Ni aibu na ni Ujinga kupeperusha picha ya Rais kwenye uwanja wenye Taa mbovu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Tulionya tangu awali na tunaendelea kuonya tena kwamba , mashabiki wajinga wanaoingia uwanjani na Picha ya Rais wakatazwe ,

Hii ni kwa sababu Rais wa Nchi hii hakuwahi kuwa Mwanasoka na wala hakuwahi hata kupiga danadana , na wala sikumbuki siku aliyowahi kuingia uwanjani kushuhudia soka , kama wabeba picha wanazibeba kwa vile Rais ananunua magoli basi wanapaswa kujiuliza kama hela za kununua magoli hayo anazitoa mfukoni mwake au la

Michezo ndio sehemu pekee inayokutanisha watu wenye itikadi tofauti , kuanzia wachezaji , mashabiki na watazamaji , maana usione wachezaji wanachezea Timu ya Taifa basi ukadhani wote ni ccm , sasa kuanza kumpigia debe Mwenyekiti wa CCM kwenye soka ya umma mtachafua hali ya hewa

Jitahidini kushangilia soka bila kuleta siasa za kijinga , Hatutakubali na iko siku kitanuka .

Tabia hii ya Kishamba inaweza kuwa sababu ya kuitia gundu Taifa Stars Kushindwa kufanikiwa .

TUHESHIMIANE .
 
Tulionya tangu awali na tunaendelea kuonya tena kwamba , mashabiki wajinga wanaoingia uwanjani na Picha ya Rais wakatazwe ,
Siungi mkono ushamba wa watu kujibebesha mizigo isiyo na tija ila sikuungi mkono kabisa wewe..., hayo mambo ya kukataza na kupangiana maisha kwa lugha ya kigeni yanaitwa Dictatorship....

To each his/her own.....
 
hueleweki unasimamia nini , uzi wangu uko wazi kabisa , hakuna udikteta ni tahadhari
 
Kusimamia nini kuhusu nini ? Unasema watu wakatazwe hio ni tahadhari ? Au kupangiana ?

Michezo ndio sehemu pekee inayokutanisha watu wenye itikadi tofauti , kuanzia wachezaji , mashabiki na watazamaji , maana usione wachezaji wanachezea Timu ya Taifa basi ukadhani wote ni ccm , sasa kuanza kumpigia debe Mwenyekiti wa CCM kwenye soka ya umma mtachafua hali ya hewa

Jitahidini kushangilia soka bila kuleta siasa za kijinga , Hatutakubali na iko siku kitanuka .

Wewe na wao wote ni walewale
 
Back
Top Bottom