Ni afadhali mwanaume kuwa na Ghubu kuliko mwanamke….!

Ni afadhali mwanaume kuwa na Ghubu kuliko mwanamke….!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Mtaalamu mmoja wa mahusiano na malezi, Dk. Grace Katterman, katika kitabu chake maarufu kinachoelezea athari za Ghubu kiitwacho, Verbal Abuse, anaelezea uharibifu wa tabia unaoweza kusababishwa na ghubu kwa mtoto.

Anaeleza kwamba Mwanamke anapokuwa na ghubu watoto huathirika zaidi kuliko ghubu hilo anapokuwa nalo mwanaume. Anaonya kwamba mwanamke anapokuwa na ghubu huweza kuwafanya watoto kuwa na tabia zisizopendeza watakapokuja kuwa wakubwa.....................
 
Ila hata mwanaume mwenye ghubu lol! ni kero kwa mkewe/mpenzi, usiombe ukakutana na mwanaume mwenye ghubu, utajuta!
 
Ila hata mwanaume mwenye ghubu lol! ni kero kwa mkewe/mpenzi, usiombe ukakutana na mwanaume mwenye ghubu, utajuta!
Kwa taarifa yako, Ghubu la mwanaume ndio linadumisha ndoa......................
 
...............ndiyo...................pasuka mkuu

Ndio maana yake.................... Ghubu la mwanaume ndio mahaba yenyewe yanayoleta chachu katika mapenzi...!
 
gubu ni nini jamani hebu tufafanulie vizuri jamani

Afadhali na wewe umeuliza maana watu wana arrogance ya ajabu sana humu. Swali limeulizwa kwa nia njema lakini hakuna hata aliyejibu - wanaliruka tu.

Ukiona hivyo ujue huenda na wao hata hawajui.....
 
Tuambieni basi jamani, hilo ghubu ni nini? mtoa mada tufafanulie basi
 
...gubu ni maana yake ni kutofurahia mapenzi..,yani mwanamke ambaye hajawah fika kilele tangu azaliwe na mwanamume ambaye ni impotent..
 
Mama ndio mlezi zaidi kuliko baba, any bad attitude of this woman will have major impact on the family. Mama ndie anayejenga na kuharibu jamii. All I want to say is tafuteni wanawake wenye maadili mema na bora matukio mtayaona kwenye watoto wenu.

I think Ghubu is destoyer of happy family
 
Ghubu ni nini?
 
Ghubu ni nini?
GHUBU maana yake ni tabia ya mtu kutoridhika na mlalamishi (kunung'unika kusiko isha)............hata akosewe jambo dogo tu kwake litakuwa kubwa au..........................Asipolalamikia hili, atalalamikia lile..................... ilimradi keroooo kerooooo keroooo zisizoisha.
 
Asante kwa kujibu.

Sielewi kwa nini ilikuwa shida kwa watu kujibu kama walikuwa wanajua maana yake. Shukrani tena.
 
Back
Top Bottom