Katika maisha yangu nimejikuta nikiingia ktk uhusiano na wanawake mbali mbali. Kinachonishangaza ktk kila mwanamke nitakayetembea naye halafu akaniacha lazima akija kuolewa hawezi dumu kwenye ndoa, lazima waachane tu.
Pia kama nilimtongoza akiwa shulen basi lazima apate mimba shule afu akishapata shule ataacha na kwenda kuolewa na huyo aliyempa kisha baada ya Muda wanabwagana.
Hali hiyo hutokea hata kwa wale ambao niliwapiga sound afu wakanitolea nje. Pia kuna wakati ambao nikipishana na mtu halafu moyo wangu ukijihisi huruma au maumivu juu ya mtu huyo ujuwe hapitishi week kabla hajaiona pepo.
Hivi nina nguvu gani?