Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), unakanusha taarifa zinazosambaa kwenye baadhi
ya mitandao ya kijamii zikielezea kuondolewa kwa baadhi ya dawa katika kitita chahuduma.Taarifa hizi hazina ukweli wowote bali zimelenga kuleta hofu kubwa kwa wanachama na wadau wote wa Mfuko na kudhoofisha kazi kubwa inayofanywa hususan katika maboresho ya huduma za matibabu nchini.Katika kuhakikisha wanachama wa Mfuko wanapata huduma bora, Mfuko kwa sasa unalipia zaidi ya dawa 975 zikiwemo dawa zote ambazo zinadaiwa kuondolewa kwenye kitita cha huduma.Mfuko unazo taratibu zake za kuwasiliana na wanachama, watoa huduma na wadau wake yanapofanyika mabadiliko yoyote ya kihuduma hivyo taarifa zote zinazosambazwa si za ukweli na hivyo zipuuzwe.Mfuko unawahakikishia wadau wake kuwa huduma zitaendelea kutolewa kama kawaida naendapo mwanachama atakutana na changamoto yoyote, asisite kuwasiliana na Mfuko kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja simu bila malipo namba 0800110063.
Imetolewa na Grace Michael
KAIMU MENEJA UHUSIANO
View attachment 1559252