Ni aibu timu kubwa kama Yanga kwenda kutumia uwanja wa Azam Fc

Ni aibu timu kubwa kama Yanga kwenda kutumia uwanja wa Azam Fc

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Hivi hizi timu kongwe za Tanzania, Simba na Yanga zitaacha lini kudeka nakupenda kutumia rasilimali za wengine.

Inatia aibu na huruma pale timu kongwe kama Yanga yenye miaka zaidi ya 80 toka kuanzishwa kwake kutumia uwanja wa Azam Fc ya mwaka 2007.

Ni aibu kubwa kwa wana Yanga wenzangu sijui hata tuweke wapi sura zetu!

Povu ruksa...
 
Niliwahi kutoa wazo, Simba na Yanga na mashabiki wao wakiacha ujinga wangeweza kujenga uwanja wa pamoja. Ni rahisi kudhaminika kwa pamoja kuliko mmojammoja
 
Simba na Yanga maneno mengi kama waimba taarabu, vitendo ziro!!!!!

Yanga kumfunga Simba na Simba kumfunga Yanga hayo ndio wanaona ni mafanikio!!!!
Mkuu umeongea kitu ki kubwa sana. Na hizo timu za Kariakoo ndio mzizi wa kubemendwa kwa Soka letu!
 
moja ya team hopeless nadhani hizi zinaongoza...

cha ajabu mashabiki wake wanasifia kufungana tu huku club hazina maendeleo
Kweli mkuu. Washabiki wa timu hizi wengi mashabiki wa Chama chetu.
 
Watanzania tunatakiwa tubadilike sio kila kukicha eti simba mara sijui yanga.

Tuiunge mkono timu ya AZAM FC,,,,tuachane na USIMBAYANGA
Ni kweli. Upo sahihi. Watanzania tuzipe nguvu timu zetu za mikoani. MCC, MBAO, SINGIDA FC, NJOMBE, hizi zinaweza kutuvusha km tutazipa support!
 
Hivi hizi timu kongwe za Tanzania, Simba na Yanga zitaacha lini kudeka nakupenda kutumia rasilimali za wengine.

Inatia aibu na huruma pale timu kongwe kama Yanga yenye miaka zaidi ya 80 toka kuanzishwa kwake kutumia uwanja wa Azam Fc ya mwaka 2007.

Ni aibu kubwa kwa wana Yanga wenzangu sijui hata tuweke wapi sura zetu!

Povu ruksa...
miradi ya watu.na ukija kugundua unaona kila siku ndio timu ambazo zina ingiza mapato mengi.katika mechi zao
 
Back
Top Bottom