Tatizo la Nchi hii Waandishi wetu hawako inquisitive na analytical ni watu wa mihemuko na kukimbilia matukio tu!
Hili suala la huyu mtu anayedaiwa kutaka kuuza nyumba ya NHC inaripotiwa kizushi sana utadhani watu wote ni wajinga!
Ni hivi, huo ni utaratibu uliozoeleka sana hapa Nchini na unaeleweka kote na siyo NHC tu!
Hata " fremu" za Halmashauri au Manispaa huwa watu wanaachiana kwa kulipana fedha ndefu sana (kati ya milioni 7 hadi milioni 15 ) na hiyo siyo kuuziana umiliki kwa maana ya " title deed transfer"!
Hakuna mtu mjinga tena mpangaji wa NHC anayeweza kuuza kwa ku- transfer title deed ya NHC kwa MTU! Hao NHC waje basi na details za hiyo transaction kwenye public domain tuone kama siyo ukilaza tu!
===
Nimeiona hiyo habari mahala iko short sana, haina maelezo ya kutosha, nahisi jamaa atakuwa ametengenezewa mtego aonekane tapeli ila lazima patakuwa na sababu nyuma ya pazia wanatuficha.
Bongo kuna ma Public relation officers hakuna waandishi kabisa
Mjinga gani anaweza kuuziwa nyumba ya NHC kwa 8 million nae akanunua? Hayo ni madili yao na inawezekana Dalali kawatapeli ndio ikabidi wasanue chezo lote
Nimeiona hiyo taarifa imeripotiwa tofauti kabisa kwa uelewa wangu yule jamaa alikuwa hauzi hiyo nyumba bali alikuwa anuza haki yake ya kupangisha hiyo nyumba.
Hizo nyumba za NHC watu wanauziana sana haki ya. kupangishana kimyakimya
nimeiona hiyo taarifa imeripotiwa tofauti kabisa kwa uelewa wangu yule jamaa alikuwa hauzi hiyo nyumba bali alikuwa anuza haki yake ya kupangisha hiyo nyumba. Hizo nyumba za NHC watu wanauziana sana haki ya. kupangishana kimyakimya
Wanaita kumvua mtu nyumba au kukuuzia mtu upangaji!
Hili jambo la kawaida Sana. Ukitaka nyumba ukiongea na NHC, wanakuunganisha na mtu anayeshindwa Kodi ili umvue ukazi,uwe mlipa Kodi, kutegemea na eneo malipo yapo 10m, 20m, Hadi 60M.
Niliona ujinga Bora kujenga! Kuliko maghorofa yasiyo na lift
Hujui chochote! Wewe ni ki.laza! Popote pale demand ya kitu ikishakuwa kubwa kutokana na scarcity basi mambo kama hayo hayaepukiki! Tukiwambia wazazi wenu walipe ada msome shule nzuri, vichwa vyenu vichemke hawataki! Wanakimbilia shule za elimu bure,kumbe wanalipia gharama kubwa kutengenezewa mabumunda vichwani!
Wewe unaishi wapi mkuu ,hii issue ni very public hadi Azam imerushwa kwenye taarifa ya habari saa 2 usiku huu and above all ipo kwenye numerous social media !