Nguvu za giza " the power of darkness"

Nguvu za giza " the power of darkness"

Infact, giza lipo na Lina nguvu halikadhalika nuru ipo na ina nguvu.
 
Labda nijidanganye mwenyewe Brethren ila siyo jamii yoyote ya wazi au ya Siri.
Yohana 1:5 "Nayo nuru yang'aa gizani; wala giza halikuishinda."
...........................
Maneno yangu: Hapa inaonesha kuwa nuru hung'aa inapokuwa gizani.
Naam, katika ulimwengu huu wa mwili ama ulimwengu wa roho ngazi fulani, ili nuru ionekane kuwa nuru ni lazima kuna giza, hakuna namna ingine yoyote ile, isipokuwa sehemu ingine ambayo nuru ni mahali pale hasa hapo ambapo hakuna usiku wala mchana, hapo daima ni nuru wala hiza lolote hakuna kabisa. Sababu hiza nalo limeumbwa kama vingine vyote vilivyoumbwa
 
Kwanza hata kama ukiichambua Hilo neno lote utapata maana halisi kwanini lilitwa hivyo..

Kwenye zohar na TANAKH (Kwa lugha ya Kiebrania)
Giza Au Darkness huitwa "חשך" (choshech).
Herufi xake ni
Chet ח
shin ש
kaf ya mwisho ך

herufi Cheti ya kwanza Humaanisha Life "Maisha" japo inaweza kuwa Mzani kati ya Maisha na Dhambi yaani Mauti na Uzima..

na huwakilishwa na namba nane (Kwenye Gemetria)

View attachment 2951143

Ukija kwenye Herufi Shin

Humaanisha Kurudi au kurudia,Pia huweza kumaanisha Jino/Meno pia mabadiliko..
View attachment 2951147
Pia Shin inatambulisha Moto wa kuumba au Moto wa Unabii ndo maana manabii wakubwa katika biblia wana Shin..Moshee(Musa), Shlomon (Suleiman) na hata Yesu (Yeshua)..

View attachment 2951149

Ukija kwenye Final kaf
View attachment 2951150
Nafikiri Hapo inaonekana vizuri
View attachment 2951151


So kwa pamoja Na kuchanganya maana zote za Giza utapata Maana yake
Sio maana mbaya hata kidogo
Mzee upo deep, napenda maarifa, napenda sana maarifa katika njia salama mzee. Naendelea kukifunza kiongozi
 
Ni miongoni mwa siri ambazo hayupo anayezifahamu ila Mwenyenzi Mungu.
Kama giza linasimamia hali ya kutokujua mambo, hasa katika uumbaji wa viumbe hai Duniani, ni wazi linaonekana kutangulia kabla kiumbe hajapata maarifa (nuru)
 
Hapa inabidi nitulie kwanza!..Nilichowahi kujifunza mahali ni kuwa,
Neno "choshech" linamaanisha giza katika lugha ya Kiebrania, ambayo inaathiriwa na matumizi yake katika Biblia ya Kiebrania (Tanakh) na maandiko ya Kikristo ya Agano la Kale. Neno hili linapatikana mara nyingi katika maandiko hayo kuelezea giza kimwili na pia kwa maana ya kiroho au kisiasa.

Katika Biblia, "choshech" mara nyingi hutumiwa kama ishara ya kutokujua au kutoweza kuelewa mambo, na pia kama alama ya uovu au dhambi. Kwa mfano, katika Kitabu cha Mwanzo 1:2, "choshech" inatajwa kama hali iliyokuwepo kabla ya uumbaji wa mwanga: "Nayo dunia ilikuwa ukiwa, tena utupu; na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji."

Kwa hiyo, "choshech" inaweza kutumiwa kumaanisha zaidi ya giza la kimwili; inaweza pia kumaanisha kutokuwepo kwa mwanga wa kiroho au maarifa, na pia kuhusiana na hali za kiroho za upotevu au uovu. Katika muktadha wa dini na imani, neno hili linawakilisha kipindi cha kutokuwa na mwanga wa mwongozo wa Mungu au kutokuwepo kwa wema na haki.

Dr!..au nilimeza sumu?
So Mungu alikuwepo Kipindi ambacho Hakuna Maarifa?
Na kipindi cha Upotevu?
Giza Lina maana Kubwa sana nakushauri Soma TANAKH sana kuna vingi kwenye Lugha ya Kiebranja imefichwa
 
So Mungu alikuwepo Kipindi ambacho Hakuna Maarifa?
Na kipindi cha Upotevu?
Giza Lina maana Kubwa sana nakushauri Soma TANAKH sana kuna vingi kwenye Lugha ya Kiebranja imefichwa
Naomba kama una document ya Tanakh nisaidie Dr.
 
Palipo na Nuru hakuna Giza.

Usidanganywe na masonry.
Ukitaka ku-prove washa taa gizani kisha jiulize giza huenda wapi? Kisha Zima taa jiulize hutokea wapi?
Hivi vitu vipo na ni kitu kilekile katika mawanda tofauti
 
Back
Top Bottom