu ya kimaamuzi ni jambo la muhimu sana kwa maendeleo ya taifa. Majaji kutumia taaluma na maadili ya utumishi wao kwa wananchi kufanya maamuzi bila kuingiliwa na mhimili mwangine ni hatua kubwa sana ambayo Tanzania tunatamani kufika huko. Hivi ingekua Mahakama ya Tanzania imekataa mtazamo wa Rais ingekuaje??
Maamuzi ya kubadilisha mfumo unatuhusu mimi na wewe!! Tuamue sasa