Ahsante mkuu Mawado,
Kama alivyosema mkuu, jina kamili la kale lilikuwa Bwagamoyo, ila jina lilibadishwa kidogo kidogo hadi likawa Bagamoyo badala ya Bwagamoyo!
Tofauti ni kuwa katika miaka mingi ya nyuma niliwahi kujulishwa Mwalimu wangu mwenyeji wa Bwagamoyo (ni marehemu kwa muda mrefu sasa, na pia namwombea Muumba amlaze mahala pema peopni) kuwa paliitwa Bwagamoyo kwa uzuri, na jinsi ambavyo ukifika hiyo sehemu una relax, na mawazo yote yanakuishi ukipata upepo mwanana wa mwambao, na kujishtukia tu moyo wako, shida zako na mawazo yako umeyabwaga hapo hapo kwa kuridhishwa tu na man dhari nzuri na upepo mwanana wa pwani hiyo ya Afrika!
Pia alitutaarifu (sisi wanafunzi wake) kuwa hata hao wazungu waliridhika na hilo jina, kwani hata wao walipapenda na kuanza kupajenga, na kwa kushindwa kutamka Bwagamoyo wakapaita Bagamoyo, na watu weusi tupendavyo kuiga ikawa nongwa, nasi tukaiga lafudhi yao na kupaita bagamoyo!
Ahsanteni, niliona ni bora nami nitoe machache niliyojulishwa na huyo mzee wetu ambaye kwa sasa ametangulia mbele ya haki.