Nguzo za TANESCO zilizotengenezwa kwa cement ni hatari, zinazua taharuki

Za sahv kuna uchakachuaji unafanyika

Ova
 
Hatari sana.

Ziondolewe zote, hazina viwango, mtu kishapiga dili lake hapo.
Sio kweli kwamba hazina viwango, nimejengea line sehemu flani hizo nguvu ni nzuri sana, ingawa Inawezekana kuna uchakachuaji maana waswahili tuna matatizo Sana..
 
Kabisa tena nasikia kiwanda kipo njia ya ile ya bagamoyo, wahuni sana.
Sio wahuni hata kidogo.. kuna mchezo unafanyika.. nilipo kinyume nao ni Derm mkataba walio ingia na Tanesco sijui kama walibadilisha au lah... Maana hata CEIL nae alitaka aanze zalisha hizo nguzo Ila kikwazo ukawa mkataba... Kama wameanza chezeana michezo ya kibiashara Tu.. Ila hizo nguzo zipo zenye ubora Sana na nimezitumia
 
Sio kweli kwamba hazina viwango, nimejengea line sehemu flani hizo nguvu ni nzuri sana, ingawa Inawezekana kuna uchakachuaji maana waswahili tuna matatizo Sana..
Kwa hiyo kama kuna "uchakajuaji" zisiondolewe? Zibaki kuwepo?

Tusizungushane kwa maneno, duniani huko wanarudisha mpaka magari kwa maelfu yanayowagharimu viwanda vyake mabilioni ya mapesa kwa akuwa yameleta pengine ajali moja tu.

Tusicheze na maneno, tunaongelea usalama wa watu na mali zao.

Wewe umezitumia tu, ulizifanyia "test" zipi za kitaalam kugunduwa kuwa zinahodhi viwango vinavyokubalika, na hizo test zilifanyika wapi?
 
Tuache siasa mkuu!

Sitetei chochote naangalia Kwa pande zote... Ndio maana hata Derm sijawakubali namna walivyo cheza kuingia ubia na Tanesco kuhusu huu mradi wa nguzo, labda hivi karibuni wawe wamrbadilisha makubaliano...

CEIL pia walikuwa wanataka zalisha hizo nguzo na wadau wengine.. uchunguzi ufanyike.. itajulikana.. Inawezekana pia ikawa michezo kibiashara kuharibiana.. Hiyo nguzo ichumguzwe itajulikana kama ni ya derm au ilipachikwaaa simple.. Tu maana kwenye ujenzi huwa nguzo zinawekwaaa.. mwingine kama ana Nia mbaya anaweza akaja akaweka na zake mbili Tatu juu
 
Habari wana jamvi,
Kama heading inavyojieleza hizi nguzo za TANESCO ambazo zimetengewa kwa cement uimara wake ni mdogo na ni hatarishi hasa maeneo ya makazi na yenye watu wengi.
Hapa kweli watu procurement na assessment wanahusika. Kama hakuna prestressed steel cage and construction moth ndani ya hizo nguzo ni janga litakaloleta maafa kilasiku. Maana hizo nguzo bila nondo na waya ndani yake zinaweza kudondoka zenyewe pale upepo unapozidi.
Dah kila sehemu watu wanapigašŸ˜©šŸ¤”
 
Mkuu katika hili umepatikanašŸ˜€. Ngoja watu waanze kuiporomoshea matusi na rejections Tanesco ili washtuke.
Kwanini lakini kila sehemu kuna uzembe tu?🄵
 
Kabisa tena nasikia kiwanda kipo njia ya ile ya bagamoyo, wahuni sana.
Hiko ni cha kuvamiwa na wakaguzi wa serikali, wakijiridhisha ni nguzo zilizokosa ubora wawajibishwe. Mtu alishafariki kwa upumbavu wa watu wachache, je yakitokea maafa makubwa zaidi itakuwaje? Itafikia kipindi tutaanza kutafutana mtaani kwa kila mzembe kwenye nafasi yake hasa viongozi na kuwajibishana kwa sheria za mtaani.
 
Hivi ni kweli, kweli kabisa kweli! Naihurumia nchi yangu Tanganyika.
 
We ndiyo unakwenda kwenye siasa.


Mradi nguzo mpaka zimeua na kuleta madhara kwa mali za raia, mimi nasema hazifai.

Teknolojia ya miaka ya 1800's tunaitumiaje leo hii bila kuiboresha? Are we that stupid?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…