Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,303
Reaction score
23,064
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?


Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
 
Hivi Masters holder akija na wazo wa kufanya biashara kama za Bakhressa kwa lengo la kumfikia bakhlesaa atakuwa mjinga??? Akienda shamba akalima ekali za vitunguuu na kuanza kuzisafirisha nje??? Ulitaka aanze kuzalisha masters zake na kuziuza?
 
cha kwanza hela mkuu,
naskia biashara ya kwanza kwanza kufanywa na Mengi alikuwa anaimport kalamu za Bic kutoka Kenya (biashara ambayo ingefanywa na mtu yoyote mwenye mtaji ) na jamaa alikuwa msomi, angeamua kufanya kazi za wasomi labda leo angekuwa nyumbani baaada ya kutumbuliwa na rais anasubii kupangiwa kazi nyingine
 
Msomi unayemsemea wewe akimbinu mbuni yake nzuri mtaji utampa wewe mkuu?
 
Mimi sioni tatizo akiamua kufanya hata hizo, ila baada ya miaka 5 asiwe kama muuza chips au mlima tikiti wa kawaida.

Sio kila msomi atakua na resource za kumuwezesha kuanzia juu...

msomi na asiyesoma wakiwa wanafanya kitu kimoja nategemea vision na realization zao zitakua tofauti
 
Umenigusa. Nafanya biashara ambayo hata asiesoma anaweza kufanya. Ila jinsi ninavyoifanya mimi na hao wengine ni tofauti kabisa jambo linalofanya nipate wateja wa kudumu kirahisi sana, kwa sababu wateja wengi wa biashara yangu ni wasomi hivyo wanakuwa na amani ku-deal na mtu wanaeongea nae lugha moja.

Ni vigumu sana kufanya jambo jipya ila unaweza kufanya kitu kile kile wanachofanya wengine kwa namna tofauti na bora zaidi,utafanikiwa. Bottom line kinachotakiwa ni kipato kizuri kama biashara ni halali hamna ubaya. Mentality kama hii unayoizungumzia ndio inawagharimu wasomi wengi na kubaki walipo kwasababu wanaona watu kama wewe mtawaonaje.
 
Mkuu,

Suluhisho nimeweka, Tuwaze kufanya vitu kwa utofauti, yani kama ni biashara ya chips basi fanya kama KFC ambayo unafanya tena kwa utofauti, sio unafungua banda la chips kama la mluguru wa pale buguruni
We unajuaje kama mtaji wake unamruhusu kufungua banda kama la huyo mrurguru ila malengo yake baadae aje afungue kama KFC unayosemea?
 
Msomi unayemsemea wewe akimbuni mbuni yake nzuri mtaji utampa wewe mkuu?
Aisee,
Watu wana ela ila hawajui pakuziweka,
kwa mtu ambae ni mjasiriamali na anapenda kufanya hivyo,
akiwa na idea iliyosimama ela zipo mkuu,

watu wanaandika pepa, wanashindanisha idea, wanazipeleka kwa masponser na ena zinamwagaa.

hao akina Zurckeberg na bill Gates hawakuwa na ela, bali walifanya watu wakaona na wakaeka ela
 
Bila chaneli utaishia kujaza mapepa gheto ya kutosha bongo siyo kama mbele
 
Hakika mkuu,
Ila inashangaza mtu na elimu yako,
umekopa mkopo bank, alafu unaenda fungua juisi ya miwa kama mpemba wa ilala,
mazingira ya kizwasi, yani vuluvulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…