Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Hii nchi viongozi wetu wa serikali wanazani maendeleo ni ujenzi wa vitu vingine tu km SGR na Majengo marefu tu.Maisha ni pamoja burudani hasa mpira wa miguu ambao ndio kipenzi kikubwa cha WTZ. Bila kupoteza mda, jamani hv kufunga taa viwanjani nayo tunahitaji msaada kutoka benki ya dunia?Yaani mikoa mikubwa km Mbeya,Arusha na Mwanza kunakosekana uwanja wenye taaa? This is a huge shame. Mfano leo Yanga na Azam wanacheza mashindano ya kimataifa mechi zetu za ligi zingeweza kuzogezwa kuchezwa usiku ili mashabiki waweze kutazama mechi za Yanga na Azamu,na baadae waende kutazama mechi za ligi kuu. Lakini kwa kukosa miundo mbinu ya taa inabidi mechi zote zichezwe mechi kwa wakati mmoja. Matokeo yake ni viwanja kukosa mashabiki kwani wanaishia kutazama mechi Yanga au Simba. WTZ tunapenda sn mpira na michezo mingine ila viongozi wetu kuna sehemu mnatukosea . Najua mkiamua mnaweza kutuondolea hii aibu.