NHC K'NJARO YAIPIGA JEKI JK.NYERERE SEC MIFUKO 50 YA SARUJI UKARABATI WA SHULE

NHC K'NJARO YAIPIGA JEKI JK.NYERERE SEC MIFUKO 50 YA SARUJI UKARABATI WA SHULE

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
NHC K'NJARO YAIPIGA JEKI JK.NYERERE SEC MIFUKO 50 UKARABATI WA SHULE

25 Julai 2024
Na Mwandishi Wetu,Moshi

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)mkoani Kilimanjaro limetoa msaada wa mifuko 50 ya simenti yenye thamani ya Tshs. 1,000,000/= kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari J.K Nyerere iliyopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Msaada huo umetolewa Leo na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Hamad Abdallah kufuatia ombi lililowasilishwa kwake na uongozi wa shule hiyo.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Bi. Mwajuma Nasombe na Meneja wa NHC Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Juma Kiaramba

Meneja Kiaramba amesema ni sera ya Shirika kusaidia shughuli za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kwani Shirika hilo linafanya kazi kwenye jamiii na lina wajibu wa kusaidia sekta mbalimbali za Maendeleo.

Kiaramba alieleza kwamba kwa Manispaa ya Moshi hii si mara ya kwanza Shirika kutoa msaada kwani mwaka 2022 Shirika lilisaidia ukarabati wa Shule ya Msingi JK Nyerere.

Kwa upande wake Mkurugenzi Bi. Mwajuma amelishukuru Shirika kwa kuendelea kusaidia huduma mbali mbali za kijamiii katika Halmashauri yake kutokana na kazi wanazofanya na kuomba Shirika liendelee kusaidia maeneo mengine katika Manispaa yake.
 
Back
Top Bottom