KERO NHIF imeikosesha nchi utawala wa sheria

KERO NHIF imeikosesha nchi utawala wa sheria

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hapa ungekuja na hoja za namna gani watanzania waweze kujiunga na bima na sio NHIF tu, bali na bima zote.
Kwa sabb hizo takwinu za wenzetu wamefanyaje kufanikiwa wananchi wao kujiunga na bima ya afya ndio ingekuwa point ili kuweza kutoka hapa tulipo kama Taifa na sio kuendelea kutoa data hapa haitasaidia wakati wananchi kujiunga na bima ya afya kwa hiari hakuna.
Ni sawa JMT walikua wakwanza kuazisha NHIF lakini utayari wa watanzania uko wapi, ni rahisi kulipia bima ya gari au nyumba lakini kukata bima ya afya sio utamaduni wetu.
Ufike wakati tukubali kuwa sisi watanzania hatuko tayari kulinda afya zetu bali tunapenda sana kulalamika
Wewe utakuwa mwana NHIF tuuuu!
 
Wewe utakuwa mwana NHIF tuuuu!
Mimi kama unavyofikiri ila nimenufaika na huduma za NHIF mimi na familia yangu ndio nimekuambia kuja na hoja za kama serikali ifanye nini ili wanachi wengi zaidi wajiunge na bima na kuwa na uhakika wa matibabu.
Yaani hivi kuwa na utamaduni wa kukata bima za afya kama vile tunapokata bima za gari na nyumba bila hata ya kujua ni lini litapata ajalu au ni lini nyumba yako itapata ajal ya moto.
 
Wewe utakuwa mwana NHIF tuuuu!
Sio kama unavyodhani bali mimi nilikua muhanga kama wewe wa kuilaumu serikali na NHIF kuwa mbovu inatoa huduma kwa upendeleo, ila kumbe nilikua najidanfanya mwenyewe nilikua na biashara yangu nimeikatia bima, gari nimeikatia bima na hata nyumba nimeikatia lakini sikua na elimu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya ili kulinda afya yangu na wapendwa wangu. Hivyo baadaye nikaamua kutafuta bima ya afya ndio nikaona umuhimu wake.

Rafiki sio kila mtu anasema mazuri kuhusu NHIF ni mhusika ila wengine ni watu tulionufaika na tunaendelea kunufaika na huduma za NHIF broo
 
Bila kuwalazimisha watumishi wa umma kujiunga na huu mfuko, sidhani kama kuna mtumishi mwenye akili timamu angebaki!!
 
NHIF wamekuwa matapeli siku hizi. Hawalipi watoa huduma wao kwa wakati na hata wakikulipa pesa zinakatwa ovyo.

NHIF wawe wawazi tu kuwa wao ndo sababu wachangiaji mfuko hawapati huduma nzuri..
 
Mimi kama unavyofikiri ila nimenufaika na huduma za NHIF mimi na familia yangu ndio nimekuambia kuja na hoja za kama serikali ifanye nini ili wanachi wengi zaidi wajiunge na bima na kuwa na uhakika wa matibabu.
Yaani hivi kuwa na utamaduni wa kukata bima za afya kama vile tunapokata bima za gari na nyumba bila hata ya kujua ni lini litapata ajalu au ni lini nyumba yako itapata ajal ya moto.
Serikali na wana NHIF waache wizi na ufisadi, kila kitu kitakuwa sawa.
 
Sio kama unavyodhani bali mimi nilikua muhanga kama wewe wa kuilaumu serikali na NHIF kuwa mbovu inatoa huduma kwa upendeleo, ila kumbe nilikua najidanfanya mwenyewe nilikua na biashara yangu nimeikatia bima, gari nimeikatia bima na hata nyumba nimeikatia lakini sikua na elimu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya ili kulinda afya yangu na wapendwa wangu. Hivyo baadaye nikaamua kutafuta bima ya afya ndio nikaona umuhimu wake.

Rafiki sio kila mtu anasema mazuri kuhusu NHIF ni mhusika ila wengine ni watu tulionufaika na tunaendelea kunufaika na huduma za NHIF broo
Mimi ninayo NHIF kwa muda mrefu. Naijua ikiwa bora, kabla wahusika hawajaanza utapeli, na pia naijua sasa walivyoivuruga! Hivyo nina uhakika na ninachosema!
 
Zaidi ya 80% ya mapato ya vituo vyote vilivyosajiliwa na Mfuko vinategemea malipo yatokanayo na kutibu wanachama wa Mfuko...tembelea vituo angalia katika watu 10 utakuta walau 8 wana kadi za NHIF.

Kila mwenye kituo anatamani kufanya biashara na NHIF toka anapoanza. Hivyo NHIF ni chaguo namba 1 kwa watoa huduma wote.

Kuhusu huduma kwa wateja, Mfuko umeweka wataalamu wake vituoni kwa kuanza na vituo ngazi ya kliniki za madaktari bingwa hadi hospitali ya Taifa ya Rufaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa ubora wa huduma na utambuzi wa wanufaika. Mwanachama anapopata changamoto

kituoni inatatuliwa papo hapo kwa kutumia wataalamu waetu au hata kwa kupiga simu bila malipo namba 199 saa 24 kila siku.

Endapo una tatizo jengine unaweza kuliwasilisha moja kwa moja NHIF kwa barua pepe info@nhif.or.tz, simu namba 199, kufika ofisini au simu ya kutoa taarifa za siri namba 0800111163. Karibu tukuhudumie
Hili jibu ni la Kisiasa sana, nyie hamlipi hospitali kwa wakati , ukilinganisha na washindani wenu, ndio maana wateja wenye card zenu wanafurumushwa kwenye hospitali za binafsi
 
nimekata NHIF TIMIZA AFYA sh 9,87000/ nimeenda kutibiwa magoti CCBRT walinikataa mpaka nianzie hospital za chini wakati huo ninaumwa sana goti nitibiwe na wao ni mabingwa wa mifupa, nimeenda SAIFEE hospital nimetoa kadi yangu hiyo ya Nhif nitibiwe wamenikatalia hawapokei kadi hiyo ya NHIF wanapokea za mawaziri, wabunge na familia zao na wafanyakazi wa makampuni na familia zao nasemaje. ikiisha muda wake hii card sirudii tena kukata NHIF mpaka nakufa sikati , sasa hivi natumia cash na kadi ninayo inaisha mwaka 25/4/2024. ukimuona mtu humu jf anatetea nhif huyo ni mfanyakazi au familia za wafanya kazi serikalini kadi wanapata bure hawaoni uchungu,NHIF waende saifee hospital wakaulize kama timiza afya wanapokea uwasikilize watasemaje
 
Utendaji dhaifu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF umeitweza nchi kwa kiwango cha kufanya Sheria ya Bima ya Afya kusiginwa kwa soli za watoa huduma za afya wa sekta zote za umma na binafsi.

Hospitali ya taifa ukiwa na NHIF utadhihakiwa na kuhudumiwa mwishoni au hata tabibu akakujibu ana hudhuru kumbe anakukwepa tu kisa huna fedha taslimu (cash). Wagonjwa wenye fedha taslimu ni wafalme kuliko wenye NHIF.

Wamiliki wa sehemu za kutoa huduma za afya; wenye asili ya Asia ndiyo hawataki asilani kuona mzimu-dhurka unaoitwa NHIF, wanaiona kama chama cha siasa tu.

Hawa wenzetu hawarembi, amri yao ni moja tu "toa taslimu au hangamia" Hatupokei NHIF.

Kongole kwa Hindu Mandal ambao wao angalau wanapokea NHIF lakini pia kwa mipaka kwamba baadhi ya huduma lipia taslimu siyo kwa NHIF.

Hospitali ya taifa hoja yao ni dhaifu sana kwamba mgonjwa akitumia NHIF matabibu hawapati ela.

Madai ya hospitali binafsi ni kuwa inawachukuwa muda mrefu kulipwa na NHIF.

Hospitali zingine binafsi zinadai kwamba NHIF imewaletea mafuriko ya wagonjwa hata wanaotibika kwenye hospitali na vituo vya Manispaa.

Tumefika mahali watanzania tunabaguliwa na taasisi za serikali yetu wenyewe; na zile za binafsi kupata huduma za afya ambazo ni haki zetu za msingi za kuishi.

Ila akienda kiongozi mkubwa na NHIF mkononi kote huko atapokelewa na kuhudumiwa kama mfalme utadhani amebeba gunia lililojaa minoti kuwapelekea.

NHIF inadharauliwa kama ripoti za ukaguzi za CAG zinavyodharauliwa. Hii hali inatweza sovereignty na commonwealth ya nchi.

Kwanini taasisi za kutoa huduma zivunje sheria ya nchi? Kwanini NHIF ishindwe ku-deliver?

Je, NHIF ifutwe turudi kwenye uzamani wa kutumia taslimu?

Kwanini taasisi ya serikali ishindwe kuamini taasisi mwenza ya serikali? Hospitali ya taifa ikatae kutambua NHIF ilhali zote ni za serikali hiyo hiyo moja?

"Wewe... una keshi (cash)? Kama una NHIF mmmh..."

Kwingine utasikia.

"Wewe iko na cash? Kama bima mimi napokea Jubilee na Strategies peke yake, hiyo NHIF, SHIB, CHF, NSSF na TIKA mimi hapana taka hapa"

Wakati fulani utaambiwa hivi:

"Kama iko cash Dr. Rajesh Kumar bingwa iko taona wewe saa hii, lakini kama iko NHIF subiri intern doctor taona wewe jioni sana"

NIDA imetweza nchi.
EWURA imetweza nchi.
REA imetweza nchi.
TANESCO imetweza nchi.
DAWASA imetweza nchi.
NHIF imetweza nchi.
Tume ya Katiba imetweza nchi.

Utawala wa Sheria na Utawala Bora viko wapi au mkoloni Sir Richard Gordon Turnbull aliondoka navyo Disemba 9, 1961?

Tafakari yafuatayo:

1. Kwanini NHIF ilifilisika na kulazimu kusukwa upya kama ina ukiritimba wa soko?

2. NHIF iko kwenye soko la walaji wa huduma zake (consumer market) lenye ukubwa wa walaji 61ml kwa maana kwamba kila mtu lazima augue maana tuko kwenye nchi ya kitropiki. Katika hao walaji 61ml wafanyakazi ni wangapi katika soko hili?

3. Tz NHIF hadi 2019 ilikuwa na jumla ya wanufaika 4,856,062 sawa na 9% ya Watz wote kwa wakati huo.

4. Hadi 2021 JMT ilikuwa na:-
4.0 Zahanati 7189.
4.1 Vituo vya Afya 956.
4.2 Hospitali 404
Jumla 8549.

5. Kwahiyo 9% ya Watz wa NHIF ndiyo michango yao inaendesha hizo health facilities 8549 vya umma na binafsi?

6. Kwahiyo 91% ya Watz hawaugui? Na kama wakiugua na siyo wanachama wa NHIF je, wanatibiwa kwa mfumo upi wa malipo? Je, kati ya 9% na 91% nani wamewezesha health facilities 8549 ziendelee kuwepo?

7. Unadhani Tz NHIF imeshindwa nini kujipatia walao 50% ya wanufaika wa huduma zake kwenye soko la walaji 61ml? Ikabaki kuwa na wanufaika chini ya 10% ya Watz?

8. Tz NHIF ilipofilisika hapo nyuma je, hizo health facilities 8549 zilifungwa kwa kukosa wateja kufuatia NHIF kufilisika?

9. Kama hazikufungwa je, zilitoa huduma bure?

10. Kenya NHIF hadi 2023 ina wanachama 26.9ml. Wanachama wa msingi (principal members) 14ml, wanachama-tegemezi (dependants) 12.9ml, jumla 26.9ml sawa na 48.6% ya watu wa Kenya wapatao 55,348,811 yaani Kenya NHIF inakaribia kufikia nusu ya Wakenya.

11. Kenya NHIF ilijifunza Tz namna ya kuanzisha na kuendesha NHIF.

12. Ghana NHIF pia kama ilivyokuwa Kenya NHIF ilijifunza na kuiga kutoka Tz NHIF.

13. Katika Afrika, JMT ndiyo ilikuwa kinara wa kubuni na kutekeleza mpango wa NHIF.

14. Sasa Kenya NHIF imefikia wanachama 26.9ml sawa na 48.6% ya watu wa Kenya DHIDI ya Tz NHIF yenye wanachama 4,856,062 sawa na 9% ya watu wa nchi.

15. Kenya ilikuja kujifunza wazo JMT na kujiwahi kutekeleza wakati JMT ikiendelea kubaki kwenye nadharia za ukosefu wa bajeti na mijadala ya nani wawe viongozi kwenye bodi na menejimenti. Kenya wakatutangulia kwenye utekelezaji.

16. Ebu mtu mmoja ataje walao matatizo 5 tu ya Tz NHIF:-

1.
2.
3.
4.
5.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app

----
MAJIBU YA NHIFTZ
Sijamaliza kusoma yote. Lakini siyo NHIF tu kila sekta, taasisi, Wizara , halmashauri mambo ni ovyo. Mfano Tanesco tu, wamewezesha biashara ya jenereta mpaka madukani zimeisha, halafu Rais eti anatoa tamko waendelee na mgawo kwa miezi 6 zaidi,ina maana hata mvua zikianza waendelee na mgawo mpaka miezi 6. Dawa itatuingia muda si mrefu tutaingia barabarani hata kabla ya uchaguzi. Acha waendelee kuchochea Kuni tu.
 
nimekata NHIF TIMIZA AFYA sh 9,87000/ nimeenda kutibiwa magoti CCBRT walinikataa mpaka nianzie hospital za chini wakati huo ninaumwa sana goti nitibiwe na wao ni mabingwa wa mifupa, nimeenda SAIFEE hospital nimetoa kadi yangu hiyo ya Nhif nitibiwe wamenikatalia hawapokei kadi hiyo ya NHIF wanapokea za mawaziri, wabunge na familia zao na wafanyakazi wa makampuni na familia zao nasemaje. ikiisha muda wake hii card sirudii tena kukata NHIF mpaka nakufa sikati , sasa hivi natumia cash na kadi ninayo inaisha mwaka 25/4/2024. ukimuona mtu humu jf anatetea nhif huyo ni mfanyakazi au familia za wafanya kazi serikalini kadi wanapata bure hawaoni uchungu,NHIF waende saifee hospital wakaulize kama timiza afya wanapokea uwasikilize watasemaje
Umewapiga machawa wa NHIF utosini kwa kitu kizito. Hao ndiyo walifisi Mfuko wakishirikiana na Anna wa Bodi ya Wakurugenzi.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la Tanzania ni Umasikini tu

Tukiweza
 
Sijamaliza kusoma yote. Lakini siyo NHIF tu kila sekta, taasisi, Wizara , halmashauri mambo ni ovyo. Mfano Tanesco tu, wamewezesha biashara ya jenereta mpaka madukani zimeisha, halafu Rais eti anatoa tamko waendelee na mgawo kwa miezi 6 zaidi,ina maana hata mvua zikianza waendelee na mgawo mpaka miezi 6. Dawa itatuingia muda si mrefu tutaingia barabarani hata kabla ya uchaguzi. Acha waendelee kuchochea Kuni tu.
Majenereta na mafuta ili inwadhRi na ludbA (zisome kiarabu) watengeneze ela, STATE CAPTURE.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom