Sina tatizo na kuitisha nguvu ya umma, naona cdm kama chama hamshiki hoja na kuimalizia. Kabla ya baa la Corona na kuzuiliwa mikusanyiko, ilikuwa kuna vuguvugu la kudai tume huru ya uchaguzi, na hoja ya kwanza ambayo tungeanza nayo baada ya kusema kutakuwa na mikutano, ni hiyo ya kudai tume huru.
Lakini baada ya bunge kuvunjwa naona kama hoja ya kudai tume huru ya uchaguzi imekufa midomoni mwenu, na sasa mnaongelea nguvu ya umma. Kwa tafsiri ya haraka ya ccm na vyombo vya dola, nguvu ya umma ni uvunjifu wa amani. Mimi nilitarajia kila kiongozi anayesimama aseme tunahitaji tume huru ya uchaguzi, neno hilo litumike mpaka liwe kero kwa kila mtu. Halafu mtangaze kutumia nguvu ya umma tena kwa herufi kubwa, kuwa mtatumia nguvu ya umma kwakuwa tume ya uchaguzi sio huru. Tunatakiwa tuingie kwenye uchaguzi huku tukiifanya tume iwe haiaminiki, na hata matokeo itakayotoa yasiaminike kabisa. Kwasababu iwe isiwe lazima tume hii iibebe ccm, namna pekee ni kuinyima uhalali wa kusimamia uchaguzi, na kuitangaza kwenye kila platform kuwa sio huru.
NB: tarehe 7/7/20 tuhakikishe tunavaa nguo nyeupe, ili kupandisha hamasa ya kudai tume huru vya uchaguzi. Madai ya tume huru ya uchaguzi ni ya halali na hayana muda. Kwahiyo hakuna kisingizio cha kuwa muda umeisha.