NHIF yaja na makali zaidi kwa Watanzania, yaondoa dawa lukuki kwenye orodha ya dawa zinazonufaika na malipo ya bima

NHIF yaja na makali zaidi kwa Watanzania, yaondoa dawa lukuki kwenye orodha ya dawa zinazonufaika na malipo ya bima

Status
Not open for further replies.

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
NHIF imekanusha taarifa hizi: NHIF yakanusha kuondoa dawa 138 kwenye Orodha ya Dawa wanazolipia wateja wake

Makali zaidi, kasi zaidi. Sasa makato yetu yana faida gani? Huu ni unyonyaji wa aina yake.

20200904_130905.jpg
 
Huu ni uthibitisho mwingine haya mashirika yanaenda kufa, nawasikitikia wafanyakazi wanaokatwa pesa zao, serikali inachota pesa kwenye hiyo mifuko halafu hawarudishi kwa wakati.

Sasa haya mashirika yameanza kulemewa na gharama za uendeshaji ndio maana kila siku wanapunguza huduma walizokuwa wanazitoa mwanzo ili kujaribu kuendelea kujiendesha, lakini hili halitasaidia, serikali inahusika moja kwa moja kwenye hili.

CCM haistahili tena kupata kura za mtanzania yeyote mwenye uchungu na nchi hii, au wananchi wanyonge wa nchi yetu, wanastahili kuondoka madarakani sasa, wamefeli, tuwaondoe mapema kabla hawajaharibu zaidi.
 
Huu ni uthibitisho mwingine haya mashirika yanaenda kufa, serikali inachota pesa kwenye hiyo mifuko halafu hawarudishi kwa wakati, sasa haya mashirika ya meanza kulemewa na gharama za uendeshaji ndio maana kila siku wanapunguza huduma walizokuwa wanazitoa mwanzo.
Yani hawa watu wanakata hela nyingi halafu hupati unachokihitaji.
 
Huu ni uthibitisho mwingine haya mashirika yanaenda kufa, serikali inachota pesa kwenye hiyo mifuko halafu hawarudishi kwa wakati, sasa haya mashirika yameanza kulemewa na gharama za uendeshaji ndio maana kila siku wanapunguza huduma walizokuwa wanazitoa mwanzo ili kujaribu kuendelea kujiendesha, lakini hili halitasaidia, serikali inahusika moja kwa moja kwenye hili.

CCM haistahili tena kupata kura za mtanzania yeyote mwenye uchungu wa nchi hii, au wananchi wanyonge wa nchi yetu, wanastahili kuondoka madarakani sasa, wamefeli, tuwaondoe mapema kabla hawajaharibu zaidi
Hali ni mbaya sana kiongozi!
 
NHIF ingejikita kutolea huduma kwenye hospitali za umma.

Juzi kati niliumwa tumbo nikalazwa kwa usiku mmoja kwenye hospitali ya Private hapa Dar (tena kwa kulazimishwa na madaktari).

Bili ilipokuja kesho yake, ilikuwa ni Tsh laki tano.

Niliuhurumia sana mfuko wa bima niliokuwepo. Yani kutundikiwa drip za buku mbili mbili ndio billi ifike huko?

Kingine kinachoimaliza hii mifuko ni kacha ya Watanzania kupenda kuumwa kwa vile wana bima.. Mtu akikohoa kidogo, hospitali. Akiumwa kichwa kidogo, hospitali.. Kwa namna hii mifuko ya bima inalipa pesa nyingi kwenye hizi hospitali hivyo kuishia kudhoofika kiuchumi.

Kingine ni hizi hospitali kufanya kipimo zaidi ya kimoja kwa ugonjwa mmoja ili kuongeza bili... Kwa kweli kwenye matibabu dawa wala hazina gharama kubwa kama vipimo.
 
Wakuu msaada wa menu ya package za Nhif
 
Makali zaidi, kasi zaidi. Sasa makato yetu yana faida gani? Huu ni unyonyaji wa aina yake.
View attachment 1558047

Hahaaaaa!! Naona umestukiwa unaanza kulia mitandaoni!!!! Kwa kifupi 10% imeyeyuka utalia sanaaaa! Ungekuwa mkweli na mzalendo (professional) Ulitakiwa kuonesha dawa za kipaumbele ambazo zimeonekana zinafaa sana kwa mazingira ya Tanzania. Mabadiliko kwenye list ya madawa ipo kisheria!

Shida ufisadi kwenye sekta ya dawa uliosababisha gharama za bima kuwa juu na kuwatesa wananchi sasa kwishney!!! Huwezi kuchagua madawa ya bei ghali yanayofanya kazi sawa na mengine ya bei ya kawaida!! UFISADI UNAOUA NHIF SASA MWISHOOOO!!!

Queen Esther
 
NHIF ingejikita kutolea huduma kwenye hospitali za umma.

Juzi kati niliumwa tumbo nikalazwa kwa usiku mmoja kwenye hospitali ya Private hapa Dar (tena kwa kulazimishwa na madaktari).

Bili ilipokuja kesho yake, ilikuwa ni Tsh laki tano.

Niliuhurumia sana mfuko wa bima niliokuwepo. Yani kutundikiwa drip za buku mbili mbili ndio billi ifike huko?

Kingine kinachoimaliza hii mifuko ni kacha ya Watanzania kupenda kuumwa kwa vile wana bima.. Mtu akikohoa kidogo, hospitali. Akiumwa kichwa kidogo, hospitali.. Kwa namna hii mifuko ya bima inalipa pesa nyingi kwenye hizi hospitali hivyo kuishia kudhoofika kiuchumi.

Kingine ni hizi hospitali kufanya kipimo zaidi ya kimoja kwa ugonjwa mmoja ili kuongeza bili... Kwa kweli kwenye matibabu dawa wala hazina gharama kubwa kama vipimo.
Huu Mfuko unatakiwa kusafishwa! Utapeli na ufisadi ni mkubwa kwa gharama za wanyonge!! Watu wana kamisheni kwenye viwanda fulani au maduka fulani ya watu fulani wanalazimishia dawa wapate kitu kidogo! Huko kwenye baadhi ya private hosp ndio uchochoro wa mafisadi. Mwisho umefika!

Hakuna unachoelewa, kuna dawa muhimu sana hapo kwa afya lakini zimetolewa.
 
NHIF wanafanya mtaji na serikali. Nawahurumia viongozi wake na bodi ya wakurugenzi
 
Hii ni fursa kwetu Sisi tunaodili na mambo ya dawa ni muda wa kupiga hela kwasabb hizo dawa walizoziondoa ni za kawaida sana.

Wale watu waliokuwa wanapata dawa Kwa njia ya BIMA watarudi madukani na demand itakuwa kubwa mtaani.

Asanteni Sana NHIF Kwa kuliona Hilo maana kufa kufaana
 
Huu ni Upumbavu saana. Wapunguze na makato kwenye mishahara
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom