Wanajeshi hata kama hauna kosa unatengenezewa kosa. Nilitumwa jeshini kikazi nimeulamba na mchuchumio juu.kufika getini nikaruhusiwa nikakaa pale mapokezi.
Kweli walinichangamkia si unajua wanaume kila mtu anataka no.mmh.
Nikawaambia nilichokifata kweli walikuwa wakijua hiyo issue ila walikuwa wakikwepa nisikutane na hao watu ambao ni wafanyakazi humo ndani ila sio wanajeshi.
Tatizo wakati naenda nikasahau kitambulisho, yesuuuuuu, hili ndo kosa kubwa nilifanya. Nikapelekwa kwa mkubwa wao.
Swali la kwanza wewe ni raia au ni mpelelezi? Nikasema mimi ni raia, unatoka wapi? Nikajibu, akasena watu wa hiyo wilaya sio raia, nikawapa kitambulisho cha nida akasema hicho kinatafutwa huko kwenu hakunaga raia.
Hapa nikawaza nimpigie boss wangu maana nilienda pale kikazi na ni ilikuwa ni amri so kikawaza nimpigie.
Nikapelekwa ofisi nyingine nilihojiwa kuanzia babu na mabibi nisio wajua.
Documents nilizopeleka pale zinaonesha ninakotoka na niko sahihi kuwa pale tatizo sina kitambulisho.
Nilizungushwa ofisi zote, mara mvua ikanyesha mjeshi mmoja akasema huyu avue viatu abilingishwe hadi getini, kwanza sio raia anatoka wilaya ovyo kabisa. Sio raia wale[emoji23][emoji23][emoji23]
Mjeshi mwingine kasema mwacheni tu aje huku tumkague kama ni raia.
Nikapekekwa kwenye kachumba na mjeshi wa kike nikavua shati aangalie kama nina ndui ile chanjo iliachaga kovu, basi akaikuta, nikarudishwa ofisini, nikataka kumpigia boss wangu hawataki maana walijua ntapata msaada fasta .
Jioni sana nikaruhusiwa kuondoka ila wakaweka ngumu nisikutane na wale watu ingawa niliwaona, nikaondoka zangu.
Nyie watu jeshini sio sehemu salama.yaani huwezi kwenda kule ukakosa kosa lolote lazima wakutengenezee kosa ilimradi tu wakunyooshe akili ikukae sawa.
Niliwaza sana hizi movie tunazoziona mtu anajitosa kuingia jeshini anakuwa hajipendi.
Sidhani katika hali ya kawaida kama kuna kaka jambazi ambae alishawahi ingia jeshini akatoka salama maana wako makini sana.