NHIF wananyima watu haki za msingi kwa sababu zisizo na mashiko

NHIF wananyima watu haki za msingi kwa sababu zisizo na mashiko

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Naomba niaze na maswali chokozi haya yafuatayo kabla ya kwenda kwenye hoja yangu;

1. Hivi mtu anaweza akafoji mzazi, mtoto, mwenza, mkwe nk

2. Ikiwa ni kweli mtu anaweza akafoji hao watu, je kwenye mfuko wa bima ya afya kunakuwa na hasara gani?

3. Hivi mtu anaweza kusajiliwa mara mbili kwenye NHIF?

4.Hivi nini maana ya kuweka ukomo wa watu na vigezo fulani fulani kwa mtumishi kuhusu wategemezi kwenye bima ya afya?

5. Mtumishi akitaka kutuma maombi ya bima ya afya je, afisa utumishi anapitishiwa fomu ya bima kwa ajili gani?

6. Je ni lipi lengo la serikali kutaka watu wakate bima ya afya?

Mara nyingi kwenye huduma za jamii (hasa ajira na kazi) tunakumbana na changamoto za vyeti. Hatahivyo serikali kwa kutambua kwamba jambo hilo ni inevitable imekuwa ikiweka njia halali na nzuri tu za kutatua changamoto hizo. Nitagusia changamoto ya kupishana au kutofautiana majina au taarifa fulani fulani kwenye vyeti, nyaraka au vitambulisho vya mtu

Tuchukulie mfano vijana au watoto ambao tangu anasoma vyeti vyake vyote anatumia jina fulani. Inaanza mtu anaenda ofisi za NIDA anaulizwa majina na "majina mengine" anataja vizuri. Kimbembe kinakuja siku anatakiwa taarifa za mzazi ambapo ataambiwa aambatishe na NIDA ya mzazi. Unakuta mzazi kwenye NIDA kaweka taarifa tofauti na zile mtoto alizozizoea tangu akiwa shuleni

Hiyo siyo shida kwa sababu watu wengine wana majina mengi ila sasa unakuta watu wa NHIF wanakataa kabisa eti kwa ajili ya kupishana kwa spelling za jina au jina la ukoo au tarehe, mwezi, mwaka nk. Kama mimi mwenye mtegemezi wangu nathibitisha mtu ni huyo na viambata nimeweka nyinyi ni nani mkatae kwamba siyo yeye? Halafu kwenye NIDA kunakuwa na sababu gani ya kuulizwa "majina mengine" sasa kama ni hivyo?

Mzee wa watu kwenye nida kaulizwa majina yake akataja akaulizwa jina maarufu akataja pia lakini kijana wake huku kwenye bima anataka kumchukulia kadi mzee anakataliwa eti hawana uhusiano kwa sababu tu cheti cha kuzaliwa hakijaendana, majina ya baba na yale ya kwenye NIDA ya baba. Huu kwanza ni uonevu lakini pia Kama siye na nimeamua kumuingiza tu si ndiyo vizuri mnichukulie hatua hizo documents zake niulizwe nimezipata wapi huyu mtu, au mimi ndiyo sielewi?

Mtumishi akimsajili mkwe, mwenza, mzazi au mtoto wake je anaweza kuja kusajili wengine tofauti na hao kwa sifa zilezile bila kuondoa hao wa awali? (Yaani mfano leo nimemuingiza mama mzazi jina linaonekana pale kwenye cheti changu cha kuzaliwa na NIDA yake halafu kesho nije na ombi lingine nataka nibadilishe mama mzazi?) Bila shaka jambo hilo ni muhali na hata likitokea kutakuwa na sababu maalumu na taratibu za kisheria zitazingatiwa. Sasa sijui shida inatokea wapi mimi hata nashindwa kuwaelewa wafanyakazi wa NHIF.

Lengo la serikali ni kila mwananchi apate bima ya afya sasa leo mnapokataa baadhi ya maombi ya wategemezi kwa vigezo visivyo na mashiko inakuwa sawa na kuivuta shati serikali katika juhudi hizo maana mkimkatalia ombi mteja wenu maana yake yule mliyemkataa atabaki bila bima. Hivi mtumishi afoji wategemezi kweli? Ili afaidi kitu gani kwa mfano? Yaani mfano afoji baba, mama, mkwe, au mtoto ili iweje? Halafu ombi linapitia kwa afisa utumishi afisa utumishi anapitisha baada ya kujiridhisha kabisa na taarifa za mtumishi halafu NHIF wao iwe ndio wanakujua sana kuliko afisa utumishi, kweli?

Mimi ninaona ukomo wa idadi ya watu na vigezo vimewekwa kwa maana kwahiyo hebu ondoeni ugumu kwenye swala hilo. Haiwezekani kwa namna yoyote kwa vyovyote mtumishi akawaingiza hasara NHIF kwa kuingiza wategemezi wake ilihali ni haki yake kuingiza watu hao. Sana sana mngejikita tu katika vigezo na masharti kwa ujumla jumla na siyo vimakosa vya kawaida ambavyo wala mtumishi hahusiki navyo.

Mfano NIDA ya mzazi kuwa tofauti na cheti cha kuzaliwa cha mtoto mara nyingi utakuta shida ipo kwa mzazi kwani yeye akiwa anajaza taarifa zake alijaza kikawaida tu wala hakuwaza au kuzingatia mambo haya ya kisasa. Sasa kumnyima huduma mtoto eti kwa sababu tu mzazi ametumia jina maarufu kwenye NIDA huku mwanae ametumia jina halisi kwenye cheti hii siyo sawa. Maana yake huyu mtoto akitaka huduma itabidi asafiri kumfuata mzazi wakarekebishe taarifa za mzazi kwanza (kitu ambacho ni kigumu kweli kweli) kisha ndipo arudi kushughulikia mambo yake

Mwisho basi serikali iweke namna ambayo mtu ataweza kuonekana taarifa zake zote kupitia namba ya NIDA ili kuepusha usumbufu. Nikisema taarifa zote namaanisha zote kwelikweli yaani kuanzia vizazi, kazi, elimu, ndoa, makazi nk
 
Back
Top Bottom