Mi nadhani kuna watu wapo duniani kupinga kila jambo linalokuja mbele yao, na mimi mara nyinga huwa sina muda wa kupoteza kupingana nao.
Wabunge, rais na hata madiwani (vyama vyote) wana kawimbo wanakaimba eti ooh nimewaletea umeme, au nitawaletea umeme mkinichagua, swali linakuwa je atagharamikia miundombinu ya huo umeme? Kwani ni wangapi waliovuta umeme kwa gharama za rais, mbunge au diwani?
Kwani mtu akienda pale TANESCO kuomba kuvuta umeme wanamwomba barua ya mbunge, diwani au barua kutoka ikulu?
Kiukweli swala la kuchangia gharama ya huduma fulani silikatai moja kwa moja, ila basi kama mtu akijitolea kuvuta umeme pawepo na makubaliano(mkataba) fulani wa namna ya ku refund japo kidogo kidogo. Imagine mtu anaishi 10km kutoka ulipo umeme, na mtu huyu kweli anaweza kulipa gharama ya kuvuta umeme mpaka pale, tunamfikiriaje mtu huyu kwa zile milioni zake kadhaa anazotumi(achilia mbali kiasi alichohonga mpaka kukamilika mchakato mzima)?
Ikumbukwe kuwa watanzania wanaotumia umeme ni chini ya 30%, lakini hii 70% iliyobaki sio kwamba wote wanashindwa kulipia tsh 5000/= kwa mwezi kwa ajili ya umeme. Watu wanashindwa kulupa kwa mkupuo mamilioni ya hela kuvuta umeme katika maeneo yao. Ukiongea na watu wa maeneo mbalimbali utasikia wanavyohitaji umeme.Binafsi nimeshuhudia maeneo kadhaa mikoa mbalimbali, wananchi wanajitolea kuchangishana hela kwa ajili ya kuvuta umeme, wakawatafuta mafundi wakafanya wiring ktk nyumba zao, lkn hadi sasa (zaidi ya miaka 5) umeme huo kwao ni ndoto.
Je, tunapokuwa tunabisha hapa kijinga, tuanajua wawekezaji wanalipia kiasi gani ili umeme upelekwe kwenye maeneo yao? Je, wawekezaji, let's say migodini, wanaanza kulipa kodi baada ya muda gani? Mimi siamini kuwa TANESCO(serikali) wanashindwa kujenga miundombinu ya umeme kuwafikia wateja. Kama zaidi ya tsh 3bil. zinaweza kutumika kutafutia ubunge kwenye jimbo moja tu, sidhani kama kiasi hicho kingetumika kusambaza umeme pale Igunga,wanaigunga wote waliojiandikisha wangepiga kura na wangeendelea kuichagua ccm miaka yote ya uhai wao.
Mimi naamini wachangiaji wengine humu JF wanajua maisha ya pale Mbezi Beach pekee, na wanafikiri watanzania wote wanaishi maisha ya vile. Au wanaishi maeneo ambayo umeme upo full 24/7. Na wakisikia mbunge fulani akihoji uhalali wa jambo kubwa kama hili anaona ni hadithi za abunuasi. They can't be serious. Jaribuni angalau (hata kwa kutalii tu) kutoka hapo na muende mikoani, vijijini huko ili muwaone walipa kodi wenzenu wana maisha gani.
This is serious issue. Serikali inaweza kuwasaidia wananchi na hilo hata Ngeleja anajua. Ni kitendo cha kuamua tu. Sio kulalamila tu umasikini kwamba watu wanaishi kwa chini ya dola moja. Hili ni jambo la kuweka pembeni tofauti zetu na kuisukuma serikali ili ihakikishe kwamba panakuwapo na magawanyo sawa wa rasilimali tulizonazo.
Napenda kuishauri serikali kwamba umeme ni kigezo kikuu katika kuwakwamua wananchi kutoka tope hili la umasikini tulionao. Watu wanahitaji umeme, wanaweza kulipia bili kwa mwezi. Tatizo ni gharama kubwa ya miundominu yake, watu hawawezi na hawatweza kamwe bila support ya serikali.
Watu wanahitaji umeme, sio barabara za angani. Hao watu wanaosababisha msonagamano huko, wamefuata umeme. Waleteeni umeme huku muone kama wataendelea kutoka mijasho huko.