shahid365
JF-Expert Member
- Jul 29, 2018
- 518
- 420
Maoni yangu YAHESHIMIWESi kweli
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maoni yangu YAHESHIMIWESi kweli
tunamuweka kundi la kina Yuda Iskariot [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna jamaa alsema hamjui jay moe ila anashabikia hip pop..huyu tunamuweka kundi gan?
Umetisha! Ila kwenye jina la shule, ni Irambo, sio Iramba.Aha! Aha! Jay Moe (Jay Moe)
Bongo Records (Bongo Records)
Maisha Ya Boarding (Aaah)
Ulimwengu ndo mama! (Aaah)! (Aaah)! (Aaah)!
UBETI 1
Maisha ya boarding noma, Jay Moe nimesoma,
Na ndo lipo nlipata neno Ulimwengu ndo mama,
Primary sikupass, sikuwa na nyota njema,
Ikabidi nikasome boarding kuziepuka lawama,
Mi n'navyoona maisha ya boarding yana raha na noma,
Ila wanafunzi wengine kwao hayakuwa salama,
Kama wewe Form One shida kibao utapata,
Kuna kuibiwa, kuna kuna adhabu, maisha kama vita
Siku za mwanzoni ni siku za kufanya tathmini,
Niliogopa sana mambo ya kupiga simu chooni,
Viongozi wenyewe wazamu, hawana akili timamu,
Bakora mtindo mmoja mpaka fulani atoke damu!
Hapo binamu sikugoma, kazi zao nilifanya
Ili nisiwe ukingoni mwa sakafu na mbio za panya,
Morning jioni niko job, me ni denti au mjeshi?
Shule za boarding bwana mizengwe haiishi,
Ukiongea Kiswahili adhabu "Swahili speaker"!
Kweli, huu ungwana? Hii si ni lugha ya taifa?
Mbona inakuwa adhabu? Mi sikusoma English Media,
Shule ya msingi Uswahilini, huko ni Swahili Media
KIITIKIO
Tunanyanyasikaa, faidikaa
Twatesekaa, maisha ya boarding,
Chakula shidaa, twahangaikaa
Taabikaa, maisha ya boarding X2
UBETI 2
Asubuhi nakwenda bwaloni nakuta uji,
Uji bila sukari ni mchemsho wa sembe na maji
Shule ina kantini kuna chai bila kushangaa
Itakubidi uweke iwe freshi ili usife njaa
Kwani mchana ni soo, kote kabichi na ugali
Wali mpaka siku ya sherehe na siku hiyo ni hatari
Waalimu fimbo mkononi kisa wali na nyama!
Hapo ndipo utauona ubora wa baba na mama
Teacher class anateach sum, nje watu wanapuff some,
Mtoto wa mama bora usome day bongo Dar es Salaam
Iramba hakuna tuition, Iramba hakuna fashion,
Kama unakwenda town hadi utegee gari ya Mission
Term inapoanza watu wako safi kama bosi
Sababu hakuna pombe hapo ni pamba misosi
Baada ya miezi miwili watu wamechoka ile mbaya
Wakianza kula ugali hali imezidi kuwa mbaya,
Wengine wana majiko mpaka pilau wanapika,
Ila teacher akishtuka basi na shule itakwisha!
Walioogopa mambo Shauritanga si mnakumbuka?
Walioogopa hata wasifanye jipu likajatubuka
KIITIKIO MARA 2
UBETI 3
Wengine wanafukuzwa shule kwa makosa tofauti,
Huyu hula bangi, huyu usiku alifumwa na binti
Yaani usiku mchana kasheshe, inahitaji uwe fiti
Ili usifukuzwe shule, ukifukuzwa itakuwa vipi?
Kama una dem subiri hadi shule kufungwa,
Sehem ni town tu, Dar es Salaam wanafugwa
Wanaojifanya wagonjwa mida ya break wanapona,
Ilimradi wazunguke wee kusaka waschana,
Baada ya break kwa bwenini story kila kitanda,
Wengine utaskia ooh Carolina ana mimba!
Na shule inakuwa chungu kwenye zamu za kwenda shamba,
Wajanja hawakwenda, wengi waliokwenda ni washamba
Watu hawaogi wiki labda iwe weekendi
Baridi kama Urusi maji bafuni hayapandi,
Watu umande kila siku, maisha ya boarding hayafai
Hata awe dada mkuu wakimwotea hakatai
Wengine wanakwenda wajiseti huku mpira hawachezi
Na vingine vingi mtu yeyote kumaliza hawezi
Ndo maana boarding zenye elimu ni za Seminari
Shule kama Iramba mwanao ni lazima atafeli!
KIITIKIO MARA 2
Maisha ya boarding bwana!
Bora mlosoma day
Maisha ya boarding siyo mchezo
Utafikiri kambi ya mafunzo
KIITIKIO
Tunanyanyasikaa, faidikaa
Twatesekaa, maisha ya boarding,
Chakula shidaa, twahangaikaa
Taabikaa, maisha ya boarding X2
pamojaUmetisha! Ila kwenye jina la shule, ni Irambo, sio Iramba.