Nguvu za kiume:-

Nguvu za kiume:-

kamkoda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2012
Posts
396
Reaction score
71
Wana Jamvi tafadhali nisaidieni mwenzenu nikipata kabao kamoja hoi sitaki tena next raundi,nipeni mchongo wa dawa madhubuti angalau nipige tatu za kuanzia naogopa kuwa mbofela mie.
 
(1) Acha kabisa kuangalia picha za ngono mahali popote.
(2) Acha kabisa kupiga punyeto.
(3) Kula chakula bora na hakikisha unalala mapema.
(4) Fanya mazoezi ya mwili kwa kiasi kila siku.
(5) Acha uzinzi hakikisha uliyeko naye ni mkeo wa ndoa.
(6) Usijaribu kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume utaharibu mambo kabisa.
(7) Kupiga bao zaidi ya mbili kwa siku sio sifa bali ni kujizeesha mapema na kujipunguzia nguvu.
 
kunywa value chupa moja bila kuchanganya na kitu chochote ila hakikisha umekula vizuri
 
Nadhani ushauri wa Ndetirima ni wa maana zaidi..anza kuuzingatia huo!!!
Ol d best...
 
Last edited by a moderator:
fanya mazoezi kimbia sana!hlf hakikisha unakula vzr na unapumzika muda mwingi?
 
Kunywa konyagi 1 kubwa huku ukitafuna mirungi ya kutosha kabla ya kuanza mechi hapo unwaweza kupiga bao hadi 6
 
Sijaona ushauri wenye maana hata mmoja. Tatizo la nguvu za kiume linasababishwa na mambo mengi sana na sio kupiga punyeto peke yake. Wengine wana matatizo ya nguvu za kiume, lakini hawajawahi kupiga punyeto katika maisha yao. Mimi nafikiri ukosefu wa nguvu za kuime ni kama kilema cha kuzaliwa nacho tu basi. Nasema hivyo kwasababu kuna watu wametumia dawa za kila aina na wamezunguka sehemu mbalimbali duniani bila mafanikio yoyote yale. Kuna dawa ambazo zitaondoa tatizo kwa muda mfupi tu na baada ya hapo tatizo lako linabaki palepale. Ukosefu wa nguvu za kiume hauna dawa ya kuondoa tatizo kabisa. Kama umezaliwa na tatizo hili basi ni bahati tu. Kuna watu wanaweza kupiga bao tatu, wengine nne, wengine ni moja tu na hawawezi kurudia tena. Hakuna dawa jamani, ni maumbile tu. Wanaosema wanauza dawa za kutibu nguvu za kiume ni waongo kabisa, hawa ni watu wanao tafuta pesa kwa kuwadanganya watu wengine. Mbaya zaidi ukiwa na hili tatizo na ukitumia hizo dawa, usipopona, huwezi kwenda kulalamika popote, sababu kutokana na mazingira ya tatizo lenyewe, mgonjwa hawezi kutangaza kuwa anatatizo hilo na ametumia dawa hajapona. Hii inawafanya wauza dawa hizi kuendelea kuwadanganya watu wengi zaidi na kujipatia faida kubwa.

Ushauri wangu kwa watu wenye tatizo hili ni kujikubali tu basi kwani hakuna njia nyingine. Zipo dawa za kuongeza nguvu kwa muda mfupi tu. Mtu akitaka anaweza kutumia hizi dawa kila mara anapotaka kukutana na mwanamke. Dawa hizi zinapatikana kwenye maduka ya kuuzia dawa. Ukosefu wa nguvu za kiume ni sawa na kuzaliwa na mkono mmoja au mguu mmoja, hakuna dawa duniani utakayotumia ukaota mkono ambao hauna, au ukapata mguu ambao hauna. Lakini kama umezaliwa na mguu mmoja, unaweza kuweka mguu wa bandia au mkono wa bandia. Huo ndio ukweli na hakuna zaidi ya hapo. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Ukisoma biblia{wale wanaosoma Biblia} utaona Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa "Maana wako matowashi {Eunuchs} waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao"....Mathayo 19:12. Hivyo basi kutokana na ukweli huu, hakuna kabisa dawa ya kutibu tatizo la nguvu za kiume na kulimaliza kabisa. Kama umezaliwa hivyo hakuna unachoweza kufanya kuibadilisha hiyo hali.
 
(1) Acha kabisa kuangalia picha za ngono mahali popote.
(2) Acha kabisa kupiga punyeto.
(3) Kula chakula bora na hakikisha unalala mapema.
(4) Fanya mazoezi ya mwili kwa kiasi kila siku.
(5) Acha uzinzi hakikisha uliyeko naye ni mkeo wa ndoa.
(6) Usijaribu kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume utaharibu mambo kabisa.
(7) Kupiga bao zaidi ya mbili kwa siku sio sifa bali ni kujizeesha mapema na kujipunguzia nguvu.

Good advice
 
Kunywa konyagi 1 kubwa huku ukitafuna mirungi ya kutosha kabla ya kuanza mechi hapo unwaweza kupiga bao hadi 6
Konyagi sijui lakini mirungi so mizuri kabisa tena raha yake wala sioni....zaidi yakuamka umechoka nakuumwa.......
 
Son of Gamba, i can not agre more!! Ukwelindio huo umeuweka bayana
 
Kizuri kwako ni kwamba kimoja unafika, sielewi nyuma uliwahi kufika viwili au vitatu na sasa huwezi tena au vipi? Vipi patner wako anaridhika? Kwako naona mazoezi yanaweza kukusaidia provided mambo mengine yapo sawa. Unaweza kumuona daktari kwa ushauri zaidi.

Nami nimeelimika kidogo kutokana na post zilizotangulia, ila nami naomba nieleze lile ninalolifahamu ingawa kuelezea mambo haya ni kazi hasa kwa kutumia Lugha yetu, ila nitajitahidi na wataalamu zaidi watarekebisha pale nilipoenda mrama.

(1)Tukubaliane ya kuwa kuna magonjwa au matatizo ya kiafya ambayo mtu anaweza kuzaliwa nayo na hayo hayo yanaweza kutokea kwa mtu mwingine baada ya kuzaliwa (mfano kisukari type 1 versus type 2).
(2)Kuna matatizo ya kiafya ambayo hayatibiki (cured) ila yanatulizwa tu (managed,symptomatically) (mf Kisukari, UKIMWI, shinikizo la damu n.k), na mengine yanatibika (mf Malaria).
(3)Kukosa nguvu za kiume (erectile dysfunction, impotence) ni hali ya uume unaposhindwa kusimama kabisa (erection) au unasimama/dinda kwa muda mfupi baadae unasinyaa (failure to maintain erection).
(4)Kukosa/kupungua nguvu za kiume kunaweza kupona au kutopona kutegemea sababu inayosababisha kuwepo kwa tatizo hilo.

Mojawapo ya sababu zinazosababisha mtu kupoteza (kupungua?) nguvu za kiume ni
(a)Unene kupita kiasi(Obesity),
(b)Kisukari,
(c)shinikizo la damu,
(d)uvutaji wa sigara,
(e)Ulevi wa kupindukia,
(f)psychological factors (msongo wa mawazo, hofu,uchovu)
(g)ukosefu/upungufu) wa hormone husika (hypogonadism),
(h)umri (inatokea kuanzia miaka 40 na kuendelea, ila kuanzia miaka 60 uwezekano ni mkubwa zaidi), (i)magonjwa ya mfumo wa fahamu (Parkinsonism etc),
(j)madhara ya dawa,n.k.

(5)Ili mashine isimame inahitaji ipate damu ya kutosha na hisia za kimahaba, yote yanadhibitiwa na mfumo wa fahamu.

(6) Sababu zilizoelezwa hapo juu zinasababisha upungufu/kukosekana kwa nguvu za kiume kwa kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye mashine (pen.s) na/au kuharibu mfumo wa fahamu unaosababisha shaft isimame.

(7) Kwa hiyo kwa kutegemea nini kinasababisha na stage ya tatizo iliyofikiwa mgonjwa, tatizo la kukosa/kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kwisha (kwa kufanya mazoezi,kupunguza msongo wa mawazo n.k) au kutokwisha.

Nashauri sana kabla hujatumia dawa naomba ukaonane na daktari ili angaalie hali yako kiundani kwani kila mmoja anaweza kuwa na sababu tofauti inayosababisha tatizo hilo. Matibabu ya tatizo yatategemea tatizo linalosababisha hali hiyo na hatua ya ugonjwa ulifikia. Si lazima kutumia dawa kwa kila tatizo la afya ulilo nalo.
Nasisitiza dawa hizi za kuongeza nguvu za kiume zinaweza kukuletea madhara zaidi kama utazitumia bila ushauri wa kitaalamu.
 
Sijaona ushauri wenye maana hata mmoja. Tatizo la nguvu za kiume linasababishwa na mambo mengi sana na sio kupiga punyeto peke yake. Wengine wana matatizo ya nguvu za kiume, lakini hawajawahi kupiga punyeto katika maisha yao. Mimi nafikiri ukosefu wa nguvu za kuime ni kama kilema cha kuzaliwa nacho tu basi. Nasema hivyo kwasababu kuna watu wametumia dawa za kila aina na wamezunguka sehemu mbalimbali duniani bila mafanikio yoyote yale. Kuna dawa ambazo zitaondoa tatizo kwa muda mfupi tu na baada ya hapo tatizo lako linabaki palepale. Ukosefu wa nguvu za kiume hauna dawa ya kuondoa tatizo kabisa. Kama umezaliwa na tatizo hili basi ni bahati tu. Kuna watu wanaweza kupiga bao tatu, wengine nne, wengine ni moja tu na hawawezi kurudia tena. Hakuna dawa jamani, ni maumbile tu. Wanaosema wanauza dawa za kutibu nguvu za kiume ni waongo kabisa, hawa ni watu wanao tafuta pesa kwa kuwadanganya watu wengine. Mbaya zaidi ukiwa na hili tatizo na ukitumia hizo dawa, usipopona, huwezi kwenda kulalamika popote, sababu kutokana na mazingira ya tatizo lenyewe, mgonjwa hawezi kutangaza kuwa anatatizo hilo na ametumia dawa hajapona. Hii inawafanya wauza dawa hizi kuendelea kuwadanganya watu wengi zaidi na kujipatia faida kubwa.

Ushauri wangu kwa watu wenye tatizo hili ni kujikubali tu basi kwani hakuna njia nyingine. Zipo dawa za kuongeza nguvu kwa muda mfupi tu. Mtu akitaka anaweza kutumia hizi dawa kila mara anapotaka kukutana na mwanamke. Dawa hizi zinapatikana kwenye maduka ya kuuzia dawa. Ukosefu wa nguvu za kiume ni sawa na kuzaliwa na mkono mmoja au mguu mmoja, hakuna dawa duniani utakayotumia ukaota mkono ambao hauna, au ukapata mguu ambao hauna. Lakini kama umezaliwa na mguu mmoja, unaweza kuweka mguu wa bandia au mkono wa bandia. Huo ndio ukweli na hakuna zaidi ya hapo. Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Ukisoma biblia{wale wanaosoma Biblia} utaona Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa "Maana wako matowashi {Eunuchs} waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao"....Mathayo 19:12. Hivyo basi kutokana na ukweli huu, hakuna kabisa dawa ya kutibu tatizo la nguvu za kiume na kulimaliza kabisa. Kama umezaliwa hivyo hakuna unachoweza kufanya kuibadilisha hiyo hali.

What is your definition ya nguvu za kiume...Jifunze kutoa ushauri mzuri na constructive criticism.
 
Wengine kwa mke wa ndoa goli mbili hoooi ila kwa outsiders usipime!!!!!5++
 
Mwambie mwenza wako unapomaliza bao la kwanza awe anajalibu kukupetipeti isia ziwe kama ndio unaanza.
 
Back
Top Bottom