Haparahatu
Member
- Jan 23, 2020
- 27
- 24
Nguzo za Nchi bye bye
Chama cha CCM kimeshinda kwa kishindo uchaguzi wa 2020. Kama ndio hivyo basi, kupeleka majeshi Zanzibar pamoja na baadhi ya maeneo ya Tanzania bara yenye upinzani ni ishara kubwa kuwa haki za watu zimepotea.
Nimefikiria sana tunaenda vipi mbele kama Taifa. Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na mapungufu yake aliiweka hii nchi vizuri kwa kuleta umoja kwa makabila yote na hii ni zawadi kubwa aliyoiacha katika taifa hili.
Mimi namwona mtanzania kama mtanzania sijali kama ametoka eneo gani,kabila, dini na rangi yake. Mimi binafsi familia yetu imetoka znz lakini tumeishi bara na pia tumepata manufaa Tanzania bara pia nimeishi Arusha naipenda Arusha sana na siungi kutengana kwa umoja huu hata kama kuna baadhi ya wapinzani wanataka hivyo kutokana na dhulma zilotendeka. Kama mfumo wa muungano utangaliwa vizuri basi Tanzania idumu.
Mambo ambayo yanajitokeza ambayo naona niyaseme na yananiuma na pia tunapoelekea kwanza nchi imeanza kuwa na mgawanyiko:
- Mgawanyiko ulikuwepo kama wapemba na waunguja. Wapemba walikuwa upinzani wakichukuwa majimbo yote na chama Tawala kikawa kinashinda majimbo mengi unguja kama kuonesha kuna mgawanyiko wa fikra katika wakazi hawa wawili (Divide and Rule). Pamoja na hayo yote wapinzani walipewa sauti bara na visiwani maisha yakaendelea.
- Sasa tumeanza level 2 kuwa wazanzibari ndio tatizo hawataki muungano na polisi wamepelekwa kuwashikisha adabu na wamefanya hayo mauaji. Kutokana na mambo yaliotokea, Znz ishabadilika kimawazo na wananchi wao kwa asilimia 100% watakua wataona vikosi vyote vya usalama kama wakoloni. Hussein Mwinyi itabidi aendeshe nchi wa kuweka majeshi tu.
- Maeneo mengi ya Tanzania bara pia wamepata mkong'oto na wengine kuuwawa. Kwahivyo pigo sio la wazanzibari tena ni Tanzania nzima.
Sasa basi nimesikia watanzania wengi wakiongea maneno yafuatayo:
Tulianza na uzanzibari, na sasa tumeingia kwenye uchama wapinzani na wanaccm, nchi za nje tunaziita mabeberu wakati pia hatujui misaada waliongiza nchini. Baada ya hapo maeneo yenye fujo tutaanza kusema lile kabila ndio limetenda mambo hayo. Jamani tunaenda pabaya, hizi nguzo za muungano ni kwisha.
Umoja na uhuru hauletwi na mtutu wa bunduki na kuna mifano mingi sana nchi nyingi zimechafuka kwa kuendesha nchi zao kimabavu.
Naoma tu niseme kwa watanzania wote wapinzani na wa chama tawala tutende haki na tukemee mgawanyiko maana huku tunapoenda kwa mtazamo wangu ni pabaya sana.
Tuiombee hii nchi itoke katika hiji janga na pia watu wote tuombe mungu kuwa nchi itakuwa shwari. UTANZANIA NI KWANZA NA SIO UCHAMA, UDINI, UKABILA.
Mpinzani ni ndugu yako, ni mtoto wako.
Ahsanteni.