KERO Ni aibu Mji kama Mkata - Handeni unaokua kwa kasi kukosa maji ya uhakika

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ni nyama,
Sema jamaa hawajapapatia tu.
Unakuta nyama yenyewe hata chumvi hawaweki Yani ilimradi tu.
Ni eneo zuri la kimkakati lipo njiani accessible lakini hawajapapatia kikazi.

Sehemu yenye uchawi na ushirikina kuendelea huwa si lelemama.
Pako hovyo hovyo tu ila ndio hivyo nyama iko vizuri.
 


Na lile daraja kati ya kwamkono na komdudu lijengwe jamani tafadhali maana ni mateso kwa wananchi.
Njia ya kutoka Kwamkono kwenda Mzundu hadi kabuku iwekwe rami au kuchongwa vizuri ipitike hata nyakati za mvua.

Lile daraja la muda kile kitu kilichowekwa pale kinatisha, linanesanesa ni hatari kupita halifai kwa matumizi ya binadamu.

Kwa hiyo magari kupita njia ile imebaki historia ?
Mbona tunarudi nyuma badaΕ‚a ya kwenda mbele ?
 
Aisee hupajui Mkata. Kuna jamaa upande mmoja anachoma kuku wa kienyeji balaa. Upande wa pili Kuna mtaalam wa maini.

Mimi sijawahi kufurahia nyama pale Sijui ni timing?

Ngoja siku niende kwa muda wa kutosha niagize nikiwa sina haraka nione kama nitapata kitu roho inapenda.
 
Mbunge wa Hapo ni wa chama gani na DED ana kazi gani?
 
Mbunge wa Hapo ni wa chama gani na DED ana kazi gani?


Kote ni CCM tangu Uhuru hadi leo lakini hali ndio hiyo tabu kupita maelezo.
Zahanati mbali sana, Shule mbali sana, Maji hakuna.

Kuna jamaa juzi alikuwa anasema anatoka kijiji cha mbali ( mazingara …..) ambako hakuna zahanati mwendo wa kufika Kwamkono kuliko na huduma hiyo ni mbali sana ,
Anakwambia anatoka na mtoto mgongoni anaumwa sana kabla ya kufika hospital mgongoni ukisikia kimyaaa ujue Huna mtoto tena 😭😭😭

Nilisikitika.

Wa mama wajawazito wanabeba na vitanda wakifika njiani uchungu umechanganya wanaume wanaambiwa hebu tupisheni kwanza, anajifungua kienyeji with high risks kishawanaitwa tena wanaume wa bebe na kitanda kurejea nyumbani kwa mwendo mrefu sana.

Halafu walioko mjini wao ni kazi ya uchawa kusifu na kuabudu tu Viongozi , mimi huwa nawaangalia !
 


Takwimu zinaonesha watoto wengi wakike na wakiume wanashindwa kumaliza masomo sababu ya umbali mrefu sana wa Shule ziliko na ulisema wa huduma za Shule za bweni.
Kwa hiyo mtoto anaona kwenda Shule kusoma ni kama adhabu maana utatembea mwendo mrefu kupita kawaida wakati wa kwenda na kurudi.
Ukitoka nyumbani kama umekula kiporo (usiga) kabla ya kufika Shule sababu ya mwendo kinaisha chote ukifika njaa na mzazi uwezo wa kukupa hata shilingi 100 hana.
Eti umsikilize Mwalimu kutwa nzima na njaa Halafu ukitoka Shule uanze kutembea mwendo mrefu kwa masaa kadhaa hadi ufike nyumbani.
Nani anaweza kuvumilia hali hiyo?

Wakike wanaingia tamaa ya lifti za Bodaboda na kuishia kutiwa mimba na kutelekezwa mazima.
 
Imba hivi.....ccm mbere kwa mbere
 
Mkata wachukue maji wami ni mbali,Kuna mto pangani karibu zaidi
Kun kipind maj yalikuw yanatoka korogwe lkn yalikata tunasikia yalishia komkonga, uko upande wa wami tulickia cjui mrad umefika mbwewe lkn n siasa nyingi tu wananchi wanatumia maji na ngo'mbe kwny vibwawa vya kwa Pala na mbweni
 
Ktk Halmashauri zna maisha magumu n handen asee, ndiomana mtt akimalza la saba tu n ndoa chaaap apunguze gharam za maisha Nyumbani.
 
Mkata Kuna chimbo la nyama kweli pale ,au unachanganya na msata
Nyama ipo balaaa ten mbuz utawakimbia, sehem pale panapo park coasta za mbezi, kushoto, kun pale stendi ya tanga ucku hatar, kun njia ya kwend handen mjin, alafu kubwaa kulikooo kun mwamba kafungua mkata highway motel ipo maeneo ya mbweni pale utazikimbiaaa nyamaa
 
Kuna bwawa la mbweni linasambaza maji pale mkata changamoto wenye visima wanajaza mavisima yao yakijaa badala ya kuuza 100 ndoo wanauza 400

Maji yamekuwa miradi ya watu
 
Kuna bwawa la mbweni linasambaza maji pale mkata changamoto wenye visima wanajaza mavisima yao yakijaa badala ya kuuza 100 ndoo wanauza 400

Maji yamekuwa miradi ya watu
Hlo bwawa lenyewe halina maji ya kutosha maji yanaachiwa mara moja kwa mwezi, na wenye visima vya mvua wanawapiga watu ndoo ad 700.
 
 

Attachments

  • IMG_1332.jpeg
    449.9 KB · Views: 1
Kumbe optimism mwanamke?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…