Ni aibu gani au kituko gani ulikifanya siku ya kwanza ulipoajiriwa?

Isenye

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2024
Posts
1,985
Reaction score
5,167
Haya maisha bana,sometimes hayana nidhamu.

Baada ya kufulia mtaani muda mrefu nimepiga mishe za saidia fundi sana mtaani nikawa nishajikatia zangu tamaa ya kuajiriwa.

Kuna siku nikapigiwa simu na wahindi flani nilifanya nao interview miezi kadhaa nyuma,walinipigia kunitaarifu week inayofuata niende ofisini kwao kuanza kazi.

Basi ilikua siku ya jtatu nimewahi kufika ofisini kwao,basi baada ya utambulisho nikakabidhiwa kwa demu flani wa kihindi ili anipige training,yule demu sijajua alikua mchoyo au hakunipenda tu,yani alikua anakula mazaga hata hanikaribishi.

Mimi wakati huo mfukoni nina ka elfu 2 tu ka kuzugia.

Sasa kituko muda wa lunch ulivyofika wenzangu wanafungua lunch box zao na wengine wanaenda mtaani kupiga msosi,mimi nikaenda zangu nje chini ya mti,nikanunua muwa wa jero nikawa naupiga mdomdo..mpaka muda wa lunch ulivyoisha nikarudi kuendelea na training,yule muhindi akaniuliza "have you taken lunch? Nikamjibu yes kumbe nilikua na ubao sio wa nchi hii.

Je ni kituko gani nawe mwana jf umewahi kukifanya siku ya kwanza kuajiriwa?
 
Aisee hii Habari yako inasikitisha na kufurahisha.
 
Nilianza kazi wakati mtoto wangu bado ananyonya ingawa alikuwa ana mwaka mmoja, toka amezaliwa sikuwahi kukaa nae mbali hata kwa saa moja tuu. Hiyo siku ilikuwa ndefu sana kwangu muda wote naangalia saa ifike nikuwahi mtoto.

Nilikuwa nikifikiria nimemuacha analia asubuhi ( day care) basi nakosa raha ilipofika muda wa kutoka kazini nilikimbia mbio mpaka boss na wafanyakazi wenzangu wakabaki wanacheka, nikakodi bodaboda ili niwahi kufika alipo nilihisi daladala nitachelewa.

Baada ya kuzoea ndio kwanza nikawa nikitoka kazini napitia na misele kwanza.
 
Siku ya kwanza kabisa nilipokelewa mapokezi na reception wa Kampuni,

Katika maongezi akaniuliza; ''Utakunywa chai au soda?''

Nikamjibu kua; ''Nitakunywa soda wakati nasubiri chai ichemke''
 
Nilisaini kwenye Daftari mda exactly kumbe nilitakiwa kurudisha nyuma mfano kama umefika saa 08:03 wa mwisho mwenzio kasaini saa 07:28 sasa mimi nilitakiwa kusain saa 07:29 hata kama nimefika saa 08:03 so wakongwe walini mind sana siku hiyo. Ndo mpaka leo sijawahi rudia
 
Back
Top Bottom