Nguvu ya umma yashinda uchaguzi chuo kikuu cha ruco

Rose Mayemba

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2012
Posts
721
Reaction score
1,017
Kwanza namshukuru MUNGU wa mbinguni kwa kuwa mwaminifu kwetu tangu wakati wa kuanza mchakato wa uchaguzi hadi kupatikana kwa ushindi.

Lakini pia niwashukuru wanafunzi wote waliotupigia kura na wasiotupigia kwa maombi yao ya usiku na mchana hadi tumeibuka kidedea katika uchaguzi huo ambao ulikuwa ni wa kihistoria

Haikuwa kazi rahisi kama inavyoweza kudhaniwa bali ilikuwa ni safari iliyojaa fitina,majungu,unafiki huku ikitawaliwa na wimbi kuu la USALITI.

Wenzetu wengi walijitenga nasi huku wakiinua vikwazo mbalimbali, wengine walisema tunatembea na bendera za vyama,wengine wakasema tumetumia mavazi ya chama, na hata wengine wakadiriki kusema kuna kiongozi mkubwa wa chama alishiriki nasi kupanga namna ya kumpata Rais.

Lakini sisi tunakiri kwamba kama si NGUVU YA UMMA, iliyotuamini na kutusikiliza na hatimaye kutupa ridhaa sisi hatukuwa chochote katikati ya wana wa RUCO,yote yaliyosemwa na fitina zote zilizofanywa ilikuwa ni mpango wa makusudi kabisa wa watu fulani kutugawa sisi watoto wa baba mmoja.

Leo tarehe 20/05/2013 mnamo saa 8:16 za usiku alitangazwa bwana MSANGI RUSTON kuwa Rais halali wa chuo kikuu cha RUCO na Bi FLORAH YOHANA kuwa makamo wa Rais kwa mwaka wa masomo 2013/2014

Ikumbukwe kuwa mwaka jana wakati wa uchaguzi vurugu kubwa zilitokea baada ya Mkuu wa Mkoa kutoa vitisho kwa baadhi ya wajumbe wa tume na wengine kupewa amri ya kujitoa ili wampitishe mgombea ambaye lilikuwa chaguo lake

SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU
 
ni mwaka wa badiliko toka ngazi za kata mpaka taifa,kwa taarifa tu,kwa vyuo vyote ambavyo uchaguzi umeshafanyika tayari, Mungu ameendelea kuonesha neema kwa Makamanda wetu ambao wengi wameshinda chaguzi zao,kuna vyuo kampeni zinaendelea na upepo upo penyewe,Japo ccm wanatumia fedha nyingi lakini si wakati wao tena, hongereni makamanda wa Ruco,NGUVU YA UMMA NI MPANGO WA MUNGU.
 
Hongereni!! Jitahidini sasa kufanya yale wenzenu wanayategemea toka kwenu!!
 
Uchaguzi umeshakwisha ongezeni juhudi kwa kilichowaleta hapo chuoni!
 
Hofu yangu wasomi wa leo mmekuwa wepesi kununuliwa na akina Mwigulu Bandia. mnatia aibu na kinyaa mmejaa tamaa ya kupata mafanikio ya harakaharaka hata kwa kudhalilisha utu wenu.
 
Back
Top Bottom