Mpingamkoloni
Member
- Feb 14, 2021
- 13
- 33
Asubuhi hii niko Idodomya. Nilitumwa na daktari wa Hospitali ya rufaa Mbeya kuja kufanya MRI. Alinipa chaguo la kufika Dodoma au Dar es Salaam. Idodomya ni jirani sana kwangu. Ni mwendo wa masaa matatu.
Kinachonihuzunisha sana ni hiki, hivi inakuwaje Hospitali kubwa kama ya Rufaa Mbeya yenye madaktari bingwa kama mia, ikose MRI? Ikose PET scan? Nasikia ndio hospitali kubwa zaidi iliyopo chini ya Wizara ya Afya ambao bado haijaanza kujitegemea.
Naambiwa bei ya MRI na PET vyote havizidi bilioni kumi, na hapo umenunua zile bora zaidi kwenye soko. Na kifaa kinategemea kutumika zaidi ya miaka 10.
Halafu nasikia pia hospitali ya Rufaa Mbeya wana CT Scan moja tu, yaani ikigoma basi hamna kitu tena. Tunazungumzia luku kukosa backup, wakati kwenye afya tunanunua kifaa kimoja kimoja.
Hivi huwa twashindwa nini kujaza vifaa na utaalam kwenye hizi hospitali kubwa za kitaifa? Hivi malengo yetu ni yapi kwanza? Tukumbuke sasa India hakuendeki.