kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Watu wetu wengi ni maskini sana na wajinga wasiofuata kanuni za afya kujilinda dhidi ya maradhi. Nchi haina maji, umeme, barabara, chakula na nyumba Bora za kuishi toshelezi kumudu kupambana na maambukizi. Elimu ya afya na huduma za afya haziwafikii watu wote.
Watu wetu wanazo tabia nyingi mno ambazo ni hatarishi kwa afya zao zinazowafanya waugue wakati wowote na kuhitaji kutibiwa.
Huwezi kumuwekea bima ya afya mtu ambae Hana maji safi, umeme, chakula, choo Wala chandarua. Huwezi kumuwekea bima mtu ambae anapanda pikipiki bila kuvaa helmet, havai viatu, aña chumba kimoja yeye na watoto na mifugo yake, asiyetumia condom, choo, kunawa mikono, nk. Watu wa aina hii wanaugua familia nzima kila siku na kuhitaji matibabu ya kila siku na kila wakati kwenye hospitali tofauti tofauti.
Serikali lazimà ipunguze umaskini, itoe elimu ya afya na iboreshe maisha ya wananchi ili wasiugue mara kwa mara kabla ya kupanua wigo wa wadau wa NHIF, vinginevyo mfuko uta collapse.
Maskini hawekewi bima