Nguzo za TANESCO zilizotengenezwa kwa cement ni hatari, zinazua taharuki

Nguzo za TANESCO zilizotengenezwa kwa cement ni hatari, zinazua taharuki

mangiTz

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2019
Posts
1,820
Reaction score
3,062
Habari wana jamvi,

Kama heading inavyojieleza hizi nguzo za TANESCO ambazo zimetengewa kwa cement uimara wake ni mdogo na ni hatarishi hasa maeneo ya makazi na yenye watu wengi.

Awali nilijua labda zinatengenezwa ndani zinawekwa nondo na seng'enge ili kuongeza uimara kumbe ni tofauti ,hii ni hatari kwasababu kokoto na cement haihusiki kama mti unavyojishika, cement ina tabia ya kujiachia tofauti na nyuzi katika mti , ndio maana hata mti(nguzo ya mti) ikigongwa na kitu kizito uangukaji wake utakuwa tofauti na nguzo ya zege inavyodondoka

Nguzo ya zege inakatika vibaya ikiwa inashuka, unadondoka mithili ya jengo kuporomoka kwa maana itashuka ikiwa vipande vipande tofauti na ya mti ambayo inaweza ikaanguka ila bado imejishikza kidogo palipo katika

Iwapo TANESCO wameamua kutumia hizi za zege vizuri hata ziwekwe nondo ambayo italinda uporomokaji mbaya au kukatika hovyo.

Inasemekana moja iliwahi kuanguka maeneo ya Mwananyamala ikaua mtu.

Kuna haja ya kuziwekea nondo ziwe imara hivi hivi zitakuwa na madhara sana.
Source: ITV

 

Attachments

  • Screenshot_20230719-232459.jpg
    Screenshot_20230719-232459.jpg
    87.5 KB · Views: 20

Nguzo za zege zina steel cage ndani yake, otherwise hao wamefanya uchakachuaji
 
Ni vigumu sana kuamini kuwa wahandisi wa Tanesco waliidhinisha nguzo za zege bila steel reinforcement kutumika!
Ndugu yangu, process ya uzalishaji nguzo za zege inahusisha prestressed steel cage, sielewi hii nguzo hata imekuwaje. Bila shaka kuna mfanyakazi ndani ya kiwanda kapewa hongo na wasomali wanaoagiza nguzo toka South Africa ili itoke moja bila nondo kisha ilete shida wapate pa kusemea, hii ni hujuma, hakuna nguzo ya Zege isiyo na nondo ndani, hata sielewi yani
 
Hatari ni utengenezaji wa cement au kutokuweka nondo / steel reinforcements; Na ni nani alitengeneza bila kuweka hizo nondo ? Hakujua hayo na yupo wapi kwanini asibadilishe na kuweka sawa kwa gharama yake ? Waliotakiwa kupima viwango wapo wapi ?

Sijui kwanini nanusa upigaji hapo anaweza kupewa tender mlamba asali mwingine apate justification ya kubadilisha nguzo zote na huenda akabadilisha zilezile na kuzirudisha hizi kwa kudai kwamba amebadilisha...., Hili taifa limekuwa kama mchwa watu ni kutafuna rasilimali kila kukicha
 
Hivi Afrika kipi tunaweza kwa manufaa yetu na watoto wetu. Hivi tumekuwaje watu waajabu kiasi hiki
 
Ndugu yangu, process ya uzalishaji nguzo za zege inahusisha prestressed steel cage, sielewi hii nguzo hata imekuwaje. Bila shaka kuna mfanyakazi ndani ya kiwanda kapewa hongo na wasomali wanaoagiza nguzo toka South Africa ili itoke moja bila nondo kisha ilete shida wapate pa kusemea, hii ni hujuma, hakuna nguzo ya Zege isiyo na nondo ndani, hata sielewi yani
Bwawa limeingia ruba hapo dili limeanza kubuma
✍️
 
Hiyo ni procurement yenye mkataba, huwezi kusema kirahisi tu "waongeze nondo."
Umeshaingia mkataba wa kimangungo, huchomoi kizembe zembe.

Mkataba unasema nguzo zitakuja mpaka shughuli za usambaza umeme zitakaposita nchini.
Tushapigwa mkao wa shenzitype
✍️
 
Back
Top Bottom