Ni asilimia ngapi kwa mwezi unatakiwa kuanza kuipata unapoanza kufanya biashara kwa mtaji ulionao?

Ni asilimia ngapi kwa mwezi unatakiwa kuanza kuipata unapoanza kufanya biashara kwa mtaji ulionao?

Abdul Mganyizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2019
Posts
1,042
Reaction score
2,005
Ndugu zangu kama kichwa cha habari kinavyojieleza. Naomba kujua ukiwia unamtaji wako wa kiwango chochote cha pesa, unatakiwa upate kiasi gani cha faida kwa mwezi kwa mahesabu ya asilimia?

Wengine wanasema minimum angalau upate 20% ya mataji kwa mwezi, wengne wanasema 30% kwa mwezi ndio utasema hiyo biashara inafaa maeneo hayo.

Wafanya biashara na wachumi nisaidieni.
 
Kweli ukiwaza faida utakuwa unagusa gusa kila kitu halafu biashara zina probation period kipindi cha kutengeneza wateja na kufahamika ndio maana wenye uwezo wanakipunguza makali hiki kipindi kwa kupitia matangazo kwenye Media!

Ila ukikomaa kimya kimya ndio kipindi kigumu sana ambacho watu hukata tamaa maana biashara ina struggle na inaweza ikakata mtaji kabisa!
 
Wewe sio mfanyabiashara ndugu jaribu jambo lingine! Unauliza faida ya Biashara kabla ya kuanza, inamaana unaogopa sana hasara akili yako iko kwene faida tu! Faida ya mtu inategemea na aina ya Biashara na uhitaji kwa wateja wake kuna faida unapiga adi 50
 
Shukrani

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Inategemeana na biashara.

Wanaonjenga nyumba faida zinaanza kupatikana baada ya hata miaka 10
 
Faida ni faida tu, hata kama ni kidogo cha msingi ni kuwa na biashara nyingi ili zibalance maisha
 
Nahisi amejikita zaidi kwenye biashara mpya?

Kama jibu ni ndio hapa inakuwa ngumu sana kujua faida yake maana kama ni mpya kuna muda wa kutengeneza wateja hapa itategemea sana na demand ya wateja wako na location.

Kuna baadhi ya biashara ukishakuwa na wateja na kutokana na demand nitakuletea faida ya 100%.
 
Inategemea na idadi ya wateja kama wateja watakuwa wengi faida utaiona
 
Back
Top Bottom