Ni aibu kubwa kwa wana Arusha kuwekewa kiingilio kama hiki

Wakitaka uwanja ujae waseme Lema ndo mgeni rasmi, otherwise ni shida.
 
Buku kubwa sana chalii yangu, mechi peleka uwanja mikoa mingine huko!!!!..
 
TFF wamekosa ubunifu wangesema kuwa Kiingilio ni Tsh 20,000 jukwaa la kawaida ila ganja na mkojo wa shetani vinaruhusiwa humo ndani watu wangejaa sana... arusha kuna wajukuu wa bob wengi sana...
 
Hapo hukuna timu ya Simba Wala Yanga. Kukosekana moja ya timu hizo fainali wana wasiwasi watu hawatakuja kuangalia mpria wakiweka kiingilio kikubwa. Hata hiyo fainali ingechezwa Dar au Mwanza kiingilio kingekuwa hicho
 
aiseee hii ni ayubu(in panjuan voice) kwa mabillionaire wa Arusha aiseee
Wale majamaa uwawekee kiingilio bure wanaweza wasifike hata 100. Afu sasa timu zenyewe zinazocheza wala hazina umaarufu kiviiile.
 
Uku watu Wako bize na Kaz halafu raia Weng s watu wa soccer pia timu zenyewe n ndogo
 
Ni sawa kwa mji wa Arusha kwakuwa huko wachache wanapesa nyingi wamewekewa kiingilio cha juu, na wengi hawana pesa za kukidhi mahitaji yao ya kila siku, ndio maana wamewekewa kiingilia cha Elfu moja.
Ni sawa kwa mji wa Arusha wanataka kila mpenda michezo aione hiyo mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa.
 
Ukweli uliowazi ni kwamba arusha michezo huwa inaonekana kama utani/uzembe na kufanywa na watu wavivu. Ni ngumu kwa mfano kwa wale wazee wa kimeru kusikia wakizu gumza habari za mpira. Timu nyini zilianzishwa arusha ila zikafa kwa kukosa support hasa ya mashabiki.
Kipimo kizuri cha hili ni mezi za simba na yanga ambapo popote wanakokwenda hujaza uwanja ila kwa arusha ni tofauti kabisa.

Arusha kwa mpira ni shida inayojitegemea, kuja ya kufanya hamasa kubwa!
 
Arusha unaweza kufanya kiingilio bure na wasifike watu 100.
Babu acha fiksi.. Sema tu team zenyewe za kiwaki ndio maana. Ingekuwa Simba na Yanga tungeenda. Hiyo tenga kumi kuliko nikaangalie mechi ya kuduanzi kama hiyo bora ninunue bombadier langu na pull zangu mbili nilipuke maghetoni
 
Unamaradhi wewe kapimwe. Arusha unaisikia tu wala huijui. Tembea uone. Yani Arusha hata wale machokoraa watoto wa dampo hawakosi tenga dala kwa siku sembuse watu wanaojielewa? Acha upuuzi mkuu
 
Babu acha fiksi.. Sema tu team zenyewe za kiwaki ndio maana. Ingekuwa Simba na Yanga tungeenda. Hiyo tenga kumi kuliko nikaangalie mechi ya kuduanzi kama hiyo bora ninunue bombadier langu na pull zangu mbili nilipuke maghetoni
Ndo maana nikamalizia kwa kusema timu zemyewe hizo hata wakisema kiingilio bure bado watu hawataenda.
 
Wanajua hali ya maisha ya watu wa mikoani...ingekuwa inafanyika Mara huko kiingilio ingekuwa bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…