NHIF yasitisha Mkataba na Vituo vya Hospitali ya Aga Khan

NHIF yasitisha Mkataba na Vituo vya Hospitali ya Aga Khan

Hii Tanzania ipo siku Mungu atatuokoa kupitia mikononi ya Hawa wararushwa
Hatuna budi kuanza jitihada za kujiokoa wenyewe tukisubiria mkono wa muweza wa yote haiwezekani magari ya kifahari yakawa kipaumbele kuliko afya za wananchi wako huo ni wendawazimu unaopaswa kupigiwa kelele na kila mwananchi
 
Aga Khan ukiwa na NHIF KWA KUFUPI HUTUBIWI BIMA WAMESHAJITOA MPAKA UTO HELA CASH SIYO KADI YA BIMA
Ajabu sana harafu waziri wa afya anacheza singeli majukwaani wakati wizara yake ameshindwa kuisimamia afya za wananchi mashakani
 
Maji yamezidi unga na moto umekata!
Hapa watakaoumia ni hawa;
1. Viongozi wakubwa/waandamizi wa serikali
2. Wabunge
3. Ndugu wa karibu wa viongozi wa serikali na wabunge.
Kweli kabisa Aga Khan ni hospital ambayo Iko Kwenye Joint commission international accreditation,hata muhimbili na JCI Hawana JCI, anaifututia bima maana yake hujaikomesha ila umepumzisha na upuuzi wako uliza mmarekani yoyote akitaka kutibiwa,ulaya nzima ni mpaka hospitali yenye acredation ya JCI
 
Hili Swala Rais hajapata washauri wazuri nchi Iko vibaya kifedha, siyo aga Khan tu tunakoelekea HUDUMA ya afya inaenda kuwa mbovu
 
Eti Saifee...hii hii inayo inflate gharama za matibabu?

NHIF inaruhusu member wake akajifungulie(c-section)pale Saifee kwa sh 4,000,000 nje ya gharama za clinic ilhali Amana haifiki sh 500,000?

Wako busy kuongeza mishahara ya wabunge kwa 45.5% ingawa bado ni kada inayolipwa ghali zaidi kwa ujumla, raisi mwenye mshahara wa pengine sh 35m anayenunua saa ya sh 118m kama walivyosema wanamtandao.

Nchi inayopima maendeleo yake kwa kuangalia namba E kwa mujibu wa mchumi mbobevu na waziri wa shilingi.

60+ years na bado Malaria ni tatizo, kipindupindu ugonjwa unaosemwa kuwa unapata kwa kula kinyesi.

Nchi inayotenga zaidi ya sh 870bn kununua magari huku ina mashine 15 tu za MRI? Mashine moja ya MRI ni sawa na VXR moja, tunazo ngapi hizo VXR, tena za 2023?

Wazee walishafeli, watu wa makamo kadhalika, vijana ndo hao machawa na wakinondoni, JENI ZII vipi?
 
Taasisi ya Aga Khan imesitisha mkataba kati yake na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa vituo vyake 11 kati ya 24 nchini ikiwemo hospitali ya Aga Khan Dar es salaam kwa sababu ya changamoto za kiuendeshaji.

Taarifa ya mfuko wa Bima ya Afya imeeleza kuwa kuanzia tarehe 14 Agosti 2024 mfuko utasitisha huduma katika vituo vya Aga Khan nchini.

Aidha katika kuhakikisha mwendelezo wa huduma kwa wanufaika wake hususan waliokuwa wanapata huduma katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam Mfuko umefanya makubaliano na kituo hicho ambapo:-

“Wajawazito wanaohudhuria kliniki katika hospitali ya Aga Khan ambao wametimiza majuma 35 wataendelea kupata huduma katika hospitali hiyo hadi watakapojifungua na kuruhusiwa.”

“Kuhusu wajawazito ambao hawajatimiza majuma 35 wanashauriwa kutumia vituo mbadala vilivyosajiliwa na Mfuko ambapo pia baadhi ya madaktari katika vituo hivyo walikuwa wanawahudumia wakiwa Aga Khan”

“Wagonjwa watakaokuwa wamelazwa kufikia tarehe 13 Agosti 2024 wataendelea kupata huduma katika hospitali
 
Hii bima makampuni mengi yanailalamikia kwenye kuchelewesha malipo ni vile tu wananazimishwa na silikale.
 
Agakhan wamepiga kwenye mshono
Lazima mfuko uombe maji!
😀 😀 local hospital ndio za kuetetemeka. kwa hao jamaa mfuko unakuwa chawa tu.
 
Back
Top Bottom