NHIF yasitisha Mkataba na Vituo vya Hospitali ya Aga Khan

NHIF yasitisha Mkataba na Vituo vya Hospitali ya Aga Khan

MDAU TZ

Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
12
Reaction score
53
HUZUNI KUBWA.
---
YAH: TAARIFA KUHUSU KUSITISHA HUDUMA KWA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA VYA AGA KHAN

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu

2. Mfuko husajili vituo vya kutolea huduma za afya kuwawezesha wanufaika wake kupata huduma hizo nchi nzima. Hadi sasa Mfuko umesajili jumla ya vituo 9,920 vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi ngazi ya Hospitali ya Taifa ya Rufaa kwa umiliki wa Serikali, Binafsi na Madhehebu ya Dini.

3. Miongoni mwa vituo ambavyo Mfuko umesajili vinamilikiwa na Taasisi ya Aga Khan vinavyojumuisha Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam na Kliniki zilizoko katika maeneo mbalimbali nchini. Hivi karibuni, Mfuko umepokea taarifa kutoka Taasisi ya Aga Khan kuwa imekusudia kutokuendelea na mkataba kati yake na Mfuko kwa vituo 11 kati ya 24 nchini ikiwemo hospitali ya Aga Khan Dar es salaam kwa sababu ya changamoto za kiuendeshaji.

4. Wakati majadiliano na mtoa huduma yakiendelea na kuepusha usumbufu kwa wanachama wake, Mfuko unatoa taarifa kuwa, kuanzia tarehe 14 Agosti 2024 utasitisha huduma katika vituo vya Aga Khan nchini. Katika kuhakikisha mwendelezo wa huduma kwa wanufaika wake hususan waliokuwa wanapata huduma katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam Mfuko umefanya makubaliano na kituo hicho ambapo:-

. Wajawazito wanaohudhuria kliniki katika hospitali ya Aga Khan ambao wametimiza majuma 35 wataendelea kupata huduma katika hospitali hiyo hadi watakapojifungua na kuruhusiwa. Kuhusu wajawazito ambao hawajatimiza majuma 35 wanashauriwa kutumia vituo mbadala vilivyosajiliwa na Mfuko ambapo pia baadhi ya madaktari katika vituo hivyo walikuwa wanawahudumia wakiwa Aga Khan;

Wagonjwa watakaokuwa wamelazwa kufikia tarehe 13 Agosti 2024 wataendelea kupata huduma katika hospitali ya Aga Khan hadi watakapopata nafuu na kuruhusiwa;

. Wagonjwa wengine wote wakiwemo wa kliniki za saratani na kusafisha damu (dialysis) watapata huduma katika vituo vingine vilivyosajiliwa na Mfuko. Tayari Mfuko umewasiliana na wagonjwa wa kliniki ya kusafisha damu na kuwahamishia kupata huduma hiyo katika vituo vilivyopendekezwa kwao;

5. Aidha, Mfuko umesajili vituo vingine vyenye hadhi sawa au zaidi ya hospitali Aga Khan Dar es Salaam ambavyo ni Saifee Hospital na Shifaa Pan African Hospital vyote vilivyo jijini Dar es Salaam. Vilevile wanachama pamoja na wategemezi wao wanaweza kupata huduma za haraka katika vituo vingine vikiwemo vituo vikubwa kama Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI). Kwa mikoa mingine, Mfuko umehakikisha kuna vituo vilivyosajiliwa katika maeneo jirani kumhakikishia mwanachama huduma bila usumbufu.

6. Hivyo kwa barua hii, Mfuko unawaomba kuwataarifu wafanyakazi kutumia vituo mbadala kwa ajili ya kupata huduma za matibabu kuanzia tarehe 14 Agosti 2024. Maofisa wa Mfuko katika kitengo cha wateja wakubwa pamoja na ofisi zake nchi nzima wako tayari kutoa usaidizi kwa wanachama kuhakikisha wanapata huduma kikamilifu bila usumbufu katika kipindi cha mpito.

7. Tunakushukuru kwa ushirikiano wako


IMG_4386.jpeg

IMG_4387.jpeg
===

nhif.jpg
 

Attachments

Duh Aghakan wanahuduma nzuri sana... Ni matumaini yetu hili litakua la mda mfupi
 
SAFI SANA AGA KHAN.

ni vyema vituo vingine vikubwa vifuate mkumbo wa aga khan ,ili kuleta shinikizo la manufaa ya wanufaika wa mfuko..

kwa kujitoa aga khan sasa mjadala uhamie.
1. gharama za vifurushi
2. bima ya afya toto
 
Mambo ni magumu sana..
Aga Khan lazima ajihami otherwise...yatamkuta ya wengine.
Sekta ya afya imekufa kifo cha mende..
Labda ipigwe u-turn
 
Hatari sana hii ,NHIF iache kucheza na pesa zetu ,waweke mikakati ya kufanya kazi na watoa huduma za Afya Kwa urafiki sio huu ubabe waliouanzisha,watatumaliza hawa NHIF,tunataka kurudi kwenye enzi za kuishi Kwa neema ya Mungu badala ya kuimarisha huduma za afya.

Poor NHIF,najutia mchango wangu kwao
 
Tatizo nao NHIF kwenye malipo wanamambo visababu vingi , ila me niliwahi tibiwa Aga khan wanahuduma nzuri
 
Hapo aghkan ndio hela ya nhif ilikuwa inapotea haya tuwaone hao wanao enda kulipa cash kipimo cha malaria milion 1
 
Aga Khan mtatoa huduma hamtoi? SUBIRI Mkurugenzi wenu atekwe Kama MO....
SERIKALI HUWA HAIKOSEI.

MITANO TENA.
 
Dah aghakan wako gud Sana..nhif chonde chonde kaen mezan
 
Hapo aghkan ndio hela ya nhif ilikuwa inapotea haya tuwaone hao wanao enda kulipa cash kipimo cha malaria milion 1
Unaongea tu sababu hujui. Hospital yoyote inayotoa huduma bora zaidi gharama zinakuwa kubwa. Na ni uongo ulio tukuka kuwa kipimo cha malaria ni mil 1
Hela ya NHIF nyingi ilikuwa inapotea gov hospital
Na watu wataendelea kwenda aga khan
 
NHIF uhuni mwingi
Na hapo agakhan kwa kulipa cash
Si mchezo lazima uumie

Ova
 
Duh.......waziri husika anaruka singeli majukwaai huku afya za watu zikipewa kisogo sio watoto wala watu wazima mfuko wa afya uko taabani halafu hakuna jitihada za kuuweka sawa.
 
Back
Top Bottom