NHC acheni "uongo" na taarifa za kizushi

NHC acheni "uongo" na taarifa za kizushi

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
Tatizo la Nchi hii Waandishi wetu hawako inquisitive na analytical ni watu wa mihemuko na kukimbilia matukio tu!

Hili suala la huyu mtu anayedaiwa kutaka kuuza nyumba ya NHC inaripotiwa kizushi sana utadhani watu wote ni wajinga!

Ni hivi, huo ni utaratibu uliozoeleka sana hapa Nchini na unaeleweka kote na siyo NHC tu!

Hata " fremu" za Halmashauri au Manispaa huwa watu wanaachiana kwa kulipana fedha ndefu sana (kati ya milioni 7 hadi milioni 15 ) na hiyo siyo kuuziana umiliki kwa maana ya " title deed transfer"!

Hakuna mtu mjinga tena mpangaji wa NHC anayeweza kuuza kwa ku- transfer title deed ya NHC kwa MTU! Hao NHC waje basi na details za hiyo transaction kwenye public domain tuone kama siyo ukilaza tu!
===

Mpangaji aliyetaka kuuza nyumba ya NHC anaswa

 
Nimeiona hiyo habari mahala iko short sana, haina maelezo ya kutosha, nahisi jamaa atakuwa ametengenezewa mtego aonekane tapeli ila lazima patakuwa na sababu nyuma ya pazia wanatuficha.
 
Hiyo habari nimeiona ITV usiku wa leo

Bongo kuna ma Public relation officers hakuna waandishi kabisa

Mjinga gani anaweza kuuziwa nyumba ya NHC kwa 8 million nae akanunua? Hayo ni madili yao na inawezekana Dalali kawatapeli ndio ikabidi wasanue chezo lote
 
Nimeiona hiyo taarifa imeripotiwa tofauti kabisa kwa uelewa wangu yule jamaa alikuwa hauzi hiyo nyumba bali alikuwa anuza haki yake ya kupangisha hiyo nyumba.

Hizo nyumba za NHC watu wanauziana sana haki ya. kupangishana kimyakimya
 
nimeiona hiyo taarifa imeripotiwa tofauti kabisa kwa uelewa wangu yule jamaa alikuwa hauzi hiyo nyumba bali alikuwa anuza haki yake ya kupangisha hiyo nyumba. Hizo nyumba za NHC watu wanauziana sana haki ya. kupangishana kimyakimya
Mkataba wa upangaji unaruhusu watu kuuziana hiyo haki ya upangaji? Tusirudi enzi ziĺe za mtu ukuwa tapeli /Fisadi unasifiwa kuwa mjanja wa mjini.
 
Wanaita kumvua mtu nyumba au kukuuzia mtu upangaji!

Hili jambo la kawaida Sana. Ukitaka nyumba ukiongea na NHC, wanakuunganisha na mtu anayeshindwa Kodi ili umvue ukazi,uwe mlipa Kodi, kutegemea na eneo malipo yapo 10m, 20m, Hadi 60M.

Niliona ujinga Bora kujenga! Kuliko maghorofa yasiyo na lift
 
Tanzania pekee ndio imejaa watu wahuni wengi maofisini, waadilifu wengi wapo mitaani
 
Hujui chochote! Wewe ni ki.laza! Popote pale demand ya kitu ikishakuwa kubwa kutokana na scarcity basi mambo kama hayo hayaepukiki! Tukiwambia wazazi wenu walipe ada msome shule nzuri, vichwa vyenu vichemke hawataki! Wanakimbilia shule za elimu bure,kumbe wanalipia gharama kubwa kutengenezewa mabumunda vichwani!
vyovyote itakavyokuwa gharama anapaswa kulipwa NHC, iwe kodi marekebisho ama
upuuzi wowote hii tabia inapaswa ikome
 
Wewe unaishi wapi mkuu ,hii issue ni very public hadi Azam imerushwa kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku huu and above all ipo kwenye numerous social media !
Hatujasikia hizo habari. Iweke kwa weledi na ukamilifu na sisi tuweze kuchangia. Hapa tumeishia kusoma hisia zako tu. No objectivity.
 
Tanzania pekee ndio imejaa watu wahuni wengi maofisini, waadilifu wengi wapo mitaani
Labda tatizo liko humo maofisini na sio kwa watu...inawezekana hata hao wa mtaani wakiingia ofisini nao watakuwa wahuni..
 
Back
Top Bottom