Ni aibu kuwa na kiongozi kama Ntobi

Vincenzo Jr

Platinum Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
24,262
Reaction score
58,728
Kibaya zaidi ndio vijana anaowaamini mwenyekiti, hivi Mbowe huyu Ntobi huoni kama anakuharibia hata hizo sifa chache ulizobakiza?

Sasa hivi chama kina watu walioamua kufanya “upinzani” bargaining chip

Tukapigania chama kwa juhudi kubwa . Tukapigwa , tukaumizwa , wenzetu wakafungwa wengine wakapotezwa na hata wengine kuuawa halafu ghafla tu tunapewa jibu la ovyo na Ntobi.

Ashukuliwe mhe. Lissu kwa kutufumbua macho, genge la kina Ntobi, Boniyai na vibaka wengine limejulikana!!
 
Aya ni mambo ya uchaguzi tu japo sio afya ,uchaguzi ukiisha watu wataombana msamaha na mambo yakaa sawa
 
Hayo ni maoni yake nanyi toeni yenu jaribuni kuheshimu mawazo ya watu!
Kutukana na kuongea uwongo, siyo sehemu ya maoni.

Ntobi ni mwongo na mnafiki. Amekidhalilisha chama kwa kusema kuwa mwaka 2020, katika kumpata mtu wa kukiwakilisha chama kwenye nafasi ya Urais, kilimtafuta mtu mwenye uwezo wa kuropoka. Je, hiyo ni kweli? Yaani unaamini kuwa sifa pekee iliyokuwa inatafutwa kwa mtu wa kugombea nafasi ya Urais mwaka 2020 kupitia CHADEMA, ilikuwa ni uropokaji? Mbona huyu anaonekana kuwa ndiye mropokaji?

Chama kichukue hatua dhidi yake, kwa kauli ya kukidhalilisha mbele ya umma.
 
Hiki chama ni shida imagine hadi wanawake ni vibaka kama wale waliochoma nguo mchana kweupe🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Kwani watu walipokuwa wanasema viroba vifungiwe ulikuwa hukuelewa huyo ntobi wala hajaongopa yupo sahihi hiyo ndio Chadema wote ipo hivyo ,Mzee Juma Duni alikuwa sahihi kabisa maneno yake!
 
Huyo Ntobi ataweka wapi uso wake endapo yule asiyemtaka akiwa ndiye kiongozi wake....
 
kwani chama chenu hakina uhuru wa maoni? huo ni uhuru wa kuongea choxhote katika chama cha democrasia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…