Ni aibu timu kubwa kama Yanga kwenda kutumia uwanja wa Azam Fc

Ni aibu timu kubwa kama Yanga kwenda kutumia uwanja wa Azam Fc

Ni kweli. Upo sahihi. Watanzania tuzipe nguvu timu zetu za mikoani. MCC, MBAO, SINGIDA FC, NJOMBE, hizi zinaweza kutuvusha km tutazipa support!
Hili haliwezekani.........kila mtoto anayezaliwa ni ama simba au yanga! Amini usiamini!
Nadhani umenielewa!
 
Hivi hizi timu kongwe za Tanzania, Simba na Yanga zitaacha lini kudeka nakupenda kutumia rasilimali za wengine.

Inatia aibu na huruma pale timu kongwe kama Yanga yenye miaka zaidi ya 80 toka kuanzishwa kwake kutumia uwanja wa Azam Fc ya mwaka 2007.

Ni aibu kubwa kwa wana Yanga wenzangu sijui hata tuweke wapi sura zetu!

Povu ruksa...
Tuepuke kukariri kwa sababu tu wanaojiita wachambuzi wanakariri. Nani wa kujenga viwanja vya michezo, wapi na lini si swala linaloanza na kumalizia na vilabu. Ni swala la sera, kanuni na sheria za nchi kwanza. Nani alikuwapo nchi hii wakati Yanga na Simba zinaanzishwa atuhakikishie kwamba ilikuwa ni sera ya Wakoloni kuwezesha viwanja vya michezo kwa ngazi ya vilabu vya Waafrika, enzi ambazo viwanja vikubwa pekee kwa nchi nzima kitaifa vilikuwa ni Ilala (Karume) na baadaye Uhuru? Nani anakumbuka enzi za kupata Uhuru atuhakikishie kwamba sera ya zama hizo za Azimio la Arusha ilikuwa ni vilabu kuwa na viwanja vya michezo na si kila Mkoa kuwa na kiwanja chake? Atuambie iwapo usingekuwa usaliti kwa Timu ya Majimaji kudai umiliki wa kiwanja ambacho Mkoa ulikipa jina moja na timu hiyo? Angalau ningekubaliana na watakaozilaumu timu hizi kwa kutofanya hivyo tangu enzi za uchumi huria (1985) kuanza. Lakini kama mchakato wa mageuzi kwa Yanga na Simba kwenye Karne hii ya 21unasuasua hivi kwa kuendekeza woga wa mabadiliko, siasa na ulafi, ingewezakanaje kwenye Karne hiyo ya 20? Sera hizi za Ruksa na biashara huria ndizo zilizoiwezesha Azam kuwa na kiwanja chake. La sivyo TPC, Pilsner, Sigara, Magunia, Tumbaku, Mwadui (ya enzi hizo), Reli, General Tyre, n.k. zingejenga viwanja vyao kama fursa ya uchumi huria na ya Wazalendo kujiamulia zingekuwapo enzi zao. Wanaodhani Mwadui, General Tyre na kama hizo zina viwanja, wasibishe kuwa Yanga na Simba zina viwanja Jangwani. Wanaolaumu timu hizi kwa kukosa viwanja, wazisifie Cosmopolitans, Nyota Nyekundu, Mseto, Pilsner, Kiltex, Kajumulo na kama hizo kwa kutoweka kwenye ulimwengu wa soka licha ya uchanga wao dhidi ya Yanga na Simba. Kisha watoke nje ya mipaka ya Tanzania wakazisifie Gor Mahia, Reunion, AFC Leopards, Express, n.k. kwa kuwa na mafanikio zaidi ya Yanga na Simba kwa kuwa zina viwanja vyao na kuchukua makombe ya Afrika ya Mashariki na Kati mara chache zaidi kuliko Yanga na Simba. Wazisifie kwa mtindo wao wa kutoweka na kurejea kwao kwenye utawala wa soka la nchi zao ilhali Yanga na Simba zimeshindwa kutoweka kwenye Daraja la juu la Ligi ya nchi hii tangu imeanzishwa.
Hivi mnataka kutuambia kuwa Azam ingeanzishwa zama moja na Yanga na Simba ingekuwa imeshafikia ilipofikia Mazembe hii leo, Azam ambayo licha ya bahati ya kuepukana na changamoto za watangulizi hao lakini bado inaendeshwa kifikra (na damu) hizohizo za Simba na Yanga? Labda kichaa ndiye atafikiria hivyo!
 
TFF wanaewadekeza hawa futa kwa ligi kuu hadi wajenge uwanja
 
Hivi siku hizi bado kuna mambo ya ushabiki damdam wa Simba na yanga naona hiZi team zimehamia kwenye music na siasa
 
Mnaongea kama mazuzu...mnakumbuka Jangwani city ?Manji alitaka kujenga uwanja unaojaza watu 60,000 .Manispaa ya Ilala ikanyima kibali cha ujenzi kwa mambo yao ya siasa...kama hujui kitu nyamaza
NB:mnajuwa Manji ni tajiri kuliko Bakhresa tofauti mmoja anauza chakula mwingine technology(TIGO)
 
Back
Top Bottom