Nguvu za ulimwengu na utakaso wa kiroho

Nguvu za ulimwengu na utakaso wa kiroho

third eye chakra

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2023
Posts
713
Reaction score
1,745
NGUVU ZA ULIMWENGU.

Nguvu za full moon.
Full moon ya mwezi June itakuwa kuanzia tar 22 Hadi 24 .

Mambo ya kufanya .
👉Kuachilia.
Kuachilia ni sehemu ya kujiponya mwenyewe na kutua mizigo na mahangaiko ambayo yameweza kukusumbua kwa muda mrefu .

Waweza achilia roho ya madeni,roho ya kuchukiwa hovyo na watu au kazini kwako,
roho ya umaskini,waweza achilia tabia Hasi kama Uzinzi,wizi,Hasira ,uzembe ,wivu,usengenyaji,Magonjwa,mikosi mbalimbali,ndoto mbaya nk ,
Achilia vyote usivyovitaka.

Tafadhali waweza washa udi kipindi unaandika.

Chukua karatasi nyeupe na mark pen ya bluu.
Andika vitu hivyo ,huku ukimaanisha kutoka ndani mwako,kwenye familia yako,watoto wako na ukoo wako.

Baada ya kumaliza kuandika Toka nje kwenye mwezi ,hakikisha unauangalia mwezi,Anza kuachilia kwa kuyatamka mambo hayo uliyoyaandika,tamka kutokea ndani ,ONA ya kwamba mambo haya yameyeyushwa na Nguvu ya mwezi inayomulika ulimwenguni.
👇👇👇
Nuru iwakapo,Giza hutoweka,Magonjwa yataikimbia Nuru ,misiba kwenu itaikimbia Nuru,
Ajali kwenu zitaikimbia Nuru,umaskini utakimbia kwako Nuru ikija Na Nuru ipo ulimwenguni ,kazi kwako.

Baada ya hapo choma karatasi hiyo yote ,inapoungua endelea kuachilia ,ikiungua yote ,Anza kuishukuru Universe kwa kuondosha mambo hayo ambayo yalikuwa yanakusumbua na Sasa kwako hayapo Tena.

Hakika ukifanya ikupasavyo ,utajiponya na matatizo haya.
Kumbuka kufanya ukiwa msafi wa mwili.
 

Attachments

  • FB_IMG_17085337028058639.jpg
    FB_IMG_17085337028058639.jpg
    235.7 KB · Views: 15
Huu ni uganga kama waganga wa kienyeji ama
 
Back
Top Bottom