NHIF ingejikita kutolea huduma kwenye hospitali za umma.
Juzi kati niliumwa tumbo nikalazwa kwa usiku mmoja kwenye hospitali ya Private hapa Dar (tena kwa kulazimishwa na madaktari).
Bili ilipokuja kesho yake, ilikuwa ni Tsh laki tano.
Niliuhurumia sana mfuko wa bima niliokuwepo.. Yani kutundikiwa drip za buku mbili mbili ndio billi ifike huko?
Kingine kinachoimaliza hii mifuko ni kacha ya Watanzania kupenda kuumwa kwa vile wana bima.. Mtu akikohoa kidogo, hospitali.... Akiumwa kichwa kidogo, hospitali.. Kwa namna hii mifuko ya bima inalipa pesa nyingi kwenye hizi hospitali hivyo kuishia kudhoofika kiuchumi.
Kingine ni hizi hospitali kufanya kipimo zaidi ya kimoja kwa ugonjwa mmoja ili kuongeza bili... Kwa kweli kwenye matibabu dawa wala hazina gharama kubwa kama vipimo.