Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,914
- 168,320
UKWELI KUHUSU USHIRIKINA: SAYANSI INAYOFICHWA NA MKOLONI HADI LEO
By
Æfrica Macka Bara
------------------------------------
Leo nadhani hata kipofu ataelewa kile ninachoelezea katika makala hii, na sidhani kama Baada ya hapo Utazidi kumuamini mzungu.. Kikubwa ni kuwa Mvumilivu na kuisoma Hadi Mwisho..
Jana katika makala yangu, Kuna mtu aliniambia kuwa Ushirikina haikuwa sehemu ya maisha ya Mwafrika..
Akasema "Mwafrika alipambana kwa juhudi kubwa kuupinga ushirikina..
Nikamuuliza,
"ushirikina ni nini haswa"
Akaniambia,
"Ushirikina ni imani au desturi zinazohusisha nguvu za kichawi. Mara nyingi, ushirikina unatokana na hofu, ujinga, au imani potofu juu ya ulimwengu na matukio yanayotokea."
Nikamuuliza, "kama ushirikina ni imani ama desturi zinazojusisha nguvu za kichawi, je uchawi ni nini?"
Akaniambia,
"uchawi ni imani ama Matumizi Ya nguvu za ajabu Zisizoeleweka ksayansi ama kimantiki.. "
Alivyoniambia neno hilo, nikakumbuka kuna siku Moja aliwahi pia kuniambia kuwa, Matumizi ya tiba za asili kiimani si dhambi wala kosa.. Kosa ni yale manuizi mtu anayo yatoa akiwa anatumia Tiba hizo za asili..
Sasa leo nimeona nimjibu kwa ujumla mtu huyu, ili atambue nini maana ya uchawi ama ushirikina ama nguvu za ajabu zisizoeleweka kisayansi ama kimantiki.
NGUVU ZA AJABU ZISIZOELEWEKA KISAYANSI AMA KIMANTIKI: SIRI USIYOFUNDISHWA SHULENI
Nguvu za Ajabu zisizoeleweka kimantiki, hutambulika kama nguvu za Miujiza ( magic )..
Hizi hupita uwezo wa kawaida wa kibinadamu na kumfanya mtu kutenda mambo yaliyo nje ya Mantiki.
Kwa Mujibu wa kitabu kikongwe cha Apicatrix, kinasema kuwa,
Kuna aina kuu mbili za nguvu za Miujiza (Magic)..
1. Miujiza nadharia ( Theoretical Magic )
2 Miujiza vitendo ( Practical Magic )
Theoretical Magic, ama Miujiza ya nadharia ni maarifa yasiyoweza kuthibitika kwa kuonekana, wala kwa kuhisika, ila yakaleta matokeo Yaliyokusudiwa..
Mienendo ya Umeme katika Nyaya, ni mojawapo ya theoretical Magic, ambapo Nguvu hii ya ajabu huwa haionekani, ila matokeo yake, kama vile taa za ndani kuwaka, Gari kuunguruma, Jiko la umeme kuzalisha joto la kutosha kupikia, huonekana..
Maneno pia, ni sehemu ya aina hii ya magic, kwa kuwa maneno yenyewe yana nguvu za miujiza..
Plato, mwanafalsafa maarufu wa kiyunani, anasema vivyo hivyo,
kwamba kama rafiki anaweza kuwa adui kwa maneno maovu na ya matusi, basi maneno mazuri na ya kirafiki yanaweza kumgeuza adui kuwa rafiki.
Kwa hivyo, ni wazi kuwa maneno yana nguvu ya Kimiujiza ndani yake, kwa kunena, mtu awe mkristo ama muislamu, mwafrika ama mzungu, hufanya Manuizi bila yeye kujuwa, na yale Manuizi huleta matokeo ya kile alichonuia.
kadiri pale nguvu kadhaa zinapounganishwa, Nguvu kubwa zaidi hupatikana katika aina hii ya magic.. na hii (maneno) ndiyo nguvu timilifu katika utekelezwaji wa aina hii ya magic..
2. MIUJIZA YA VITENDO
Hakika mzungu ni mwerevu sana.. Ukisoma Kitabu cha Apicatrix hutorudia tena kuamini katika maneno
ya kishenzi kama vile Ushirikina, Uchawi n.k..
Miujiza ya vitendo ama practical magic, kwa upande mwingine, mzungu akaipa brand kubwa, yenyewe mzungu hakuiita Uchawi, usirikina ama Ushenzi.. Badala yake akaiita Science..
Na ninyi mnaiita Science bila kujuwa kuwa hiyo ni aina ya pili ya Uchawi (magic/ witch–craft type two).. Na unakuta mtu na suit akijinadi kuwa, mimi siamini uchawi, naamini science.. Sijui kama watu wa aina hii huwa wanaelewa wanachozungumza.
Aina hii ya pili, ni muunganiko wa asili tatu ambazo sitazielezea hapa, maana nahitaji kudumu kwenye hoja ya msingi..
Na vitu hivi vitatu ndivyo vinavyochochea Gunduzi nyingi za kisayansi zinazokustaajabisha wewe mtu mweusi..
Sasa, Iko hivi..
Dini zote hutumia aina ya kwanza ya Uchawi ambapo, kupitia nguvu ya vitu vya asili, na manuizi kwa jina la Mungu, jambo hutokea..
Kwa wale wafia dini wanaopingana na hoja zangu, kumbukeni kuwa
Katika dini, kuna visa vingi vya Kimaandiko vinavyoonesha kuwa Hata watawa walitumia kundi la kwanza la magic katika tiba na kuondoa matatizo ya watu..
Mfano,
Eliya alichukuwa Chumvi Akaiweka katika chombo na kuimwaga katika Maji, baadaye kama nilivyo sema awali kuwa katika Aina hii ya Magic, maneno huwa na nguvu kubwa.. Eliya akayanenea yale maji (akanuiza) kwa jina La Mungu, maji Yakapona, yakawa Matamu na salama kwa kunywa.. 2 wafalme 2:19—22.
Nabii Musa, aliyaponya Maji kwa kukitupa kipande Cha Mti katika mto Uitwao mara na maji yalipona.. Hii ni baada ya Wana wa israel kufika pale na kukuta maji yale ni machungu na hayafai kwa Kunywa.. Kutoka 15:23-25
Yesu, alikutana na kipofu, akatema mate chini na kufinyanga udongo. Kisha akachukuwa udongo na Kumpaka yule kipofu machoni, kisha akasema "nenda kanawe katika birika la Siloamu". Na yule mtu aliponawa tu, akarudi akiwa anaona.. Yohana 9:6
Sitaelezea Mifano mingi kama Musa na Nyoka wa Shaba ama Musa na mwamba ulitoa Maji jangwani Watu wakanywa, ama Musa Na maji kugawanyika katika Bahari ya Shamu, ama ezekiel kuinuizia Mifupa Mikavu.. Nitaishia hapo ili muendelee kuliwa hela zenu kwa manabii wanaowauzia Mafuta ya upako, na maji ya upako kama shemu ya Kukomboa mali zenu na fikra zenu, kumbe ni utapeli wa kidini kwa kutumia elimu ya kale ya mtu mweusi iliyozikwa..
Kwanini Dini, ( hasa wakristo) ziseme kuwa aina hii ya sayansi (Theoretical magic) ni ushirikina kwa kuwa unapotumika sana na wale wasioenda katika makanisa na misikiti, na kwa upande wa pili, uitwe ibada ya haki mbele za Mungu kwa wale wanaoenda katika taasisi zao za kitapeli?
Natumai jibu umelipata tayari..
Ni kwasababu ya propaganda za awali za kikoloni. Katika zama za uenezwaji wa dini, Walipiga marufuku Tamaduni za mwafrika na kuziita ushirikina ama uchawi..
Waliiona nguvu kubwa iliyokuwa ikitokana na Aina hii ya Magic kama tishio katika uenezaji wa propaganda zao, na hivyo basi,
Kama nilivyosema hapo awali kuwa, kadiri pale nguvu kadhaa zinapounganishwa,
Nguvu kubwa zaidi hupatikana katika aina hii ya magic,
Na nikasema Pia mwanzoni kuwa
'Maneno/ manuizi / maombi ndiyo nguvu timilifu katika utekelezwaji wa aina hii ya magic"
walilazimika kuipiga marufuku aina hii ya sayansi na kubakiza kipande kidogo sana katika sayansi hii kiitwacho "Manuizi/ maneno/ maombi kwa jina la Mungu" ambacho walikibatiza jina la "Maombi", wakijuwa kuwa kitakuwa na nguvu ila kidogo sana ukilinganisha na pale ambapo kipande hiki kingeungana na vipengele vingine na kuleta Nguvu kubwa zaidi..
Zamani mvua zilipogoma kunyesha, wazee walienda msituni ama milimani na kufanya Ibada zao zilizounganisha matumizi ya vitu na manuizi/ maneno/ maombi kwa Mungu, na mara baada ya muda mfupi Mvua ilinyesha..
Leo hii ni tofauti kabisa, maana makanisa yanaweza hata kufunga siku kadhaa wakianya manuizi/ maombi/ maneno na bado mvua isinyeshe— sijui kama waliisha wahi kujiuliza why!! Na hii ndio sababu Mungu wao hutukanwa na wale wasio mwamini, kwamba hajibu maombi yao.. Kumbe kuna vipengele wanashindwa kuviunganisha ili kupata nguvu kubwa, yenye utisho ndani yake..
Wakoloni, ili kudhohofisha Tamaduni za mtu mweusi, wakamzuia:
1. Asijihusishe Na Matumizi ya muunganiko wa Vitu vy asili na manuizi/maombi/ maneno, badala yake ategemee manuizi/maombi/ maneno pekee.
Baadhi ya vitabu vilivyohusiana kwa karibu na Tamaduni za mwafrika na matumizi ya theoretical magic, wakaviondoa katika biblia zao wakiviita Uzushi na kudai kuwa havikuandikwa na wahusika wenyewe bali wachawi ndio walioandika ili kuwapotosha watu. Wakaviondoa na kubakiza vitabu 66 kwa biblia za waprotestant, na 72 kwa biblia za wakatoliki..
Mfano wa vitabu vilivyopigwa marufuku na hawa wazungu ni pamoja na:
Kitabu cha Sirach, Baruch, The book of Enoch, kitabu cha Jubilees, The book of Maccabees n.k
Sitaweza kuvitaja vyote ila hivyo ni baadhi ya vitabu ambavyo kwa upande mmoja viligusa tamaduni za mwafrika, kuonesha uhusiano alio kuwa nao na Mungu.. Ninaposema siamini biblia huwa namaanisha hoja hii hasa, kwamba, waandishi wa hizi biblia walichambua vitabu vitakavyoendana na sera zao za kumtawala muumini kifikra..
2. Asijihusishe na masuala ya siasa.. Wakamwambia, siasa na dini haviingiliani na Mungu hapendi— kwanini wafanye hivi?
Walihitaji jambo moja kwamba: mara baada ya Mtu mweusi kuingia katika mkenge wa dini, wataweza kutawala ardhi yake milele.. Kwa kuwa dini itamzuia kujihusisha na siasa pamoja na harakati za kudai uhuru, itakuwa rahisi kwa wao kuendelea kumtawala..
Jambo hili ndilo lililochelewesha uhuru wa Mtu mweusi, maana baadhi ya wafia dini waliwaona wale wanaodai uhuru kama waasi, waovu na wavuruga amani..
Hivyo wakajikuta wakiungana na wakoloni kuwakwamisha wana harakati.
Na Hiki ndicho kinachoendelea hadi Leo, Ni waumini wa dini wachache wenye uchungu na ardhi zao, wenye moyo wa chuma wa kusimama hadharani na kukemea Watawala wanao waonea wengine— asilimia kubwa ya dini za kigeni zinawalia waumini sadaka na kuwapotosha kwa maneno makavu, huku ardhi waliyopewa na Mungu ikiendelea kuliwa na mapebari.. Aibu kabisa!!
Pongezi kwa Umoja wa Maaskofu katoliki Tanzania, ambao wanaonesha jinsi walivyokomaa katika Uelewa wa uhusiano uliopo kati ya dini na Siasa.. Pongezi pia kwa baadhi ya Masheikh na wachungaji ambao husimama mstari wa mbele kama makuhani, kama wapatanishi baina ya wanajamii na watwala wao, kuhakikisha haki inatendeka katika ardhi yao..
Ila sijawahi kuona Mchungaji wa kisabato na makanisa mengine akikemea uovu wa viongozi waovu—why?
ni kwasababu, wameathiriwa na propaganda za mtu mweupe..
Ninapomalizia hii makala yangu ya kumuamsha mfia dini,
Hatuipingi dini kwa chuki binafsi, tunaipinga dini kwa kuwa inatuchukia sisi.. Inatutenganisha sisi na Asili, sisi na Mungu, na pia sisi na Uongozi unao tutawala..
Ni muda wa Yule anayeamini kuwa matumizi ya asilli ni uchawi kubadili mawazo yake, maana kabla ya ujio wa wazungu hatukuwa na neno "Ushirikina"..
Neno hili, tulilitambua kama sayansi,
Na lilitumika hata katika ibada za kale za kwenye biblia na quran hadi pale wazungu walipoleta propaganda zao.