Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nimekuwa nikijiuliza, hivi kama Taifa tunakwamia wapi?
Hivi Tanzania ya leo, ndiyo ihangaike kuwatafutia wananchi wake umeme na maji, baada ya kujitawala toka kwa mkoloni miaka 60 iliyopita?
Nchi iliyojaa rasilimali tele, kama vile mito inayotiririka maji mwaka mzima, maziwa matatu makubwa yanayoizunguka nchi.
Nchi ambayo ina gesi ya kumwaga zaidi ya ujazo wa 57trililioni cubic meters, ambayo ingetuwezesha kuwa na umeme wa uhakika, kwa Maisha yetu yote!
Na umeme mwingine tuwauzie majirani zetu ambao hawajajaliwa na Mungu kuwa na nishati hiyo ya gesi kama tuliyo nayo sisi!
Hivi tunakwama wapi, wakati kuna nchi, ambazo zipo maeneo ya majangwa yakipata maji bila Shida katika kipindi chote cha Maisha yao??
Tunakwama wapi, wakati kuna nchi ambazo hazina rasilimali ya nishati ya gesi, kama tuliyo nayo sisi, zikiwa na umeme wa uhakika kipindi chote bila kujali Hali ya hewa ya ukame??
Tuseme sisi tumepata laana toka kwa Mungu kuwa Katika Hali hii??
Nimetafakari yote hayo kwa uchungu mkubwa na kugundua kuwa nchi yetu ina tatizo kubwa la uongozi wa kudumu uliopo wa CCM
Hivi inawezekanaje kutokana na ukame tulio nao, anaibuka kiongozi mkubwa wa mamlaka za maji, anasema kuwa, mgawo wa maji utapungua, kama siyo kwisha kabisa, kwa kuwa tayari wameshawadhibiti wale waliokuwa wanamwagilia mashamba yao, na hivyo tayari mto wa Ruvu umejaa maji?!
Ukweli lazima usemwe, nchi yetu bila kupata Katiba mpya ya nchi, hatutoboi!
Tutaendelea kuhangaika na "petty issues" kwa Maisha yetu yote!