Nguzo za TANESCO zilizotengenezwa kwa cement ni hatari, zinazua taharuki

Hatari sana kama hawakuweka nyavu na vinondo vya 10mm ndani.

Hapo watu wa production wamepiga mzigo.

Hiyo nguzo iliyodondoka hapo ilikuwa hamna cha nondo wala mesh wire.
 
Ni upuuzi sana inakuwaje washindwe kuweka hata meshwire? Nguzo za Umeme za miti Bado ni salama tofauti na hizi.

Kwa mfano nakumbuka zile nguzo zilikuwa zinaagizwa south Africa Hadi inawekwa kubeba nyaya za umeme unakuta Bado inachemka na Ile treatment ya dawa na zimedumu sana zaidi ya miaka 30.

Sasa Jiwe aliposema zianze kuletwa nguzo za Bongo kama kawaida wanapata rangi,miti haijakomaa na hivyo ndani ya mda mfupi inaoza.

Kiufupi Watanzania sijui tukoje aisee
 
Hiyo ni procurement yenye mkataba, huwezi kusema kirahisi tu "waongeze nondo."
Umeshaingia mkataba wa kimangungo, huchomoi kizembe zembe.

Mkataba unasema nguzo zitakuja mpaka shughuli za usambaza umeme zitakaposita nchini.
Mkataba ni wa ku-supply nguzo zisizo na viwango ? Bila steel reinforcements za kutosha concrete sio stable (hilo lipo wazi)

Ndio maana hapa nanusa hujuma au uzembe; rahisi tu waangalie hio nguzo ilitoka batch gani siku gani, nani alikuwa zamu na kina nani walipekeka kufanya installation (waulizwe kama waliweka ile ya kiwandani au walitoa zao wanapojua) na kama kuna huu uwezekano zote ambazo zimekuwa installed zichekiwe kama zimechezewa... Hii checks and balances itawafanya wenye mchezo huu waogope kuendeleza hii tabia mbovu
 
Ni hatari sana hizi nguzo za miti bado ni salama kushinda hizi

Angalau ya mti ikiwa na hitilafu huwa inakuwa na ishara ,
 
Nguzo zinajengwa na wapigaji kuanzia juu mpaka chini wote wezi watupu.

Poleni huko.
 
Tindikali msikilize mdau , hizi zinatakiwa ziwe na iron steel kwa ubora sidhani kama kuna mhandisi anaweza kukubali nguzo kupitisha zitumike bila kuwa na nondo kama mimi mwenyewe natambua ikiwa haina inakuwa hatari mhandisi ashindwe kutambua
 
Hii ni aibu, huu mradi wa fedha nyingi alafu kweli tunaweka nguzo za namna hii? Zichukuliwe hatua haraka kabla haijaibuka kashfa nyingine kubwa zaidi.
 
chochote chenye viashiria vya kuzua taharuki chi hii polisi huwa sharp wanaingilia kati vip hapo wajafika kutoa wito kwa wahusika kuhojiwa
 
Mkuu katika hili umepatikana😀. Ngoja watu waanze kuiporomoshea matusi na rejections Tanesco ili washtuke.
Kwanini lakini kila sehemu kuna uzembe tu?🥵
Wizara nyingi zimeoza ukitaka kujua ingia kwenye hiyo wizara ndio unajua kuna zingine mtu anashindwa kwasababu watu tayari wametengeneza mizizi yao huwatoi
 
We ndiyo unakwenda kwenye siasa.

Mradi nguzo mpaka zimeua na kuleta madhara kwa mali za raia, mimi nasema hazifai.

Teknolojia ya miaka ya 1800's tunaitumiaje leo hii bila kuiboresha? Are we that stupid?
Sawa mkuu.. Yakwisheee
 
Umeme pia ni hatare zidisheni umakini sw.
 
Mkuu katika hili umepatikana😀. Ngoja watu waanze kuiporomoshea matusi na rejections Tanesco ili washtuke.
Kwanini lakini kila sehemu kuna uzembe tu?🥵
Uzembe upo hatukai.. na ninaona ni desturi ya Tanzania kutoa maboko... Niambie idara gani Tanzania imenyooka... Zaidi ya JWTZ nao kuna mapungufu ingawa wao ndio wanatuibua kama Taifa, kwingine kote huko maviii matupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…