Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Tarehe 9 mwezi wa kumi na mbili mwaka huu inatimia miaka 60 ya uhuru wetu. Itakuwa ni siku maalum yenye kila sababu ya kupambwa na nyimbo za furaha na zenye kukumbusha maana pana ya uhuru wetu.
Ni lazima tukumbushane kuwa umri huu tunaoufikia mwaka huu haujaweza tu kwa bahati kuweza kufikiwa, tukiwa ni nchi yenye makabila zaidi ya 120 tumeweza kuendelea kujitanguliza katika utanzania kabla ya kutanguliza makabila na dini zetu.
Ni lazima tuwaenzi viongozi wenye maono kama Hayati Julius Nyerere na Mzee Karume na wengine wote waliofanya kazi nzito ya kuunganisha watu na kukumbusha juu ya kutunza ile tabia ya kuvumiliana na kutazamana kama wamoja kabla ya kutanguliza viburi vyetu vya asili.
Tunapoelekea kutimiza miaka 60 ya Tanzania ni bora tukakumbushana maana ya uwepo wa viongozi wa dini wakati wa shughuli za kiserikali, wale wanasimamia umoja wetu. Tunapoyasikia maombi ya shekhe, yakafuatiwa na yale askofu au yule kiongozi wa wahindu, tunakumbushwa maana ya kuvumiliana, maana ya kuchukuliana kindugu licha ya wingi wa tofauti tunazoishi nazo.
Na kuvumiliana kuna maana pana zaidi, ni ule uwezo wa kumkubali mwenzako hata kama huamini katika imani yake. Ni ule uwezo wa kuvumilia vipindi vya dini vinavyorushwa runingani hata kama hukubaliani kiimani na kile kinachohubiriwa. Siku hizi kuna neno utangamano (compatibility), lenye kumaanisha uwezo wa watu kuishi pamoja na kutengeneza jamii moja. Unaingia ndani ya basi unakutana na wamasai, wagogo, wasambaa, wazinza na wazigua wakiongea kiswahili na wakijadiliana maswali ya kitaifa.
Ni vyema tukawakumbusha watanzania wenzetu haswa wale wenye umri mdogo juu ya umuhimu wa kuvumiliana, umuhimu wa kutozitangulia zile jeuri zetu za asili (prejudices) kama tunataka kuona Tanzania siku moja inasherehekea miaka 100 ya uhai wake. Kuna wanaojenga hoja kwamba maadam wanalipa kodi basi hata vipindi fulani vya dini visipewe kipaumbele siku za ijumaa na jumapili, hii ni hoja yenye kwenda kinyume na msingi wa kuvumiliana.
Tajiri kama RIP Subhash Patel kodi aliyokuwa anailipa kwa mwezi mmoja tu ni nyingi kulinganisha na ile inayolipwa na watanzania wengi kwa maisha yao yote, alikuwa ni mhindu, hivyo wahindu wasipewe haki ya kuwa na uhuru wa kuabudu na vipindi vya dini visiwepo radioni kisa mtu au watu fulani wanaona kama haviwahusu?.
Tunapokaribia kutimiza miaka 60 ya uhai wetu na uwe ni wajibu wa wote wenye kufahamu faida za kuvumiliana kitaifa kuingia kazini kwa nguvu zao zote ili waweze kuwapa elimu watanzania wa vizazi vya sasa juu ya suala zima la kukwepa aina zote za fikra zinazozaa ubaguzi na udhaifu wa utaifa.
Kuna mataifa mengi maarufu ambayo kwa nje yanayoonekana kuwa ni imara lakini kwa ndani utaifa wao ni teketeke sana. Wanatazamana kiukabila na kimaeneo na msingi wa udhaifu wa utaifa wao ni kutokukubaliana na hoja za kuvumiliana.
Mungu aibariki Tanzania ili wengi wetu tuweze kuuelewa ujumbe alioujenga Mwalimu Nyerere kwa muda mwingi wa uhai wake, ujumbe wa kupiga vita ukaburu wa kule afrika ya kusini na ukaburu kwa maana ya mawazo ya uzawa wenye kuzaa usisi.
Mungu ni mwema na aendelee kulitunza taifa hili.