Uchaguzi 2020 "Nguvu ya umma" itaamua uchaguzi huru na haki mwaka huu

.
 
Ushindi utaibiwa mara ngapi Zanzibar hadi wazanzibari kusema tumechoka? Mara moja ,mbili ,tatu,nne, tano ? No sixth my friend listen to the wind.
 
Mnyika ni failure, sijui kwanini hata waliamua kumpa Ukatibu mkuu.
CHADEMA wao walishasema hawazingatii elimu Dunia.. Kwa hiyo wanaokoteza mwanachama yeyote mwenye umaarufu na kumkasimisha majukumu makubwa bila kujali uwezo wake!
 
Mnyika ni failure, sijui kwanini hata waliamua kumpa Ukatibu mkuu.
Mnyika tulisoma nae Mlimani mwanzoni mwa miaka ya 2000 ila kuna mtu alisema jamaa kumbe haku graduate!! wenzake hatukujua!!! nakumbuka tukiwa wanafunzi pale tulimpigania akagombea ubunge wa ubungo na kushindwa!!!
 
tulisoma nae Mlimani mwanzoni mwa miaka ya 2000 ila kuna mtu alisema jamaa kumbe haku graduate!! nakumbuka tukiwa wanafunzi tulimpigania akagombea ubunge wa ubungo na kushindwa!!!
ndio hivyo mkuu. Ubungo palimshinda, akakimbilia Kibamba napo ameshindwa vibaya zaidi , wapinzani saa nyingine wanapopewa huruma na wananchi wanaishia kuwa dissappoint wapiga kura wao
 
Nguvu ya Umma ilipaswa kutumika mwaka 2015.. Mwaka huu ile Morali ya Umma imefifia sana, sidhani kama nguvu ya Umma itakuwa na nguvu dhidi ya Nguvu ya Dola.

Too late.
 
Nguvu ya umma?!? Umma upi?
 
CHADEMA,

Kwa kutumia nguvu ya Unma, ndiyo njia pekee ya kukabiliana na hao CCM, ambao wao wanaamini kuwa vyombo vyote vya dola viko upande wao.
Alafu ccm ni waoga sana. Mwaka huu utafanyika uvunjifu wa amani kwenye mikutano yao. Tuone kama watahimili. For a very action there is equal and opposite reaction. Hii imekuwa kero maana mikutano ya upinzani inavamiwa na police wakijifanya wao ni wana jamii kumbe ni police. So this year they can see something.
 
Aidha, Mhe. Mnyika amewataka wananchi wote bila kujali itikadi ya vyama vyao kuhakikisha mgombea aliyeshinda uchaguzi anatangazwa kwa kutumia nguvu ya umma.
Naipenda Chadema, lkn nguvu ya umma kwa mfano Mzaramo, Mdigo, msambaa na makabila mengine watavumilia milio ya risasi?, risasi za kuua? Mkurya sina wasi wasi atavumilia kufa, siyo mkabila mengine. Tutafakari zaidi what next! what to do! Niliandika wakafuta mods kuwa wimbi la kukimbilia CCM ni kuwa watatangazwa haka mama hawakushinda! Mmawia
 

Sina tatizo na kuitisha nguvu ya umma, naona cdm kama chama hamshiki hoja na kuimalizia. Kabla ya baa la Corona na kuzuiliwa mikusanyiko, ilikuwa kuna vuguvugu la kudai tume huru ya uchaguzi, na hoja ya kwanza ambayo tungeanza nayo baada ya kusema kutakuwa na mikutano, ni hiyo ya kudai tume huru.

Lakini baada ya bunge kuvunjwa naona kama hoja ya kudai tume huru ya uchaguzi imekufa midomoni mwenu, na sasa mnaongelea nguvu ya umma. Kwa tafsiri ya haraka ya ccm na vyombo vya dola, nguvu ya umma ni uvunjifu wa amani. Mimi nilitarajia kila kiongozi anayesimama aseme tunahitaji tume huru ya uchaguzi, neno hilo litumike mpaka liwe kero kwa kila mtu. Halafu mtangaze kutumia nguvu ya umma tena kwa herufi kubwa, kuwa mtatumia nguvu ya umma kwakuwa tume ya uchaguzi sio huru. Tunatakiwa tuingie kwenye uchaguzi huku tukiifanya tume iwe haiaminiki, na hata matokeo itakayotoa yasiaminike kabisa. Kwasababu iwe isiwe lazima tume hii iibebe ccm, namna pekee ni kuinyima uhalali wa kusimamia uchaguzi, na kuitangaza kwenye kila platform kuwa sio huru.

NB: tarehe 7/7/20 tuhakikishe tunavaa nguo nyeupe, ili kupandisha hamasa ya kudai tume huru vya uchaguzi. Madai ya tume huru ya uchaguzi ni ya halali na hayana muda. Kwahiyo hakuna kisingizio cha kuwa muda umeisha.
 
Haitoshi kuliongelea tu hili la kuvurugwa kwa kura na wakurugenzi au mtu mwingine yeyote.

Jitihada kubwa zinatakiwa kuhakikisha hili halitokei, na ili juhudi hizo zionekane kufanya kazi ni lazima pawepo na mikakati ya kuzuia hali hiyo.

Je, kuna njia zinazoandaliwa kuzuia uhalifu huo? Wananchi wataandaliwa wafahamu taratibu za kufanya hivyo bila ghasia na kama inalazimu kwa njia zingine zisizoleta madhara kwa wananchi kama inawezekana?

Mkurugenzi au polisi anapofanya uharifu wa kuvuruga uchaguzi, huyo ni mharifu kama waharifu wengine, na kama analindwa na vyombo vinavyotakiwa kumshughulikia, wananchi waelezwe namna ya kuwashughulikia hawa waharifu papo kwa papo.

Ni lazima hawa wakurugenzi waelewe, uharifu wanaofanya wataulipia wao moja kwa moja hapo hapo wanapofanyia uharifu huo.

Lakini la muhimu zaidi katika hayo ni kuwa na ushahidi usiowekewa mashaka kwamba uhalifu unatendeka. Kwa hiyo ni wajibu wa CHADEMA kuhakikisha kwamba wanazo mbinu za kuchukua ushahidi wa uhakika bila ya kuwa na wasiwasi nao.

Kama ni matokeo, kumbukumbu ziwepo na namba zisomeke wazi bila ya kupindishwa.

"NGUVU KUU YA UMMA NGUZO YAKE KUBWA NI KUWEPO KWA USHAHIDI USIOTILIWA MASHAKA"
kalamu1
 

Hivi Kwanini CHadema mnapenda sana kujikuza kwa Lipi hiyo nguvu ya umma.
 
CHADEMA,

Kwa kutumia nguvu ya Unma, ndiyo njia pekee ya kukabiliana na hao CCM, ambao wao wanaamini kuwa vyombo vyote vya dola viko upande wao.
Umma upi ambao CCM haina? Unafikiri wapinzani wana umma kuliko CCM? Endelea kuota mchana!
 
Erythro, eti unasemaje?
Hebu andika tena, mbona leo sikuelewi kama siku zote?

Huyu 'Hunter' ni wa chama gani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…