Ni agizo la TCU au Chuo kinatuibia?

Ni agizo la TCU au Chuo kinatuibia?

Mjamaajr

Senior Member
Joined
Nov 13, 2013
Posts
110
Reaction score
80
Waungwana.
Kuna mgogoro unaendelea hapa Chuoni kwetu (UoA) kuhusu Assuarance Fees toka kwa TCU.

Chuo kinataka kila mwanachuo alipe 20000/=Tshs kama agizo toka TCU lakini baadhi ya vyuo vimelipa bila wanachuo kuhusishwa sasa tunauliza hizo pesa ni za nini!? na wanachuo zinatuhusu nini!? Hayo ndio maswali makubwa lakini tena kwanini tulipe tena kwa kutumia Account ya Chuo!? Naomba mnisaidie mwenye taharifa sahihi.

Nawasilisha
 
Ni kweli ikusanywe kwa wanafunzi au !?
Mbona vyuo vingine km St Joseph Dom, Saut Mwanza hawajatoa kwanini.
 
We St Joseph tumetoa wotee inawekwa kwenye akaunti ya chuo then inatumwa
 
We St Joseph tumetoa wotee inawekwa kwenye akaunti ya chuo then inatumwa

Mmehoji hiyo ni ya nini mbaka ikusanywe kwa wanafunzi...
Na je wale wasiopitia TCU kupata chuo wanahusikaje hapo.
 
Hiyo wanaita Quality Assurance Fee ambayo inalipwa kwa TCU na wanafunzi kuanzia level ya cheti (certificate) hadi shahada ya uzamivu (PhD) kote nchini. Maelezo ya TCU juu ya malipo hayo bado ni utata hadi leo zaidi wanawatishia wakuu wa vyuo kua vyuo vyao visipolipa watakiona cha mtema kuni. Imeumiza watu wengi sana hiyo pesa especially ambao hawahusiki na TCU moja kwa moja. Vyuo vinakusanya na kuzituma TCU na kwa vyuo ambavyo wanafunzi wao hawajalipishwa direct, kuna baadhi wanaongezewa kwenye malipo ya ada so utailipa kama ada, wengine wanaongezewa kwenye michango mingine ya chuo so utailipa huko ukilipia michango mbalimbali ya chuo lakini sharti ni kila mwanafunzi anaesoma nchini Tanzania lazima alipe hyo elfu 20. PERIOD
 
Back
Top Bottom