Sijaona ushauri wenye maana hata mmoja. Tatizo la nguvu za kiume linasababishwa na mambo mengi sana na sio kupiga punyeto peke yake. Wengine wana matatizo ya nguvu za kiume, lakini hawajawahi kupiga punyeto katika maisha yao. Mimi nafikiri ukosefu wa nguvu za kuime ni kama kilema cha kuzaliwa nacho tu basi. Nasema hivyo kwasababu kuna watu wametumia dawa za kila aina na wamezunguka sehemu mbalimbali duniani bila mafanikio yoyote yale. Kuna dawa ambazo zitaondoa tatizo kwa muda mfupi tu na baada ya hapo tatizo lako linabaki palepale. Ukosefu wa nguvu za kiume hauna dawa ya kuondoa tatizo kabisa. Kama umezaliwa na tatizo hili basi ni bahati tu. Kuna watu wanaweza kupiga bao tatu, wengine nne, wengine ni moja tu na hawawezi kurudia tena. Hakuna dawa jamani, ni maumbile tu. Wanaosema wanauza dawa za kutibu nguvu za kiume ni waongo kabisa, hawa ni watu wanao tafuta pesa kwa kuwadanganya watu wengine. Mbaya zaidi ukiwa na hili tatizo na ukitumia hizo dawa, usipopona, huwezi kwenda kulalamika popote, sababu kutokana na mazingira ya tatizo lenyewe, mgonjwa hawezi kutangaza kuwa anatatizo hilo na ametumia dawa hajapona. Hii inawafanya wauza dawa hizi kuendelea kuwadanganya watu wengi zaidi na kujipatia faida kubwa.
Ushauri wangu kwa watu wenye tatizo hili ni kujikubali tu basi kwani hakuna njia nyingine. Zipo dawa za kuongeza nguvu kwa muda mfupi tu. Mtu akitaka anaweza kutumia hizi dawa kila mara anapotaka kukutana na mwanamke. Dawa hizi zinapatikana kwenye maduka ya kuuzia dawa. Ukosefu wa nguvu za kiume ni sawa na kuzaliwa na mkono mmoja au mguu mmoja, hakuna dawa duniani utakayotumia ukaota mkono ambao hauna, au ukapata mguu ambao hauna. Lakini kama umezaliwa na mguu mmoja, unaweza kuweka mguu wa bandia au mkono wa bandia. Huo ndio ukweli na hakuna zaidi ya hapo. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Ukisoma biblia{wale wanaosoma Biblia} utaona Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa "Maana wako matowashi {Eunuchs} waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao"....Mathayo 19:12. Hivyo basi kutokana na ukweli huu, hakuna kabisa dawa ya kutibu tatizo la nguvu za kiume na kulimaliza kabisa. Kama umezaliwa hivyo hakuna unachoweza kufanya kuibadilisha hiyo hali.