Ni aibu kwa mashindano ya taifa ya riadha kufanyikia kwenye kiwanja kisicho na running tracks zenye hadhi ya olimpiki

Ni aibu kwa mashindano ya taifa ya riadha kufanyikia kwenye kiwanja kisicho na running tracks zenye hadhi ya olimpiki

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
INASIKITISHA SANA. Mimi kama mdau wa riadha ninasikitishwa na mashindano ya taifa ya riadha kufanyikia kwenye uwanja wenye njia za kukimbilia za vumbi badala ya tartan kama za uwanja wa taifa. Kwa ambao hamfahamu ni kuwa leo 03/07/2026 mashindano ya taifa ya riadha yameanza huko Kibaha, Filbert Bayi School.

Wakati wanariadha wa Ethiopia kina Kenenisa Bekele wana viwanja binafsi vya mazoezi vyenye hadhi ya olimpiki sisi tunafanyia mashindano makubwa ya kitaifa kwenye running tracks za vumbi. Inatia hasira balaa. Halafu ninavyojua mashindano ya taifa kwa nchi nyingi huwa yanatumika kama sehemu ya kupata wanariadha wa kuwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa. Huko Kenya, Ethiopia, USA, Jamaica hata SA huwa ni tukio kubwa mno wanariadha hawalali. Ni hekaheka ili kuweza kuingia kwenye timu ya taifa. Ila hapa kwetu ni huzuni tupu. Haya mashindano yako kama ya UMISETTA.

Ninawasihi chama cha riadha, TOC, BMT na serikali kwa ujumla kuangalia jinsi gani wanaweza kutenga pesa na kuviwekea viwanja tartan tracks ili kuondoa hii aibu. Ninajua serikali haiwezi kosa bilioni 5 ikaweka running tracks viwanja kadhaa. Pia chama changu CCM kama mmiliki wa viwanja vingi nchini itafute hata wawekezaji wa kuweka running tracks za kisasa viwanjani. Waanze na Sheikh Amri Abeid Stadium kwa sababu ndo kiwanja kinachotumika zaidi na wanariadha.

735038050_18329491018284551_2095222580971559484_n.jpg
731541147_18329491027284551_6313125661999896119_n.jpg
731754310_18329491036284551_1230203766029673510_n.jpg
images.jpg
images (1).jpg
 
Pia chama changu CCM kama mmiliki wa viwanja vingi nchini itafute hata wawekezaji wa kuweka running tracks za kisasa viwanjani. Waanze na Sheikh Amri Abeid Stadium kwa sababu ndo kiwanja kinachotumika zaidi na wanariadha.
Ccm hivyo viwanja mlivyopora Kuna siku mtapokonywa tu.
 
Back
Top Bottom