Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Hivi Masters holder akija na wazo wa kufanya biashara kama za Bakhressa kwa lengo la kumfikia bakhlesaa atakuwa mjinga??? Akienda shamba akalima ekali za vitunguuu na kuanza kuzisafirisha nje??? Ulitaka aanze kuzalisha masters zake na kuziuza?
Yes,
bora huyo anayewaza kusafirisha nje,

sio yule anelima na kumpelekea dalali pale mabibo

ndipo mada yangu ilipo
 
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?

Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
Kama zipi Mkuu
 
Kwanza kabisa kabla ya kulalamika, Je unaijua Education System tunayotumia Tanzania?
Je unajua Mtanzania huanza kujiwekea akiba kwa malengo yake ya badaye akiwa na umri gani?
KUMBUKA PIA HILI SI JANGA LA TANZANIA PEKE YAKE.
 
Niliwahi kuandika uzi humu, mtu anasoma shule expensive, Feza hadi Havard. Halafu wanakuja kufanya kazi na mimi niliyesoma shule ya kata chuo Theofilia kisanji.
Katumia milioni 700 kusoma, mimi nimetumia milioni 10 kusoma, lakini tunafanya kazi ofisi moja kazi ileile, na tena mimi namsaidia.
Kwanini usome havard urudi bongo, pambana na heavy weight wenzako.
 
Yes,
bora huyo anayewaza kusafirisha nje,

sio yule anelima na kumpelekea dalali pale mabibo

ndipo mada yangu ilipo
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Anaweza kuanza kumpelekea dalali hapo mabibo few years down the line anapeleka nje. Hujui watu wanafikiria nini dont judge.

Btw wewe ni mfanyabiashara hebu tuambie unafanyaje?
 
Mkuu ndo maana ya kupelekwa shule,
umiza ubongo ujue nini cha kufanya
Kikwazo kikubwa ni mitaji, vijana wengi hawana mitaji ya kutosha, pia kuna taaluma ambazo lazima uwe umesajilwa na professional bodies mfano kijana aliyemaliza shahada ya uhasibu haruhusiwi kabisa kufanya kazi kama mshauri wa kodi au kazi za kuandaa hesabu za makampni au watu binafsi kama hajasajiliwa na Bodi ya uhasibu kwa maana lazima awe na chati cha CPA na awea amefanya kazi chini ya ungalizi kwa miaka mitatu, mlolongo huo wote unahitaji pesa na muda ni kikwazo kwa vijana.
 
Mimi sioni tatizo akiamua kufanya hata hizo, ila baada ya miaka 5 asiwe kama muuza chips au mlima tikiti wa kawaida.

Sio kila msomi atakua na resource za kumuwezesha kuanzia juu...

msomi na asiyesoma wakiwa wanafanya kitu kimoja nategemea vision na realization zao zitakua tofauti

nimeipenda signature yako Chinchilla coat!!😳
 
Kikwazo kikubwa ni mitaji, vijana wengi hawana mitaji ya kutosha, pia kuna taaluma ambazo lazima uwe umesajilwa na professional bodies mfano kijana aliyemaliza shahada ya uhasibu haruhusiwi kabisa kufanya kazi kama mshauri wa kodi au kazi za kuandaa hesabu za makampni au watu binafsi kama hajasajiliwa na Bodi ya uhasibu kwa maana lazima awe na chati cha CPA na awea amefanya kazi chini ya ungalizi kwa miaka mitatu, mlolongo huo wote unahitaji pesa na muda ni kikwazo kwa vijana.
Mkuu,
kama hujawahi fanya biashara hata ya karanga,hata tukikupa million 100 zitapukutika tu,

tatizo sio mtaji, tatizo hatuna mawazo solid, hatuwazi kufikiri kufanya vitu kwa utofauti
 
Mimi nafikiri wasomi wangekuja na mawazo ili tujikwanue zaidi juu ya uzalishaji. Kwa nini uzalishaji iwe ni hasara tu?
Jingine la muhimu ni siasa. Siasa iwekwe mbali kwenye masuala yanayohitaji usomi, biashara ikiwamo.
Pengine wanaishia kufanya biashara za kawaida kutokana na hasara sio kubwa, na wanayaendesha bila ya kuonesha tofauti, kwa sababu nchi yetu ukionesha tofauti na ukafanikiwa, wanasiasa ni adui wako.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Anaweza kuanza kumpelekea dalali hapo mabibo few years down the line anapeleka nje. Hujui watu wanafikiria nini dont judge.

Btw wewe ni mfanyabiashara hebu tuambie unafanyaje?
Watu wasomi, gena wa fani za ukulima,
nina wajua,
wanalima miaka 10 sasa,
hakuna jipya Zaidi ya kufanya katika mfumo huu huu wa udalali
 
Umegusa sehemu ambayo naiwaza kila siku kuiandika humu jamvini,, Swala la wasomi kufanya kazi za kishenzi au ambazo hazina hadhi ya elimu walizonazo... hili linaonyesha dhahiri kuwa walikuwa na mategemezi mengine wakati wakiwa madarasani... Ajira bongo ni ndoto za mchana na cha ushauri ni kujiongeza zaidi kusogea kuomba kazi nchi za jirani kama wenzangu mmebarikiwa kuwa na vyeti vilivyoshiba..
 
mkuu nchi zipi hizo..
 
Umenigusa. Nafanya biashara ambayo hata asiesoma anaweza kufanya. Ila jinsi ninavyoifanya mimi na hao wengine ni tofauti kabisa jambo linalofanya nipate wateja wa kudumu kirahisi sana, kwa sababu wateja wengi wa biashara yangu ni wasomi hivyo wanakuwa na amani ku-deal na mtu wanaeongea nae lugha moja.

Ni vigumu sana kufanya jambo jipya ila unaweza kufanya kitu kile kile wanachofanya wengine kwa namna tofauti na bora zaidi,utafanikiwa. Bottom line kinachotakiwa ni kipato kizuri kama biashara ni halali hamna ubaya. Mentality kama hii unayoizungumzia ndio inawagharimu wasomi wengi na kubaki walipo kwasababu wanaona watu kama wewe mtawaonaje.

Nimejifunza hapa wacha nibadilike
 
Aisee,
Watu wana ela ila hawajui pakuziweka,
kwa mtu ambae ni mjasiriamali na anapenda kufanya hivyo,
akiwa na idea iliyosimama ela zipo mkuu,

watu wanaandika pepa, wanashindanisha idea, wanazipeleka kwa masponser na ena zinamwagaa.

hao akina Zurckeberg na bill Gates hawakuwa na ela, bali walifanya watu wakaona na wakaeka ela[/colour]
Maliza chuo kwanza halafu ndio uje uongee na wanamume.

Au kama unaishi nyumbani, nakushauri usihame ukuekue kwanza kiakili.

Sikutishi.
 
Back
Top Bottom