Mtambuzi ni kheli mwanamke mwenye gubu, kuliko mwanaume. Husiombe ukutane na mwanaume mwenye gubu kha!!! utajuta, maana baadhi ya wanawake ni kawaida sana kulalamika, gubu na ulalamishi vinaendana. Mwanaume anayelalamika, lalamika ni kero haswa, ebu fikiria upo nyumbani na marafiki zako wewe mwanamke mume wako anatoka kazini/kwenye mihangaiko yake anakuta labda umembadilisha mtoto pampers, akaikuta hapo chini, haukuwa umeiacha makusudi labda ndo tu umetoka kuitoa, ile kuiona tu anaanza, we mwanamke haya makitu ya mtoto unayaacha, acha hapa kwa sababu gani? Au dada kwa nini huwa mnakuwa wachafu hivi mna acha, acha vitu hovyo, lakini kwa mwanamke kuulizia kwa nini hiyo kitu ipo hapo chini ni sawa kabisa kwa maana ni jukumu la mwanamke kuangalia usafi wa nyumbani japo itakuwa ni gubu ila itaonekana tu kwamba ni moja ya majukumu, nimetoa mfano huu sababu mtu mwenye gubu huwa hachagui kitu cha kuongea, na ni wakati gani wa kuongea, kila kitu yeye kwake ni kibaya yaani ni kero tu, afadhali mwanamke awe na gubu maana bwana anaweza kumbadilisha si unajua wanawake huwa ni wepesi wa kutii, ila baba akiwa na gubu, mama yangu!!! Si ndo mama na watoto wakimwona tu kila mtu anatafuta mahali pa kutokea ili hasikumbane na dhahama za jamaa.